There shall be a day!



Haya bana. Hizi lugha za watu ni utata mtupu. Inabidi tukimaliza hii issue ya Muungano tujiunge na English course. Hatuna jinsi mkuu.
 
Nundu again?..siku ingine ukiamua kuandika thread... please tumia kiswahili ili walengwa tukuelewe..wengi wetu tumesoma shule za kata..

anyway time will tell.

IF You didn't take ..litereture class, that is not his case...

We Salute you Omar Nundu ...the truth will prevail ...that once upon a time ,stand men and women who to this land they bow....,and there came the masters asking for there head....but with the striking power of alimighty ..,from above ...the survived at last ..., when the wind pulled all the ashes ...they will be standing aside strong like corner stones ....and thee come men singing song of praise and revolution ..as wreath of power is bestowed upon them .....there shall be a day!!
 
mkuu unamuonea tu huyu muheshimiwa,

wengi ya watendaji wezi na wabovu hakuwa na mamlaka nao, na wala hawaripoti kwake!

Mfano ni naibu waziri wake! Anazama masafari anaaga kwa pm.

we unacheza na tanganyika wewe? Wizi upo damuni.
wewe mzanzibar ni mnafiki tuu!
Wizi ndo unaita watanganyika na wewe unakuwa wa kwanza kutetea majizi ya ccm!
Acha unafiki mkuuu!
 
Omari R Nundu, kabla hujapata huruma ya watanzania unayotaka, hebu jisafishe. Funguka utupe ukwel wa kinachotokea huko ndan. Kiapo ulchoapa siku unaapishwa kuwa wazir labda kilikuzuia that time, sahv upo nje.

Hukumu waliyokuhukumu wao haitakuwa na nguvu kama watanzania tutaujua ukwel. Hiyo ndiyo kiu na njaa yetu jangwani hapa.
 
Last edited by a moderator:
Ana Post Tatu tu,
ya kwanza alituma 2007, ya pili 2010, ya tatu 2012, ya nne atatuma 2015.!!!

tehe tehe tehee!!
Junior Member Array Join Date : 11th November 2007
Posts : 3
Rep Power : 0
Likes Received: 7 Likes Given: 0

Yawezekana huyu ni Nundu kweli
 
Nundu ustadhi wangu nimeanza kukuchukia kama ninavyomchukia Lowassa.

Mna kitu mioyoni mwenu kwanini hamtaki kusema ili mpone, kwanini mnakubali kuwa wachafu kwa kubeba uchafu wa watu wengine. Kwanini mnakuwa wanafiki!?
 
Pole sana Kaka yangu wa Tanga lakini we always learn from mistakes natumaini mbeleni tuendako utakuwa makini kuchagua gari bora !
 
Kwako Mheshimiwa Omari R Nundu, nafikiri lililokutokea sio geni kabisa katika siasa. Linaitwa kuwajibika kisiasa. Nafikiri ulishapewa nafasi mbalimbali za kutoka msafi lakini ulishindwa kuzitumia. Ulikuwa na nafasi ya kukemea hayo maovu wakati ukiwa waziri kabla hata ya report ya CAG na haukufanya hivyo. Vile vile ulipewa nafasi ya kujiuzulu mapema lakini haukuitumia. Leo hii hii unataka sympathy yetu baada ya kufurumushwa na Rais?

Sijasema kwamba wewe ni mchafu au kuna lolote baya ulilifanya wakati ukiwa waziri, lakini ilibidi uwajibishwe maana haukuweza kututetea sisi wananchi wakati tulipokupa hiyo dhamana.

Tunakupatia nafasi ya tatu ya kuja msafi. Jitoe katika chama chako, njoo huku kwetu wananchi na tueleze kinaga ubaga nini hasa kilitokea. Na ufanye hivyo bila kuficha majina. Na sisi wananchi tutaamua kama tutakusamehe au la. Otherwise, yote haya unayojaribu kuyaongea mimi nachukulia kama re-bound na kushindwa kuamini kama umetoswa.

Pole sana Mheshimiwa kwa misukosuko ya kisiasa.
 
Last edited by a moderator:
.....na kwa vyovyote vile sintotoa SIRI ZA BARAZA LA MAWAZIRI....
 
Mkuu Keil umesema kweli, tutabadilisha mawaziri sana tuu lakini tusipobadilisha mfumo mzima basi tusitarajie miujiza yeyote. Mfumo mzima umeoza tunahitaji kuubadili kwa faida ya wananchi wote wa sasa na baadae.

Sasa ni nani atabadirisha huo mfumo? Hao mawaziri wanabadirishwa ili wakiingia kule warekebishe mfumo! Naam, nguvu za kurekebisha mfumo ili ulete matokeo wanazo. Sasa kwa nini wakiingia humo humezwa na mfumo? Ni nani atakayebadirisha huo mfumo? Unashauri watanzania wote tukaubadirishe huo mfumo?

Mfumo mbovu huwekwa na kusimamiwa na watu wabovu! Watu wazuri wakiingia kwenye mfumo mbovu; ama wataubadirisha au wakishindwa watatoka kwa hiari yao wenyewe! Sasa mfumo wetu ni dude gani hilo kila mtu mzuri akiingia anamezwa na mfumo hawezi kufurukuta? ......... na hata kujitoa hawezi!!!!!

Mfumo ni watu,
 
Last edited by a moderator:
WanaJF,

Nilibahatika kufanya kazi na huyu mhe. Nundu kwa kipindi chake chote cha U waziri hakika nasema kama kuna kitu ambacho kimenisikitisha ni Mhe. Rais kumuondoa mkuu huyu pale Wizarani.

Tatizo kubwa nililogundua kwa Mhe. Nundu yeye si mwana siasa ila ni mtendaji na ni mtu anayesimamia ukweli kwa kile anachoamini ndio sahihi kwa wakati huo nimegundua nchi hii haiwataki watu kama Nundu hata kidogo; kwa misingi hii hatutafika kokote. Alikuwa na mikakati mizuri ya kufufua mashirika yetu yalifisadiwa na viongozi waliopita ambao waliua ATC ili shirika lao la ndege liweze kushamiri.

HII NDO TANZANIA BWANA! PUMZIKA Mhe. Nundu mm ni miongoni mwa watu tunaokufagilia kwa kazi zako.
 
Mh. Omari R Nundu, kwanza pole sana hii ndio Tanganyika yetu ulitakiwa kuijua kabla hujajiingiza ktk siasa za Unafiki. Lakini kinachonishinda kuelewa ni hiyo ngonjera yako inaonyesha udhaifu wako ktk kujitetea maana unaposema innocent lamb inanipa picha kwamba hukuondolewa kama mboga ya walaji bali kafara umetolewa kuwalinda watu wengine.

Kama ndivyo basi bila shaka unaijua kafara hii imewapa uhai kina nani na nilitegemea ungekuja hapa na kuzungumzia mwanzo wa kuitafuta haki yenyewe ili hiyo one day itokee. Maana nijuavyo kila siku ni siku mpya na hiyo siku unayoizungumzia lazima itokane na nguvu ya wewe na wananchi wengine kusimamia yale wanayoamini ni haki yao kuyatetea. Tunachoka na hizi habari za Bangusilo kila mtu anapomwagwa.

Navyoamini mimi wewe sii bangusilo wala hukutolewa kafara bali ni ktk mfumo utekelezaji wa KULA KWA ZAMU kama wewe ulitaka kufanya kinyume cha machinjioni ambako hapakosekani nyama basi hiyo ndio sababu yako kuondolewa. Hakuna zaidi umeziba riziki za watu na ukubali matokeo maana wenzako wako kazini kuchukua chao mapema. Historia inajieleza wazi kwamba toka JK ameingia madarakani mawaziri na Manaibu waliopona na kukaa zaidi ya awamu moja ni chini ya asilimia 20 na wote waliobakia hukaa meza gani.

Hata siku moja usijetegemea mbuzi au kondoo wa kafara ktk mila na desturi za chama CCM ila ni sherehe kwao.. Hawataachwa kuchinjwa mbuzi wala kondoo na kuokwa kwa ndimu na pilipili maadam sikukuu za Unyago, ndoa, Hitma, maulidi, Christmas, Idd na kadhalika ndio kwanza zinazidi kupata waumini wengi zaidi, na hivyo yanayofanyika sii kafara bali umewekwa mboga mezani - UMELIWA kama tunavyoliwa sisi wengineo!
 
Last edited by a moderator:
Mh OR Nundu, pole saaana kwa yaliyokusibu. Kwa mtizamo wangu ni kuwa, kwa serikali iliyopo sasa hivi, ni afadhali ukakataa uteuzi wowote ili kuepuka matokeo kama haya. Kikwete anataka watu ambao ni maswahiba wake au maswahiba wa mwanaye wenye uwezo wa kufanya ufisadi na kuficha vizuri ufisadi wao. Kama ikitokea ukafanya ufisadi na ukajulikana kupitia Kamati ya Bunge, au kupitia Mkaguzi wa Mahesabu ya Fedha, Kikwete atakugeuka na kukubebesha lawama zote.

Kikwete ukifanya naye kazi utachafuka na kuharibu jina lako. Ni raisi wa ajabu sana dunia haijapata kuona. Kama wa-Tz wangekuwa na nusu ya roho ya ki-Arab Kikwete asingeweza hata kumaliza mwaa mmoja pale Ikulu yetu. Lakini bado yupo pale kwa sababu sisi wananchi tupo kama tulivyo, wapole kama kondoo.

Tatizo jingine ni aina ya wasaidizi unaojikuta kufanya nao kazi. Wizara yako ina watu ambao ni hatari sana kwa taifa hili. Mfano Omary Chambo - huyu mtu hana hata 0.0% ya uzalendo moyoni mwake, na mtu anayemhifadhi pale ni huyo Kikwete kwasababu zilizopo na zinahifadhiwa. Mtu mwingine aliyekuzunguka ndiyo huyo jamaa mwenye maneno meeengi, fisadi asiye na haya Mh Mfutakamba. Jamani hata anayewateua sijuwi huwa anawatowa wapi na anatumia vigezo gani kuwapata watu wa jinsi hii!!! Mtu mwingine ni huyo mutu yenye maneno miingi Saad Fungafunga... orodha ni ndefu ya viongozi wabaya wakiongoza Wizara nyeti na mhimili wa uchumi wa taifa.

Pole sana, mimi nakuomba utumikie taifa lako kupitia Bunge la JMT. Kule serikalini hakuna kitu huko ni wizi tu..
 
Inspiring piece of verse. Yet, be sure that many of your fellow citizens will be gleeful of your predicament. Our society is riddled with puzzling hipocrisy. Otherwise, CCM would have been long gone into the dustbins of history trash. As for me, I'm just sad that you were so naive as to not have discerned the workings of the system all this time. Even if you had been away for so long, you should have kept yourself well apprised of the current reality.

Do not be fooled. In my dear Tanzania, there cannot be any lucrative contract/deal without the knowledge and interest of the "mafia establishment" with its tentacles deeply entrenched in all corridors of power - especially in the magogoni manor. Trying to correct things while riding on the crocodile's back? That's too naive! I've always believed that all those struggling to get opportunities thro' CCM like you as being driven by pure greed and ready to serve the system.

It comes as a surprise to me that you also seem taken aback by the lies of the system! That you could be a really honest being wrongly penalised by the system! I'm now keenly interested to see your next move especially if offered a consolation prize; RC, DC, etc.
 
Mh Omari R Nundu, .....good that you come over here and try to show your innocence on the matter.....calling yourself a sacrificial lamb.....But i have matters which need clarity from you please......now that you are out of office....

a]Can you please give us your genuine take on the two Chinese companies which were involved in contradictory port building contracts/MOU under your leadership??..i mean..the CCCC Ltd and the China Merchant..

b]If you saw that your depute...Athuman Mfutakamba was wrong in going to china for the CCCC Ltd deal....why didn't you report him to your boss for further disciplinary measures?....why wait until everybody started shouting at you two ministers???.....many people thought that your failure to deal with your errant depute was one way of showing your involvement in the China merchant's deal......i mean.. both of you ministers had conflicts of interest in those two companies....otherwise..why did you tolerate corruption from your depute?

c]There are allegations that you didn't deliver at all as a minister......i mean....considering the country has no any functioning plane...the railway is a mess....the port.. with those corrupt deals..etc etc.......Can you please tell us where in TZ have you been successful in your tenure as transport minister?

d]Lastly,...what advice do you offer to the new transport minister...Hon.Mwakyembe???considering that he has had issues in dealing with corrupt individuals in this country...and he will probably meet them again at this new ministry......
 
Last edited by a moderator:
Iweje magufuli aweze pambana na wanaotaka kumuaribia kazi hadharani wengine washindwe. Yamemkuta kwa-kuto chapa kazi sasa anataka huruma ya jamii na kulaumu wengine.

He had the chance to fight his case when he was in his position tatizo lao hawa watu ni dharau na kujiona miungu watu wanapopewa nafasi yakiwakuta (something they never expected ndio hizi sympathy wanazotaka). Asingedharau parliament committee, akajielezea bungeni nini kimetendeka ambacho akija mfurahisha kutokana na huo mkataba uliopo na kwanini aliona aende nyuma ya channels za kuomba tender leo watu wangekuwa upande wake.

Maji yamefika shingoni na kutemwa sasa ndio haya ya mashairi ya lamb sijui nini. He deserves everything he got out of his slackness in his role.
 
amen, may all of us think, feel and act in the dark as we will be courageous to act in broad day light, look back and say we did it right!
May The Good Lord save us all, as He saves Tanzania,
 
"A day when an innocent lamb survives slaughter"
Umeisema mara mbili mkuu; inaonesha ni jinsi gani unatamani uonevu uliopo nchini ukomeshwe!!
Je, ni hatua gani unachukua, Mh. Nundu, ili kujenga mazingira ya kutimia kwa ndoto yako?!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…