Theluthi 2 ya wanawake hawajui kusoma, kuandika

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Habari za Kitaifa

Theluthi 2 ya wanawake hawajui kusoma, kuandika

Imeandikwa na Mwandishi Maalumu; Tarehe: 24th February 2011 @ 07:46 Imesomwa na watu: 20; Jumla ya maoni: 0








WANAWAKE theluthi mbili ambao ni watu wazima hawajui kusoma na kuandika huku ikielezwa kwamba hakuna dalili zinazoonesha kushuka haraka kwa idadi hiyo ya wajinga.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake (CSW), mjini New York, Marekani.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo, unaongozwa na Naibu Waziri, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummi Ally Mwalimu.

Akihutubia umati wa wajumbe kutoka nchi wanachama 192, Migiro alisema kuwa licha ya kwamba uwekezaji katika elimu hususani kwa wanawake na watoto wa kike ni jambo lisilo na ubishi, bado kundi hilo la jamii limeendelea kuachwa nyuma.

Alisema, “wakati mkiwa mmechagua elimu kama dhima kuu la mkutano wenu, na wakati tunajadili hali ya wanawake, ni vema mkatambua kwamba theluthi mbili ya watu wazima wasiojua kusoma ni wanawake.

Na takwimu hizi hazijabadilika kwa kipindi cha miaka 20.” Naibu Katibu Mkuu alisema hakuna jambo jema kama uwekezaji katika elimu kwa kuwa manufaa yake ni makubwa na ni mengi.

Alisema nchi nyingi zimejizatiti katika kuhakikisha kwamba zinafikia lengo la kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule na bila ya kujali jinsia yake anapata fursa hiyo.

Hata hivyo, alisema kuwa pamoja na jitihada hizo kumnufaisha mtoto wa kike, bado zipo changamoto kubwa wenye ubora wa elimu inayotolewa.

“Bado ubora wa elimu inayotolewa hususani katika nchi zinazoendelea haujaendana na kasi ya uandikishaji wa watoto. Watoto wengi wanamaliza shule wakiwa hawana ujuzi na maarifa ya kusoma wala kuhesabu,” anabainisha Migiro.

Kwa mujibu wa Dk. Migiro, uwakilishi wa wanawake katika nyanja za sayansi, teknolojia, elimu na ajira bado ni wa kiwango cha chini.

Akawataka wajumbe wa mkutano huo, kuutumia mkutano huu kujadiliana na kubadilishana mawazo na hatimaye kutoka na majibu ya mambo ya msingi yanayoendelea kuwa kikwazo kwa maisha bora na maendeleo ya mwanamke.
 
Ukombozi wa mwanamke kupitia majukwa yaelekea bado kuzaa matunda na pengine ni debe tupu ambalo haliachi kutika............
 
Du ni hatari hizo takwimu mimi ninaziamini kabisa kwani ukitaka kujua hilo tembela vijijini ni hatari!
 
Back
Top Bottom