Uchaguzi 2020 This is Bishop Gwajima in his true colours

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,794
GWAJIBOY AKIMKARIBISHA JPM: Mheshimiwa Rais karibu sana jimbo la Kawe. Watu wa Kawe wamekusanyika hapa kwa wingi kukupongeza kwa kazi kubwa uliyowafanyia. Kwa miaka mitano ya uongozi wako umetatua kero ya muda mrefu ya maji maeneo mengi ya jimbo letu.

Umepeleka umeme kata nyingi, umejenga vyumba vya madarasa kwenye kata karibu zote, umetanua barabara ya Bagamoyo kutoka Morocco hadi Mwenge ili kupunguza msongamano, umejenga barabara nyingi za mitaa kwa kiwango cha lami na zinapitika muda wote. Mheshimiwa Rais tunakushukuru sana.

GWAJIBOY AKIMZUNGUMZIA MDEE:
Mheshimiwa Rais jimbo hili ni kama halina Mbunge. Kwa miaka mitano ya viti maalumu na 10 ya ubunge huyu mama hajali shida za wananchi kabisa. Maeneo mengi ya jimbo letu yana shida ya maji. Kata ya Mabwepande, Madale na Goba maji yanatoka mara moja tu kwa wiki na wakati mwingine hadi wiki mbili hayatoki.

Baadhi ya maeneo mtandao wa umeme haujafika kama kule Kisauke na Mbopo. Maeneo ya Mabwepande kuna uhaba wa vyumba vya madarasa watoto wanasongamana darasani na wengine wanakaa chini. Barabara nyingi za mitaa hazijakarabatiwa na hazipitiki. Mbunge yupo tu hakuna anachofanya. Kazi yake ni kuchochea migomo na kutoka bungeni.
 
Nitampima 'Mbunge' wangu mtarajiwa Gwajima baada ya miaka yake Mitano na kuhusu 'Mapungufu' yake ya Kibinadamu hata Sisi pia tunayo sana.
Tukubali tu kwa Siasa ndani ya ccm yani Diwani na Mbunge hawana nafasi yakutuletea maendeleo jamani kwasababu ni kunguru wa kueleza matatizo ya nchi. wako kama wasindikizaji tu. kazi zao za msingi wameshindwa wote probably ndo maana watu wanaona ni fursa kwako kiuchumi.
 
Haeleweki, kata zenye maji yameletwa na JPM ila ukosefu wa maji ni Mdee.
Hiyo ndiyo aina watu ambao Magufuli anataka waingie Bungeni,hawana kumbukumbu na uwezo wa kuhoji/kupinga/kupigania chochote.Anawapenda anaoweza kuwadhibiti na siyo wabunge wanaojitambua.

Tukifanya kosa la kuruhusu CCM kuingia madarakani kiharamu,watahakikisha wanabaki milele kwa kufuta sheria zilizopo kwa manufaa yao.Mfano halisi ni Kyle Visiwani. Wapiga kura wasifikia milioni 1 wanapigishwa kura kwa siku mbili lakini Bars yenye wapiga kura zaidi ya milioni 28 wapige kura kwa siku 1.Wizi?
 
Back
Top Bottom