Theologians,Why is Sin an Automatic Inheritance But Salvation isn't, Even Though Both Happened Before You Were Born?

Theologians,Why is Sin an Automatic Inheritance But Salvation isn't, Even Though Both Happened Before You Were Born?

Vitabu vya dini huwa vinakubali tafsiri yoyote, ndiyo maana hata watetezi wa jinsia moja wanaweza kunukuu kifungu hiki au kile kwenye hiko hiko kitabu.

Hivyo ni ngumu kujadiliana nao pale unapowapa nafasi ya kutumia vitabu vyao

Wanaweza kukujibu kirahisi tu, Yes Watu wanazaliwa na ukombozi automatically lakini baadhi yao au wengi wao wanaamua kuukata kwa kufanya dhambi

As long as unacheza kwenye sheria zao hakuna swali wasiloweza jibu

Ni kama kucheza drafti na njiwa.
 
Wana Theolojia, Kwanini mtu Anazaliwa na Dhambi na kurithi automatically, Lakini sio ukombozi?

Ingawa vyote vilitokea kabla ya mtu kuzaliwa?

Kwa nini mtu huyu asizaliwe na ukombozi tayari?
Wrong

Sin ni kitu mtu anatumia utashi wake kukifanya au kukataa kufanya.

Tofauti na hivyo ni makosa tu na sio dhambi.

Madhara ya makosa yanaruhusiwa kurithiwa kama tu ambavyo faida za mazuri hurithiwa.

Mtu huzaliwa akiwa ni mzuri, mwenye mwanga na mwema hahitaji ukombozi kabla hajasin bado. So haileti mantiki azaliwe na ukombozi🙅‍♂️. Na kwa nature ya dhambi haiwezekani kuwa nayo kabla mtu hajajitambua🧘.
 
Wrong

Sin ni kitu mtu anatumia utashi wake kukifanya au kukataa kufanya.

Tofauti na hivyo ni makosa tu na sio dhambi.

Madhara ya makosa yanaruhusiwa kurithiwa kama tu ambavyo faida za mazuri hurithiwa.

Mtu huzaliwa akiwa ni mzuri, mwenye mwanga na mwema hahitaji ukombozi kabla hajasin bado. So haileti mantiki azaliwe na ukombozi[emoji2285]. Na kwa nature ya dhambi haiwezekani kuwa nayo kabla mtu hajajitambua[emoji3257].
Wakatoliki wana sema kila binadamu huzaliwa na dhambi ya Asili, kwamba mpaka ubatizwe ndio dhambi hiyo huondoka.
 
Actually kwa uwelewa wangu hapa tulipofikia ndio Ile vijana wanasema Dunia simama nishuke, wanaadamu tumefikia sehemu ambayo hatuwezi tena kuendelea mbele kwa kuishi kwenye basics za Utu, kujitambua Na malengo yetu kama binaadamu hapa ulimwenguni, kwa sababu Mungu mwenewe alituumba akatuwekea Sheria Na akatupa utashi wa kuchagua Kati ya kutenda mema au mabaya, vitabu vya dini pamoja Na Sheria za kidunia zinatoa hukumu ya aliefanya mema atalipwa mema Na aliefanya mabaya atalipwa mabaya, Ila deep down Mungu kama Mungu hawezi kuwa Na chembe ya mawazo ya kumuadhibu kiumbe wake kwa ubaya alioufanya, hili ni jukwaa la great thinkers ndio maana nimeongea haya, mwanaadamu ni the best creature the God has ever made, mambo mengi Sana yametokea tokea kuumbwa kwa ulimwengu Na mpaka sasa yanaendelea kutokea Ila cha muhimu Sana kuliko yote ni suala la binaadamu kujitambua, Na hapa kuna kundi la watu wanaojifanya wajanja wajanja Na kutumia nafasi Na uwezo wao walionao ama katika taasisi za dini au mamlaka za nchi au ushirikina kupotosha,kukandamiza au kutoa vitisho kwa wale ambao bado hawaja jitambua, kama mpaka Leo binaadamu tunaamini kuwa mungu ametuumba Na baadae akatuchome Moto basi bado binaadamu tuko nyuma Sana katika kujitambua, Na kwa mwenendo huu haiwezekani binaadamu kujitambua, ndio maana nikasema inabidi tuanze upya katika kumtafakari mungu Na kusudio lake kwetu wanaadamu, ikiwa binaadamu wa kawaida tu hata kujitambua hajitambui au kujitambua kwake kwa uchache tu anaweza kumsamehe binaadamu mwenzake akiwa amefanya kosa lolote lile kama binaadamu huyo atasikiliza roho ya Utu aliyonayo ndani yake iweje mungu ashindwe ambae ni muweza wa yote, hizi Sheria zipo ili maisha yawe Na nidhamu lakini kimsingi binaadamu hapaswi kuishi chini ya Sheria, kwa sababu kuishi chini ya Sheria maana yake huyo kiumbe bado hajajitambua, mwanaadamu anaejitambua maumbile yake mwenyewe yatamuongoza kufanya kila linalotakiwa kufanywa Na ataacha kila linalotakiwa kuachwa, sadly tumezifanya Sheria kuwa ndio muongozo wa maisha yetu kiasi ambacho hatuwezi tena kuendesha maisha yetu bila kufuata Sheria zilizowekwa,kimaumbile ya binaadamu kuna Sheria nyingi Sana ndani yetu ambazo hakuna dini, serikali au mamlaka yoyote Yale ambayo yanaweza kuzigusa au kuzichezea, naongea hivi with evidence ya kila nafsi ya mwanaadamu analitambua hilo, lakini tulivyoamua kujifungia kwenye brackets za Sheria ndio tumejimaliza, nafsi ya mwanaadamu ni zaidi ya Sheria zote unazozijua zinazomtawala mwanaadamu. Kwa hapa tulipofikia lazima tukae chini tuanze upya, tuanze kuweka misingi mmoja baada ya mwengine, kwa kila ambacho mwanaadamu anakihitaji Na asichokihitaji katika mustakbali wa maisha yake, tena tukiongozwa Na nafsi zilizokuwa Safi bila upendeleo au ubinafsi wowote mbele yetu, vyenginevyo hatuwezi kufika tunakotakiwa kufika, huu ulimwengu mungu ameuumba Na akatuumba Na sisi binaadamu ili kuutawala lakini cha ajabu binaadamu huyu yeye mwenyewe ameshindwa kujitawala, kula yake tu inamshinda, leo walioendelea wanapigana vikumbo Na kujititumua kutaka kuitawala Dunia Na ulimwengu wakati kuna binaadamu wenzao wanakufa kwa njaa Na maradhi halafu wanajifanya wameendelea THUBUTU? Kama hayo ndio unaona ni maendeleo basi wewe Na huyu mlala hoi unaemdharau hamuna tofauti yoyote vichwani mwenu au inawezekana akakuzidi hasa maana yeye hajapata exposure Na resources kama ulizonazo wewe, hizi double standards tulizoziweka ndizo zimetufanya tumesimama hapa Na hatuwezi kupiga hatua hata chembe kama hatutaondoa hilo. Huu sio wakati wa kusema Dunia simama nishuke Bali ni wakati wa kutia Sheria mfukoni Na kila mwanaadamu aanze kuishi kwa mujibu wa nafsi Na maumbile aliyoumbiwa Na mungu. Sote tumeumbwa Na mungu mmoja Na nafsi zetu ni sawa, tuache ujanja ujanja kwa sababu ujanja ni kwa watu walioishiwa Na wasio Na maono ya mbali.
Ni hayo tu kwa Leo kesho pia ni siku.
Was salaam.
 
Wana Theolojia, Kwanini mtu Anazaliwa na Dhambi na kurithi automatically, Lakini sio ukombozi?

Ingawa vyote vilitokea kabla ya mtu kuzaliwa?

Kwa nini mtu huyu asizaliwe na ukombozi tayari?
Swala la ukombozi nila mtu binafsi, kila mtu atabeba flushi lake mwenyewe mkuu!
 
Wana Theolojia, Kwanini mtu Anazaliwa na Dhambi na kurithi automatically, Lakini sio ukombozi?

Ingawa vyote vilitokea kabla ya mtu kuzaliwa?

Kwa nini mtu huyu asizaliwe na ukombozi tayari?


Kwa mtazamo wa Uislamu: Swali lako linapata jibu kwa sababu Uislamu haufundishi kwamba mtu anarithi dhambi ya Adamu. Qur’an inasema: “Kila nafsi haibebi mzigo wa mwingine.” (Qur’an 6:164). Adamu alikosea, akatubu, na Mungu akamsamehe (2:37). Kwa hiyo mtoto huzaliwa hana dhambi ya kurithi; kila mtu anawajibika kwa matendo yake mwenyewe.

Kwa mtazamo wa Ukristo: fundisho la dhambi ya asili linasema dhambi iliingia kwa wanadamu kupitia Adamu (Warumi 5:12). Lakini ukombozi kupitia Kristo hauhesabiwi kuwa kitu cha kurithi automatically; Biblia inaufanya kuwa wokovu unaohusishwa na Kristo na imani kwake (Yohana 3:16; Waefeso 2:8–9).

Lakini hapo ndipo swali lako linakuwa zito: kama matokeo ya kosa la Adamu yanamfikia mtu kabla hajazaliwa, kwa nini wokovu wa Kristo usimfikie mtu kwa namna hiyo hiyo? Hilo ni jambo ambalo Ukristo unapaswa kulieleza, si kuliepuka.
 
Back
Top Bottom