This Mchepuko is another level to my wife, mpaka najuta

This Mchepuko is another level to my wife, mpaka najuta

INSONSILE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
1,938
Reaction score
2,904
Miaka sita iliyopita nilikutana na binti huyu, tukafahamiana, tukapeana contacts. Off course, tulishawahi kuonana kabla katika mazingira official. Anyway, tukajikuta katika dimbwi la mapenzi ambalo mpaka sasa kutoka imekuwa kasheshe, na kwa sasa, liwalo na liwe.

Ni hivi, huyu mchepuko ni single mother, na huyu mtoto alimpata katika stage za mapema form four. Alikiri kuwa ilitokea bahati mbaya tuu wakati wanaingia ujanani enzi hizo. Ninafahamiana na familia yake yote (mama, dada na kaka zake).

Alifiwa na baba yake akiwa form two, wakawa katika mazingira magumu sana kimaisha.Kwa upande wangu wakati nafahamiana naye, tayari nimeshaoa ila kwa kuwa nilikuwa mbali na familia kwa muda mrefu basi nikawa napoozea hapo. Huyu mchepuko hakuwa na kazi yoyote, basi tukawa marafiki.

Kusema ukweli, hana tabia ya kupiga mizinga, hana tamaa ya maisha, wala pesa za short cut. Anaishi maisha ya kawaida sana, naweza kusema maisha ya chini kulingana na anachopata kutokana na kazi yake. Wakati mwingine anapungukiwa na 10,000 lakini asiniambie, nikigundua basi huwa nampa surprize namsaidia hata zaidi ya hiyo.

Kadiri maisha yalivyombana ndivyo alikuwa ananiomba sana ushauri (na wala si pesa) ili ajikwamue kimaisha. Kwa upande wangu, pia maisha yalikuwa magumu, mshahara ulikuwa hautoshi hata kidogo kuendesha familia.

Nikawa nasoma sana vitabu vya Robert Kiyosaki kuhusu masuala ya fedha, uwekezaji na kuwa na furaha maishani. Vile vitabu vilinipa mwangaza mkubwa wa uhalisia wa maisha. Kiyosaki Anapinga maisha ya kutegemea mshahara, anasisitiza uwekezaji, biashara na maisha ya kujitegemea.

Basi nikawa namshauri huyu binti japo sikuwa na wazo specific la nini afanye, ila nilikuwa napanua mawazo yake. Siku moja akaja na bonge la wazo kuhusu mradi fulani. Akanipa business plan. Daaah, nikatafakari nikaona ni kitu inalipa sana, tena si gharama kihivyo kuianza.

Basi, nikafanya mpango, tukakubaliana nimkopeshe laki 5, atairudisha kwa miezi miwili. Nikaikopa kazini, nikampatia. Kweli dada wa watu akaifanya biashara hiyo na kila step akawa ananishirikisha, mpaka mauzo akiuza mzigo ananijulisha faida bila kuficha hata senti tano.

Kweli biashara ilikuwa inalipa na mimi nikapata uzoefu wa aina yake. Hatimaye, akataka kuirudisha hela yangu, nikamkatalia. Nikashawishika na mimi kuifanya hiyo business, ila mazingira ya kazi yananibana. Tukakubaliana tufanye biashara pamoja, yeye kwa asilimia kubwa ndo msimamizi, alafu tugawane faida.

Ninachofanya, wakati wa kuchukua mzigo basi mimi naongeza kama laki moja au mbili za ziada, kama kulipia usumbufu anaopata kwa mimi kutokuwepo kwenye usimamizi wa biashara. Hivi ninavyoandika uzi huu, kila mwezi tukigawana faida, kila mtu anaondoka na 1.5m, nje ya matumizi yooooote.

Kwa upande wa pili,
Mke wangu alikuwa form four leaver, hakufanikiwa kuendelea mbele. Nikamsihi sana nimfungulie biashara yoyote atakayoichagua, na mtaji wowote ule, nitakopa hata benki, lakini wapi, akakataa kata kata. Anataka kazi ya kuajiriwa.

Nikahangaika, akareseat paper form four, miaka miwili, akafanikiwa kupata credit ya kwenda chuo cha ualimu private grade A, akapiga miaka miwili, akamaliza ndo akaajiriwa anafundisha shule ya msingi, mshahara laki tatu kwa mwezi, alafu nauli kwa mwezi kwenda shule ni 50,000. Anasota, anachoka mpaka namhurumia.

Mpaka leo nikimpa wazo la biashara hayupo kabisa huko. Tukidraw mshahara wake 300,000 na wangu 1,000,000, hiyo hela haitufikishi hata tarehe kumi ya mwezi husika. Kama mjuavyo matumizi ya mshahara, ukiweka list ya mahitaji unaweza kukimbia.

Sasa, mimi wala sipanic, akitaka kununua kitu mi nampa hela tuu, ila anasema mbona tunatumia hela nyingi kuliko mshahara? Simjibu napata wapi, nawaza nikimjibu nitaelezaje? Anyway, nikisema nitengeneze story ya kawaida ya kitu ninachofanya, atataka twende face to face aone shughuli.


 
Biashara gani hiyo, wape mchongo na madem wengine humu watoke.
 
Mmmh.akati njia kuu stress.anaeza akaengage kune bzness tuu akiamua.
 
Huna jinsi huyo ndio mkeo ni lazima utafute njia ya kuhakisha ana kubali na anabadilisha mind set na aweze kujikwamu! Una kazi ya kuhakisha ana jikwamua hata kwa lazima.
 
Moral ya hii story ni moja. Jamaa mkewe Hana akili ya biashara, Hana plan B ya Maisha na atabaki kuwa tegemezi Maisha yake na sijui kama Kuna ndoa hapo
 
Hapo issue ni kuangalia maisha, huwezi kumwacha eti kisa ni mchepuko. Ila ili story hii iwe na mashiko weka bayana biashara gani mnayoifanya
 
Mmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhh! Sasa huu mchepuko umeugonga tayari ama? Mi naona uongo mzuri ni uongo wa ukweli. We mwambie una biashara na huyo dada. Sababu umejishtaki mwenyewe hatokuhisia vibayaaa. Mtambulishe kila kitu. Ficha ficha hii siku utakufa ghafla wanao wateseke bureee. We unafikiri yule dada atamwambia mkeo?
 
Kwa hii story yako ingekua mkeo ni mama wa nyumbani ningesema ni fulani ninamfahamu yeye, mkewe na mchepuko.
 
Ajabu sana kama mkeo hajaiona hii. Ndiyo maana mara kwa mara huwa nasisitiza kuwa na ndoa ya mkataba
 
Hapo njia panda kweli kweli...Maana na haya maisha lazma huyo "mchepuko" atakua anakuvutia zaidi, ukizingatia huo upambanaji na kujituma. Huku upande wa pili wife anaonekana kama mzigo.Kwa heshma ya mkataba wa ndoa kwasababu uliuingia mwenewe, basi ukumbuke kua ulisema "katika shida na raha"
 
Back
Top Bottom