They know everything

Tinde nsalala

JF-Expert Member
Feb 12, 2017
248
253
Kauli ya bwana mkubwa fulani alipokuwa anahutubia siku fulani ktk warsha fulani.

Alimaanisha wana kijiji,eti( kwa tafsiri isiyo rasmi)wanelewa kila kitu.Pengine alimaanisha wanatambua maendeleo ambayo awamu hii inayaleta kwao.

Niandikapo mada hii nipo huku kijijini kwetu, PUNI mkoa wa SHINYANGA wilaya ya SHINYANGA vijijini.Ajabu wanakijiji wenzangu hawa kwa namna wanavyouponda utawala wetu,ni dhahili si kweli tena kwamba; THEY KNOW EVERYTHING!

Wanalalamikia sana Uhuru wao wa kung'amua!Wanalalamikia sana uminywaji wa demok.... ktk nchi yao!Wanahoji pia,eti kwanini BASHITE (LAGHAI wa ELIMU)hajachukuliwa hatua hadi wakati huu tena kwa makosa yaliyo bayana kabisa aliyoyafanya!Zaidi,Wanalalamikia sana sana jamaa yao mpendwa,MPIGANIA na MFIA chama NAPE NNAUYE kwa alivyotendwa!Kwa ujumla malalamiko yao ni mengi!

Jamani,TUSIDANGANYE!Wanakijiji wa leo si wa JANA!Shime,viongozi tendeni haki na wema ktk kila maamuzi yenu.

2020 si mbali!
 
CCM ni chama chenye MTANDAO Mpana kuanzia ngazi ya mashina.. CCM kina mitandao ya Wazazi, vijana, pia kina wafuas na mashabiki pande zote mijini na vijijini.. CCM kinapendwa hata chadema kina wafuas wengi.. Tatizo ni moja tu ambalo watu hawaelewi.. Magufuli anakubalika kuliko mwanasiasa yoyote Kwa Sasa hotuba zake anazozitoa Kwa LUGHA ya KISWAHILI zinawafanya wazalendo wazidi kumpenda jinsi anavyosimamia FALSAFA Yake ya hapa kazi.. Magufuli ni chaguo la MUNGU. Magufuli anajua nini anafanya. Kujenga uchumi Imara usio legelege.. Mipango Yake ya muda mrefu inawatofautisha na viongozi wa upinzani ambao Bahati mbaya wamebaki kusubiri matukio au mkuu akosee kidogo tu kwenye hotuba zake. Kwa hiyo navoona mimi magufuli anakwenda kushinda Kwa kishindo zaidi ya asilimia 69 kwenye uchaguzi ujao
 
Asante,lakini mtendee haki kidogo MKUU mwambie kwa sasa yuko uchi, mwambie avae kabla hajachelewa.
 
Back
Top Bottom