Gwanggaeto the Great
JF-Expert Member
- Apr 14, 2018
- 901
- 1,936
Waziri mkuu wa UK Theresa May ameshinda kura zilizopigwa na wabunge za kutokuwa na Imani na utawala wake. Wabunge wa Chama cha Conservative 315 wameuunga mkono utawala wake. Kama May angalishindwa basi ingalimlazim kuachia ngazi.
Chanzo: Al Jazeera na Press tv
======
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameshinda kura ya kuwa na imani naye katika uongozi wake wa chama tawala cha Conservative kwa kupata kura 200 kwa 117.
Baada ya kupata asilimia 63 ya kura zote, sasa ana kinga ya uongozi kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Hata hivyo Waziri Mkuu May amesema pia anasikiliza mawazo ya wale waliopiga kura ya kumpinga na kuahidi kuwa atafanyakazi na vyama vyote vya siasa, kuirudisha tena nchi hiyo katika hali yake.
Waziri Mkuu wa Uingereza hii leo atakabiliana na kura ya wabunge kutokuwa na imani na uongozi wake.
Wabunge wa chama tawala cha ndio waliopiga kura jana usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Mhariri wa siasa wa BBC Laura Kuenssberg anasema kucheleweshwa kwa Brexit ndiyo karata ya turufu ambayo wafuasi wa Bi May wametumia kuwashawishi wabunge wasimng'oe madarakani.
Chanzo: BBC Swahili