This Sunday LIVE on Star TV 19th DEC

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Mapendekezo: Mchakato wa Upatikanaji wa Katiba Mpya uweje? Ni dhahiri katiba mpya haiepukiki kwa sasa. Utaratibu upi utasaidia kupatikana Katiba itakayokidhi mahitaji ya Watanzania.

Shiriki katika mjadala huu kwa maoni yako ikiwa ni sehemu ya pili na ya mwisho mpaka hapo utakapoandaliwa tena mjadala huu.

Wageni waalikwa wanatarajiwa kuwa wahadhiri wa Kitivo cha sheria kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino na bado jitihada zinafanyika kumpata Jaji Mstaafu Joseph Warioba Jijini DSM. Profesa Shivji yupo Nje ya Nchi.
 
nafikiri ingependeza kama ungealika na viongozi wa dini maana hili suala muhimu kwa watz wote bila iman wa itikadi.
 
Ndugu yahya wewe ni makini pamoja na star tv, kiujumla inaonesha mnataka kuweka legacy sahihi ya itv, kwanza nishukuru kwamba ulisoma mchango wangu kuhusu kwanini tunahitaji katiba mpya bila uchakachuaji ingawaje hukusoma maoni yangu kuhusu kombani -waziri. Okay kuhusu mjadala wa mchakato wa katiba mpya uweje, mimi maoni yangu ni kama ifuatavyo

1. Serikali iunde tume ya kuandaa rasimu ya katiba mpya-tume hii iwe na wawakilishi walioteuliwa na vyama vya siasa kutoka vyama vyao, wawakilishi kutoka bakwata, tec, cct, sabato, yaani dini, mwakilishi kutoka civil society, mwawakilishi kutoka vyuo vikuu, mwakilishi kutoka law society, mwakilishi kutoka haki za binadamu, mwakilishi kutoka mahakama, na mwakilishi kutoka balaza la watoto na vijana, mwakilishi kutoka media na baraza la habari, katika tume hii awemo jenerali ulimwengu, prof issa shivji, jaji amir manento,dr lwaitama, deus kibamba na ayoub lioba.

2. Tume hii ifanye uchambuzi yakinifu na kwa kukutana na vikundi mbalimbali ili iweze kutengeneza rasimu ya katiba mpya

3. Ikishatengeneza rasimu ya katiba mpya iweke hadharani rasimu hiyo ya katiba mpya kwa muda wa miezi sita wananchi kuijadili na kutoa mapendekezo yao

4. Ikishamaliza kupokea mapendekezo ya watanzania wote itengeneze final draft for preresentaion ipeleke kwa kamati ya bunge kwa ajili ya mapitio na mapendekezo.

5. Bunge lipewe nafasi yake kujadili na kutoa mapendekezo ya mwisho kabla ya kuifanya kuwa sheria.---angalizo bunge lisifanye maamuzi ya katiba kwa kupiga kura za kichama badala yake kamati ya bunge na tume vifanyie kazi mapendekezo ya bunge kabla ya kuipitisha.

6. Watawala wasiingilie mchakato huu manake katiba ya nchi inatakiwa kuwa huru na sustainable yaani tufikirie kuibadaili baada ya miika 50 mpaka 100 ijayo.

7. Tume isiwe ya watu wenye njaaaaaaaaa kali ndio maana nimependekeza kwa maoni yangu baadhi ya watu wanojua nini maana ya katiba.

8. Wananchi washirikishwe kutoa maoni wanachotaki kibadilike tukumbuke elimu ya uraia ni utata lakini kwa tume hiyo inawezekana kupata maoni yao, ni uzandiki eti kuwaambia watanzania tubadili au tusibadili wakati wengi wao hawaijui,

9. Tume hiyo iwe huru na uhuru uonekane siyo kama nec -tume pandikizi. Tume iwajibike kwa watanzania wa sasa na kesho

10. Mwisho star tv nawapa big up kama ninanvyo wafagilia mwanahalisi, raia mwema, tz daima na mwananchi
 
Katika Mjadala wenu wafahamishe wananchi haya.
1.Ni nani hasa mwenye uamuzi wa mwisho wa kuamua kama tuwe na katiba mpya au La.
Hii itasaidia kujua hata mtu/watu/kundi la kudili nalo badala ya kuongea tu kama vile tunapiga kelele

Inawezekana tunamlenga mtu fulani hivyo kama yuko nje ya nchi tusubiri akirtudi tumueleze kiu yetu ya katiba mpya

Pia Yahya na star tv nawapongeza kwa utartibu huu wa kutumia New media katika uandaaji wa vipindi vyenu lakini nashauri mfanye kama wenzetu nje CNN,BBC na Aljazeera kama mnaweweza ,fanya mjadala huo wa studio na ule wa interenet hasa kwenye thread yako viendane sawa wakati wa kuchangia.

ingawa hapa kuna changamoto ya mtandao ,vifaa nk lakini pole pole tutafika

napongeza kwa ufanisi katika fani

Byabato
 
Mapendekezo: Mchakato wa Upatikanaji wa Katiba Mpya uweje? Ni dhahiri katiba mpya haiepukiki kwa sasa. Utaratibu upi utasaidia kupatikana Katiba itakayokidhi mahitaji ya Watanzania.

Shiriki katika mjadala huu kwa maoni yako ikiwa ni sehemu ya pili na ya mwisho mpaka hapo utakapoandaliwa tena mjadala huu.

Wageni waalikwa wanatarajiwa kuwa wahadhiri wa Kitivo cha sheria kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino na bado jitihada zinafanyika kumpata Jaji Mstaafu Joseph Warioba Jijini DSM. Profesa Shivji yupo Nje ya Nchi.

Tatizo lenu mnaalika wageni ambao mitazamo yao tayari inajulikana sasa utapataje mawazo ya upande mwingine? haya mwalikeni huyo warioba aongee tunachokifahamu tufurahi halafu maisha yaendelee! democracy haijengwi hivyo wazee!
 
yahaya, big up and endelea kutu update kupitia humu jamvini wakati wa kipindi hicho ili na sisi tupate kujua nini kitakacho kua kinaendelea huko.
 
Yahya, naomba mkiweza fanya kuwapata japo kwa dakika mbilimbili au tatutatu kila mmoja:

Dr. Slaa & Prof. Lipumba
Kiongozi wa kidini yeyote toka wakristo na kiislam,
Waziri Kombani
Jenerali Ulimwengu

Kisha mwendelee na discussion yenu na wageni waalikwa ili mnapojadiliana hao wageni watoe mitizamo yao kuhusiana na kauli za niliowapendekeza (the list can be modified). Mnaweza kuwa-record hawa mapema ili kuepusha muda wenu kupitiliza (editing inaweza kufanyika ili kuzingatia hoja zaidi bila kuchakachua).

So far, nice move!
 
Ndugu yahya wewe ni makini pamoja na star tv, kiujumla inaonesha mnataka kuweka legacy sahihi ya itv, kwanza nishukuru kwamba ulisoma mchango wangu kuhusu kwanini tunahitaji katiba mpya bila uchakachuaji ingawaje hukusoma maoni yangu kuhusu kombani -waziri. Okay kuhusu mjadala wa mchakato wa katiba mpya uweje, mimi maoni yangu ni kama ifuatavyo

1. Serikali iunde tume ya kuandaa rasimu ya katiba mpya-tume hii iwe na wawakilishi walioteuliwa na vyama vya siasa kutoka vyama vyao, wawakilishi kutoka bakwata, tec, cct, sabato, yaani dini, mwakilishi kutoka civil society, mwawakilishi kutoka vyuo vikuu, mwakilishi kutoka law society, mwakilishi kutoka haki za binadamu, mwakilishi kutoka mahakama, na mwakilishi kutoka balaza la watoto na vijana, mwakilishi kutoka media na baraza la habari, katika tume hii awemo jenerali ulimwengu, prof issa shivji, jaji amir manento,dr lwaitama, deus kibamba na ayoub lioba.

2. Tume hii ifanye uchambuzi yakinifu na kwa kukutana na vikundi mbalimbali ili iweze kutengeneza rasimu ya katiba mpya

3. Ikishatengeneza rasimu ya katiba mpya iweke hadharani rasimu hiyo ya katiba mpya kwa muda wa miezi sita wananchi kuijadili na kutoa mapendekezo yao

4. Ikishamaliza kupokea mapendekezo ya watanzania wote itengeneze final draft for preresentaion ipeleke kwa kamati ya bunge kwa ajili ya mapitio na mapendekezo.

5. Bunge lipewe nafasi yake kujadili na kutoa mapendekezo ya mwisho kabla ya kuifanya kuwa sheria.---angalizo bunge lisifanye maamuzi ya katiba kwa kupiga kura za kichama badala yake kamati ya bunge na tume vifanyie kazi mapendekezo ya bunge kabla ya kuipitisha.

6. Watawala wasiingilie mchakato huu manake katiba ya nchi inatakiwa kuwa huru na sustainable yaani tufikirie kuibadaili baada ya miika 50 mpaka 100 ijayo.

7. Tume isiwe ya watu wenye njaaaaaaaaa kali ndio maana nimependekeza kwa maoni yangu baadhi ya watu wanojua nini maana ya katiba.

8. Wananchi washirikishwe kutoa maoni wanachotaki kibadilike tukumbuke elimu ya uraia ni utata lakini kwa tume hiyo inawezekana kupata maoni yao, ni uzandiki eti kuwaambia watanzania tubadili au tusibadili wakati wengi wao hawaijui,

9. Tume hiyo iwe huru na uhuru uonekane siyo kama nec -tume pandikizi. Tume iwajibike kwa watanzania wa sasa na kesho

10. Mwisho star tv nawapa big up kama ninanvyo wafagilia mwanahalisi, raia mwema, tz daima na mwananchi

Thanks DENYO Mchango Umefika.
 
Yahya, naomba mkiweza fanya kuwapata japo kwa dakika mbilimbili au tatutatu kila mmoja:

Dr. Slaa & Prof. Lipumba
Kiongozi wa kidini yeyote toka wakristo na kiislam,
Waziri Kombani
Jenerali Ulimwengu

Kisha mwendelee na discussion yenu na wageni waalikwa ili mnapojadiliana hao wageni watoe mitizamo yao kuhusiana na kauli za niliowapendekeza (the list can be modified). Mnaweza kuwa-record hawa mapema ili kuepusha muda wenu kupitiliza (editing inaweza kufanyika ili kuzingatia hoja zaidi bila kuchakachua).

So far, nice move!

Yes Invisible, Tulikuwa na wazo moja kwa bahati mbaya kutokana na majukumu baadhi ya viongozi uliowataja tulifikiria kuwahoji mapema ila kutokana na majukumu yaliyowabana ths week hatujafanikiwa. Ila onrecord tayari yupo MhJ.Cheyo, J.Ulimwengu & A.Rioba.
Jitihada zinaendelea
Yahya
 
Katika Mjadala wenu wafahamishe wananchi haya.
1.Ni nani hasa mwenye uamuzi wa mwisho wa kuamua kama tuwe na katiba mpya au La.
Hii itasaidia kujua hata mtu/watu/kundi la kudili nalo badala ya kuongea tu kama vile tunapiga kelele

Inawezekana tunamlenga mtu fulani hivyo kama yuko nje ya nchi tusubiri akirtudi tumueleze kiu yetu ya katiba mpya

Pia Yahya na star tv nawapongeza kwa utartibu huu wa kutumia New media katika uandaaji wa vipindi vyenu lakini nashauri mfanye kama wenzetu nje CNN,BBC na Aljazeera kama mnaweweza ,fanya mjadala huo wa studio na ule wa interenet hasa kwenye thread yako viendane sawa wakati wa kuchangia.

ingawa hapa kuna changamoto ya mtandao ,vifaa nk lakini pole pole tutafika

napongeza kwa ufanisi katika fani

Byabato

Tunafanya Maandalizi Byabato...Verysoon tutaanza kuwa na mijadala ya papo kwa papo online wakati wa LIVE Discussion on Studio
Yahya M
 
Tatizo lenu mnaalika wageni ambao mitazamo yao tayari inajulikana sasa utapataje mawazo ya upande mwingine? haya mwalikeni huyo warioba aongee tunachokifahamu tufurahi halafu maisha yaendelee! democracy haijengwi hivyo wazee!

Nayo pia ni mawazo Kalagabaho though umejicontradict kwa mtazamo wangu.
Yahya M
 
Mapendekezo: Mchakato wa Upatikanaji wa Katiba Mpya uweje? Ni dhahiri katiba mpya haiepukiki kwa sasa. Utaratibu upi utasaidia kupatikana Katiba itakayokidhi mahitaji ya Watanzania..

Ni vyema upatikanaji wa katiba uhusishe makundi yote pasipo kubagua kwa mfano eti kundi la walemavu wa miguu,mikono liwasilishe na walemavu wa ngozi {albino} hii si sawa wote wanapaswa kuingia katika mchakato wa katiba kwa kutuma wajumbe. Cha msingi serikali iwe makini hapa katika huu mchakato kila kundi au kila fani iwe na wawakilishi ili kuondoa manung'uniko mbeleni. Mi napendekeza kila kundi katika jamii lihusishwe moja kwa moja katika mchakato wa katiba.
 
Nafikiri watanzania tuwe serious ili suala hili lisonge mbele. Tusisubiri mkutano wa Pinda na Kikwete maana naamini watatukwaza
 
Mtafute pia Prof. E. Rwaitama na Pia linahitajika kundi la vijana wa sheria pale chuo kikuu cha Dar es Salaam au kundi la wabunge vijana
 
Mkuu mjadala uliopita niliufuatilia vizuri sana, na nawapongeza sana mjadala ulikuwa mzuri! Mkuu tunaweza kumpata mtu toka tanzania visiwani kuleta usawa naona kama tunajadili katiba ya tanganyika wakati hii ni tanzania.
 
Henge nakubalian na wewe. Lakini ukweli ni kwamba Zanzibar wao wana katiba yao ambayo tayari wameipitisha. Utaona ukweli ni kwamba katiba hii tunayoizungumzia ni kama ni ya Tanganyika. Kwani umeshasikia Zanzibar wanajishughulisha na jambo hili? Kilio chote kiko kwa watanganyika.
 
Mchakato mzima uanzie kwa kuwapata wawakilishi kutoka makundi mbali mbali ya kijamii, vyama vya siasa, madhebu ya kidini, na asasi mbalimbali. Hii itatusaidia kuwa na katiba itakayo kuwa imewashirikisha wananchi kutoka katika ngazi ya shina tofauti na katiba tuliyokuwa nayo sasa ambayo haikumshirikisha mwananchi kiasi kwamba hata mwananchi wa kawaida kule mkuzi lushoto, Nyamanoro au Buhemba hajui kuwa kuna katiba inayo tambua stahili zake.

Tunahitaji katiba mpya yenye tija na inayoendeana na mazingira na wakati tulio kuwa nao leo na kesho. Hivyo hata mchakato wake unatakiwa uwe makini ili kuondoa mazonge yaliyopo yasijitoke. Katiba tuliyokuwa nayo ilipita ndani ya Dk 10 na ikatufikisha hapa tulipo! Hatutegemei mchakato wa katiba mpya uwe wa kasi ya kutimiza matamanio ya kuwa na katiba mpya. Mchakato uwe makini kuhakikisha kuwa tunapata katiba itakayo dumu kwa kipindi cha miaka kadhaa yenye kukidhi mahitaji laki bila kuwa na malalamiko ya mara kwa mara.

Kuwashirikisha wananchi ndio msingi mkuu wa kuwa na katiba yenye kuangalia maslahi ya wananchi maana wanaweza kuwawajibisha au kuwaarudi viongozi wao pale wanapo potoka tofauti na sasa, Na si kuangalia maslahi ya viongozi peke yao ambao hutumia udhaifu wa kutokuwashirikisha wananchi kuji vimbiza vitambi vyao kwa tamaa na ulevi wa madaraka.

Naomba kuwasilisha.

MouddyMtoi
 
Yahya, asante kwa vipindi vyako unavyotushirikisha kuhusu msitakabali wa nchi yetu. Imenipa faraja sana kwamba sasa waandishi mmekomaa maana mnatushirikisha msitakabali wa nchi yetu na kuvunja ile kasumba ya kufanya mawazo yenu ndio mawazo ya wananchi wengi.

Mimi nina mawazo zaidi kwamba hata kabla ya kufikiri jinsi ya kuunda Katiba yetu mpya ya muungao ebu tufikirie zaidi na muundo wake. Tusiende mbio sana.

Kwa upande wangu wakati tunafikiri kuhusu mchakato wa kuunda katiba iweje na nani wahusike, kwanza naomba niseme mimi ningefikiri kwanza katiba hiyo mpya ilenge kuwa na serikali 3, ile ya Tanzania bara (Hapa nitaiita Tanganyika), Tanzania visiwani (Hapa nitaiita Zanzibar) na Muungano (Hapa nitaita muugano wa nchi Tanzania). Na kwa kweli kila nchi hapa inahitaji kwanza katiba yake ambayo itaitambua nchi hiyo kama nchi huru (identity of the state). Bahati nzuri ndugu zetu Zanzibar tayari wameshakwenda hatua ndefu zaidi kwa kutengeneza katiba yao ambayo inaitambua nchi yao kama nchi huru. Sisi bara (Tanganyika) je? tutaendelea kuwa nchi isiyo na utambulisho? Lazima tuwe na utambulisho katika katiba ya muungano. Hatuwezi kuendelea kuwa nchi inayosemekana kuwa imeungana na nyingine lakini wenzetu wakiwa na state yao sisi tukiwa hewani na tukiwa hatujulikani ni nchi au la. Na kama ni nchi katiba yetu ni ipi?. Tujiulize je kama tutasema tutengeneze katiba ya muungano ni kati ya nchi ngapi? mbona moja ina katiba na nyingine haina?

Jambo hili litatuletea matatizo mbeleni tu. Hivyo kuwe na katiba tatu kama nilivyoainisha, moja ya Tanganyika, nyingine ya Zanzibar na ya mwisho ya muungano.

Sasa tunapokuwa tunafikiria jinsi ya kupata hizo katiba lazima makundi yote mawili ya kwanza, yaani katiba ya Tanganyika na ile ya Zanzibar yashughulikiwe na nchi husika tu. Ile katiba ya Tanganyika iwahusishe watanganyika tu, na waamue je wanahitaji kuiunda vipi, na ile ya Zanzibar ishughulikiwe na wazanzibar peke yao. Kwa bahati hawa wameshashughulikia ya kwao.

Tukishamaliza kabisa kupata katiba za nchi zote mbili sasa ndipo michakato ya kuunda kamati zitakazoangalia jinsi tutakavyounda katiba ya muungano itakapofanyika kama baadhi ya wadau wengine hapa wanavyopendekeza.

Yahya, ikumbukwe kwamba katiba ya Tanganyika ni muhimu sana ili huko mbele tusijejikuta tunarudi kubebeshana lawama kwamba viongozi wetu wametubulura kuingia katika muungano ambao ni batili kwani hakuna muungano wa nchi moja na muungano wa nyingine isiyokuwepo utakao kuwa halali katika katiba ya muungao kama ilivyo sasa. malalamishi yataendelea kuwepo maana tayari yapo. Tunaposema tuna nia ya kushughulikia kero za muungano let's consider both sides of our union. Tusidhani kushughulikia upande mmoja tu itakuwa tiba. Asante
 
Ndugu zangu nimeona na haya maono tusiyapuuze! Ila tuyafanyie kazi sivyo tutavuna tutakacho kipanda sasa WAPO WAZALENDO WALIOTUONYESHA NJIA LAKINI VIONGOZI WETU WA WAKATI HUO HAWAKUYAWEKEA MAANANI mawazo yale WAZALENDO HAO NI MAREHEMU JAJI NYALALI JAJI KISANGA.....LICHA YA GHARAMA KUBWA ZA PESA ZILIZOTUMIKA KUKAMILISHA KAZI HIZO KAZI WALIO IFANYA HAIKUTHAMINIWA LEO TUTHAMINI KAZI ZAO NA ZIWE DIRA KWA KUTEKELEZA YALIYOMO KWENYE RIPOTI ZAO hapo ndipo tuanzie mchakato wa mkutano wa KATIBA! mnaonaje WATANGANYIKA?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom