This is the other side of Dubai

Mbaya saana mzee, wakati mwingine mafanikio huja baada ya kurisk!
Aisee!Kuna nchi sababu ni za msingi kama syria au hata eritrea au dprk mkono wa chuma wa watawala ndo unazalisha wakimbizi lakini hizi nyingine kweli marisk taker.
 
Hao sio warabu, Ni wafanyakazi toka India Na nchi nyinginezo za Asia
 
wamedakwa chanzo itv raia wa ethiopia wanatia huruma ila ndo hivyo wahamiaji haramu ndo wanavoitwa ila hivi tukiwaruhusu wapite kimya kimya manake hawa ni on transit jumuiya ya kimataifa itaruka na sisi tuongeze matukio zaidi ya lile za zanzibar.
 
Sio kweli hiyo kuhusu Dubai huo ni uzushi wa ajabu
 
m mwenyewe kuna jamaa amenipa dili la kwenda dubai kufanya kazi za ICT.....anadai ukifanya kazi miaka miwili tu ukirudi umaskini bai bai.........nilipoona hizo picha nimeghairi siendi tena nakomaa hapahapa bongo.......dubai ntaenda kutalii sio kufanya kazi
 
Mkuu hio style ya "pay as u go" ipo sehemu nyingi.
Kariakoo mtaa wa congo wenye nyumba wengi walikua wanawalipisha wamachinga tsh.200 kwa kichwa kulala varandani. Wanakua kama watu 20 hvi. Asubuhi wanasepa zao.
London pia kuna landlords wanawalaza wahindi kibao kwa basement kwa £10 per night.

Haya mambo ya kusave hatari sana.
 
Naomba unitajie nchi 5,
Ambazo hazina watu wanaoishi katika mazingira magumu.
Hayo sio mazingira magumu.....huo ni unyanyasaji, hata wakimbizi UK,Sweden,Denmark hawaishi hivyo....kumbe ndio maana wanakimbiliaga Ulaya badala ya Uarabuni!
 
Ndio maana mkaka mmoja aliondoka huko akaja kufanya kazi ya 1.5m bongo. Sikumuelewaga aisee
 
Hayo sio mazingira magumu.....huo ni unyanyasaji, hata wakimbizi UK,Sweden,Denmark hawaishi hivyo....kumbe ndio maana wanakimbiliaga Ulaya badala ya Uarabuni!

Wamenyanyaswa na nani wkt serikali haitambui uwepo wao,
Nataka unitajie nchi 5 ambazo hakuna watu wanaoishi kwa mazingira magumu,

Unazungumzia wakimbizi wkt hao wanajulikana mpk idadi zao.
 
Jamaa wamekwenda kwaajiri ya ujenzi wa viwanja vya mpira 2020 Dubai wanatoka Bangladesh na Nepal ndio wengi na india
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…