Dogo anapenda sifa za kijinga.
Mara aseme alialikwa kama msaili kutoka taasisi nyingine, mara aseme ameyaona majina yako kwenye word document, mara seme asingekua mzee angeomba.
Kikubwa ni kwamba dogo hana sifa za kuomba hiyo kazi au aliomba akapigwa chini, ndio maana unaona anahangaika sana na hizo kazi. Aliomba kazi kisha akasingizia mke wake ndio kaomba kazi.
Sifa za kijinga hua hazina maana. Mwaka juzi November aliomba asaidiwe kazi ya uhasibu, maana ndio mwaka alikua kamaliza masomo ya chuo.
Kazi za serikali lazima uwe na cheti, vyuo vingi hua vinatoa cheti miezi 6-12 baada ya kumaliza masomo. Kwa hali ya kawaida, mwaka jana serikali haikuajiri, hata kama aliajiriwa mwanzoni mwa mwaka jana, maana kuna taasisi ziliajiri, bado ni junior sana na mshahara usiozidi milioni.
Kwa kupenda sifa hua anadai analipwa milioni zaidi ya 2, sasa anajiita msaili.
Bora ukose mali upate akili.