This is Politics.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
04_09_4heph6.jpg


"Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) Mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto) na Katibu Mkuu wa CUF Seif Shariff Hamad wakitoka nje ya ukumbi wa Hoteli ya Lamada Dar es Salaam baada ya ibada ya dua ya kumuombea marehemu Mzee Shaaban Khamis Mloo ambaye ni mmoja wa waasisi wa CUF aliyefariki hivi karibuni. Rais Kikwete alialikwa kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Inasikitisha sana kuona wanapelekwa mapolisi kwenda kuuwa Zanzibar ,kwa kweli inasikitisha sana unapoona watu hawa wanakenua mpaka jino la mwisho ,mhusika Mkuu yupo kati kati ,Je huu uislamu wake hapa unajali maisha ya watu wanaopigwa na kudhalilishwa kule Zanzibar au sehemu nyingine yeyote ,wale wanaoouliwa na kupigwa na vyombo vilivyop chini yake wanaweza kuwa kama hao anaocheka nao na kufurahi nao ni wafuasi wa Chama pinzani sawa na wale wanaopigwa na kudhalilishwa na vyombo vilivyo chini yake, maisha ya hapa duniani ni ya kupita ,sioni sababu ya kutokuendesha uchaguzi ulio sawa na waki ,we need kuifanya Tanzania iwe yenye viongozi wanye nyuso za furaha kama hawa ,furaha hizi zienee hata kwa wafuasi wa vyama vyao ndipo tutaweza kuijenga Tanzania na kufikia lengo.
Siasa za mabavu na chuki hazileti faida ,viongozi hawa waliojaa furaha ni kitu gani au ujumbe gani wanawapelekea wananchi ?
 
Last edited:
Haqbari hii ingenoga kama picha hiyo ameweka mtu mwingine halafu wewe unalalamika. Ukiisoma habari hii unaoneka kama vile ulikuwa unataka picha hii tuione vile?

Hongera kada wa chama cha mapinduzi kwa kazi yako nzuri
 
Si wanasema dini na siasa havichangamani? sasa hayo mauaji yanahusiana vipi na dini ya huyo jamaa na uanasiasa wake?
 
kwangu mimi hayo matabasamu si ya kulazimishwa, inaonekana ndani ya kila mmoja wao kunautu! Utu ambao ukitafutiwa namna kunamambo yanayoweza kuongeleka. Cha maana zaidi nikiangalia picha hiyo, nafurahishwa jinsi ambavyo kizazi hiki kimepata neema ya kujuana hata nje ya siasa! Nashidwa kuelewa kwanini wanashidwa kutumia hizo social fabric zao kutatua matatizo.

Siasa ya vizazi vijavyo - kuanzia 2020 itakuwa mdumange kweli kweli! maana Raisi kasoma marekani, waziri dar es salaam, mwingine ujerumani! hawa watu hawajawahi kukutana shule ama wapi! wamekutana katika majukwaa ya siasa! itakuwa kazi kweli kweli!
 
CCM/CUF versus CHADEMA ? - Habari ndiyo hiyo. Matunda ya MUAFAKA !
 
Sijui lakini hii picha kusema kweli ,inajieleza kabisa ,Tanzania inaweza kujiepusha na migongano ya kisiasa maana siuoni ule uadui wa Mwai Kibaki Na Raila Odinga ,ambapo wawili hao wanapokutana kila mmoja anaweka ndita iwe kwenye msiba au furaha ni vita tu ,iko haja kubwa ya Muungwana kujipiga kifua na kuigeuza Tanzania kuwa kisiwa cha Amani ya kweli na si unafiki ,inawezekana kabisa.
 
Chama cha mapinduzi kinapindua vyama vingine lakini kimeshindwa kujipindua chenyewe
 
Kanzu, makoti, kofia, tabasamu, zimewapendeza sana.

Tulumbane kwa tofauti za itikadi zetu lakini isifikie kuwa mahasimu.

Hilo ndio somo la hiyo picha kwa waTanzania wote.
 
kanzu, makoti, kofia, tabasamu, zimewapendeza sana.

tulumbane kwa tofauti za itikadi zetu lakini isifikie kuwa mahasimu.

Hilo ndio somo la hiyo picha kwa watanzania wote.

tumekupata mkuu si unapenda kanzu??? Wangekuwa si akina yakhe ungesema leo mpaka dunia ipasuke
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom