Yahya Mohamed
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 270
- 317
Mapendekezo: Mchakato wa Upatikanaji wa Katiba Mpya uweje? Ni dhahiri katiba mpya haiepukiki kwa sasa. Utaratibu upi utasaidia kupatikana Katiba itakayokidhi mahitaji ya Watanzania.
Shiriki katika mjadala huu kwa maoni yako ikiwa ni sehemu ya pili na ya mwisho mpaka hapo utakapoandaliwa tena mjadala huu.
Wageni waalikwa wanatarajiwa kuwa wahadhiri wa Kitivo cha sheria kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino na bado jitihada zinafanyika kumpata Jaji Mstaafu Joseph Warioba Jijini DSM. Profesa Shivji yupo Nje ya Nchi.
Ndugu yahya wewe ni makini pamoja na star tv, kiujumla inaonesha mnataka kuweka legacy sahihi ya itv, kwanza nishukuru kwamba ulisoma mchango wangu kuhusu kwanini tunahitaji katiba mpya bila uchakachuaji ingawaje hukusoma maoni yangu kuhusu kombani -waziri. Okay kuhusu mjadala wa mchakato wa katiba mpya uweje, mimi maoni yangu ni kama ifuatavyo
1. Serikali iunde tume ya kuandaa rasimu ya katiba mpya-tume hii iwe na wawakilishi walioteuliwa na vyama vya siasa kutoka vyama vyao, wawakilishi kutoka bakwata, tec, cct, sabato, yaani dini, mwakilishi kutoka civil society, mwawakilishi kutoka vyuo vikuu, mwakilishi kutoka law society, mwakilishi kutoka haki za binadamu, mwakilishi kutoka mahakama, na mwakilishi kutoka balaza la watoto na vijana, mwakilishi kutoka media na baraza la habari, katika tume hii awemo jenerali ulimwengu, prof issa shivji, jaji amir manento,dr lwaitama, deus kibamba na ayoub lioba.
2. Tume hii ifanye uchambuzi yakinifu na kwa kukutana na vikundi mbalimbali ili iweze kutengeneza rasimu ya katiba mpya
3. Ikishatengeneza rasimu ya katiba mpya iweke hadharani rasimu hiyo ya katiba mpya kwa muda wa miezi sita wananchi kuijadili na kutoa mapendekezo yao
4. Ikishamaliza kupokea mapendekezo ya watanzania wote itengeneze final draft for preresentaion ipeleke kwa kamati ya bunge kwa ajili ya mapitio na mapendekezo.
5. Bunge lipewe nafasi yake kujadili na kutoa mapendekezo ya mwisho kabla ya kuifanya kuwa sheria.---angalizo bunge lisifanye maamuzi ya katiba kwa kupiga kura za kichama badala yake kamati ya bunge na tume vifanyie kazi mapendekezo ya bunge kabla ya kuipitisha.
6. Watawala wasiingilie mchakato huu manake katiba ya nchi inatakiwa kuwa huru na sustainable yaani tufikirie kuibadaili baada ya miika 50 mpaka 100 ijayo.
7. Tume isiwe ya watu wenye njaaaaaaaaa kali ndio maana nimependekeza kwa maoni yangu baadhi ya watu wanojua nini maana ya katiba.
8. Wananchi washirikishwe kutoa maoni wanachotaki kibadilike tukumbuke elimu ya uraia ni utata lakini kwa tume hiyo inawezekana kupata maoni yao, ni uzandiki eti kuwaambia watanzania tubadili au tusibadili wakati wengi wao hawaijui,
9. Tume hiyo iwe huru na uhuru uonekane siyo kama nec -tume pandikizi. Tume iwajibike kwa watanzania wa sasa na kesho
10. Mwisho star tv nawapa big up kama ninanvyo wafagilia mwanahalisi, raia mwema, tz daima na mwananchi
Yahya, naomba mkiweza fanya kuwapata japo kwa dakika mbilimbili au tatutatu kila mmoja:
Dr. Slaa & Prof. Lipumba
Kiongozi wa kidini yeyote toka wakristo na kiislam,
Waziri Kombani
Jenerali Ulimwengu
Kisha mwendelee na discussion yenu na wageni waalikwa ili mnapojadiliana hao wageni watoe mitizamo yao kuhusiana na kauli za niliowapendekeza (the list can be modified). Mnaweza kuwa-record hawa mapema ili kuepusha muda wenu kupitiliza (editing inaweza kufanyika ili kuzingatia hoja zaidi bila kuchakachua).
So far, nice move!
yahaya, big up and endelea kutu update kupitia humu jamvini wakati wa kipindi hicho ili na sisi tupate kujua nini kitakacho kua kinaendelea huko.
Katika Mjadala wenu wafahamishe wananchi haya.
1.Ni nani hasa mwenye uamuzi wa mwisho wa kuamua kama tuwe na katiba mpya au La.
Hii itasaidia kujua hata mtu/watu/kundi la kudili nalo badala ya kuongea tu kama vile tunapiga kelele
Inawezekana tunamlenga mtu fulani hivyo kama yuko nje ya nchi tusubiri akirtudi tumueleze kiu yetu ya katiba mpya
Pia Yahya na star tv nawapongeza kwa utartibu huu wa kutumia New media katika uandaaji wa vipindi vyenu lakini nashauri mfanye kama wenzetu nje CNN,BBC na Aljazeera kama mnaweweza ,fanya mjadala huo wa studio na ule wa interenet hasa kwenye thread yako viendane sawa wakati wa kuchangia.
ingawa hapa kuna changamoto ya mtandao ,vifaa nk lakini pole pole tutafika
napongeza kwa ufanisi katika fani
Byabato
Tatizo lenu mnaalika wageni ambao mitazamo yao tayari inajulikana sasa utapataje mawazo ya upande mwingine? haya mwalikeni huyo warioba aongee tunachokifahamu tufurahi halafu maisha yaendelee! democracy haijengwi hivyo wazee!
Mapendekezo: Mchakato wa Upatikanaji wa Katiba Mpya uweje? Ni dhahiri katiba mpya haiepukiki kwa sasa. Utaratibu upi utasaidia kupatikana Katiba itakayokidhi mahitaji ya Watanzania..
Henge nakubalian na wewe. Lakini ukweli ni kwamba Zanzibar wao wana katiba yao ambayo tayari wameipitisha. Utaona ukweli ni kwamba katiba hii tunayoizungumzia ni kama ni ya Tanganyika. Kwani umeshasikia Zanzibar wanajishughulisha na jambo hili? Kilio chote kiko kwa watanganyika.Mkuu mjadala uliopita niliufuatilia vizuri sana, na nawapongeza sana mjadala ulikuwa mzuri! Mkuu tunaweza kumpata mtu toka tanzania visiwani kuleta usawa naona kama tunajadili katiba ya tanganyika wakati hii ni tanzania.