Think about this.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Think about this..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by shinyela, Jun 28, 2009.

 1. s

  shinyela New Member

  #1
  Jun 28, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kadri siku zinavosonga, Waafrika tunazidi kupoteza utamaduni wetu na historia pia. Nadhani ingekua ni jambo la hekima kuutunza utamaduni na historia yetu kwa ajili ya vizazi vijavyo. Wenzetu watu wa Magharibi, wanatunza na kuzikumbuka tamaduni zao kupitia makumbusho na majumba ya sanaa.

  Tanzania ina makumbusho ya kijamii yaani public museums chache sana. Jambo la kusikitisha zaidi kama si kutia aibu, hatuwezi kuzitunza hata hizo chache zilizopo.

  Mimi ni mtu wa Mwanza, Msukuma haswaa. Nasikitika sana kuona, Makumbusho ya Bujora hayapatiwi matunzo ya kutosha. Ikumbukwe kuwa makumbusho haya yalijengwa na mapadri kutoka Magharibi kama ishara ya kuuenzi USUKUMA. Ni ajabu sana kuona wao angali wageni waliona umuhimu wa kuwepo kumbukumbu ya watawala wa Mwanza na pia mila na desturi za Wasukuma wakati wazawa wa Mwanza na wakazi kwa ujumla hawana muamko kama huo kabisa.

  Moja ya mipango mizuri ya waanzilishi wa Bujora ilikua ni festival Bulabo (soma kuhusu Mwanza kwenye wikipedia nimeeleza kwa upana zaidi) ambayo ingefanyika kila mwaka wa mavuno ikishirikisha vikundi vya ngoma za utaduni yaani Bagika na Bagalu. Waanzilishi walijenga kiwanja eneo la kisesa Mwanza kwa ajili ya tamasha hili. Enzi hizo tamasha hilo lilifana sana, huniambia baba yangu. Vikundi kutoka Ulaya vilishiriki kama inavoonekana kwenye picha.

  Wageni wetu wakifurahia nasi 1995..

  [​IMG]


  Leo hii uwanja huo wa tamasha umeanguka baadhi ya kuta zake na majani yameota kimo cha mbuzi kana kwamba hakuna anaejali wala kuthamini.

  Angalia mfano wa tamasha la Sauti za busara zanzibar, ni tamasha zuri na lina leta watu wa sehemu mbalimbali pia linatangaza taifa letu. Kama kungekuwepo na mawazo endelevu kama haya pia uwezeshaji, naamini inawezekana kabisa KUFUFUA tamasha la Bulabo, ambapo vikundi vya jadi kutoka Tanzania na dunia yote kwa ujumla wake, vitafurika mwanza kila msimu wa tamasha pia vikundi vya burudani za kisasa vitakuwepo kuleta uwiano wa leo na jana. Hii haita kuwa namna ya kuenzi utamaduni wetu tu, bali ni sehemu ambayo watu watapata manufaa ya ajira ya kuuza bidhaa za kitamaduni na pia kuwa pamoja pasipo tofauti. Fikiria hili.....


  Bulabo enzi hizo...
  [​IMG][​IMG]
   
  Last edited: Jun 28, 2009
Loading...