Weledi uko api hapo? Hivi kwanini huyu ndugu polisi amuadhibu mtuhumiwa badala ya kumkamata, kukusanya ushahidi dhidi yake, kumpeleka mahakamani na akamtolee ushahidi madhubuti ili haki itendeke?
Hata katika ushikaji wa chombo cha kurusha vitu vizito hakuna weledi kwani yale yale ya Mwangosi (RIP brother) Je kama kitu kizito chenye ncha kali kingechomoka kwa bahati mbaya ingekuwaje?
Mbaya zaidi wananchi wanapita kando na kuangalia kana kwamba kinachofanyika ni sahihi au hakiwahusu. Utaona na watoto wetu wako kando wamesimama na wajifunza tabia mbaya hapo.
Hakika sina nia ya kumtetea huyo mtuhumiwa ila utaratibu si upo? basi na ufuatwe. Kila mtu atimize wajibu wake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.