The universe and origin of man

Callisto

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2017
Messages
241
Points
250

Callisto

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2017
241 250
......................nilipo kuwa form one mwaka 2011 nilifundishwa mambo meng kuhusu ulimwengu pamoja na asili ya mwanadamu kupitia somo la historia na jeografia..........evolution of man ni nadharia ambayo ilitolewa na Charles Robert Darwin( english man) ni mwana sayansi mkongwe wa kipindi hicho karne ya kumi na tisa (19century) ambaye alijikita zaidi kufanya utafiti kuhusu asili ya mwanadamu pamoja na mimea.....ndani ya miaka mitano ya utafiti ambayo ilifanywa na Charles uko america kwenda kuchunguza wanyama na mimea (flora and fauna) ...tayari Darwin akawa ameandika na kitabu kinacho elezea asili ya mwanadamu........Darwin akadai asili ya mwanadamu ni jamii ya mnyama sokwe........je uwepo wetu sisi apa duniani tumekuja kwa bahati mbaya je na uyo nyani alitoka wapi...? Aya maswali nitajibiwa na watu wenye mawazo ya Darwin...............kila kitu kilicho ndani ya mwili wetu kipo ktk mpangilio hakuna siku ambayo utakuja kuvutia pumzi au hewa kupitia sikio,........kuna mambo mengi yakujifunza ebu twende mbali kidogo mfumo wetu wa jua kuna sayari kama nane tunawashukulu NASA kwa utafiti wao, tupo ktk galaxy inayo itwa milky way, kuna mamilion ya nyota kama mchanga wa bahari ..........kuna kitu kinaitwa JUA Mimi na wewe atujui ni lini liliundwa na lina umri kiasi gani, na kila siku tunaliona likipita kutoka magaribi kwenda mashariki according to NASA........ukienda ktk biblia ktk ktabu cha mwanzo Mungu ndiye muumba wa ulimwengu pmj na hili jua tunalo liona ....je sayansi inasemaje kuhusu kuundwa kwa jua? Nao wanamajibu yao.................lakini ktk mfumo wa jua kuna sayari kama vile mercury, venus,dunia,mars,Jupiter, nk kila sayari inamwendo wake ambao haubadiliki milele na milele, hakuna siku ambayo dunia yetu itaenda kuwa kalbu na Jupiter au Jupiter kwenda kuwa sayari ya kwanza afu mercury kuwa sayari ya tano.......... Dunia yetu ipo inaelea sio kwa sababu ya gravitation force kama tulivyo fundishwa ktk physics na geography.........je nayo iyo gravitation force ilikuja kwa bahati mbaya kama alivyotokea mwanadamu ....? Je dunia ilitoka wapi ? Kuna nadharia kibao zinazo elezea chanzo cha ulimwengu (dunia) lakini zote hazina majibu yaliyo jitosheleza zaidi ya kuwa na challenges chungu nzima .....je mpangilio wa sayari tunaojua nao ulikuja kwa bahati mbaya ? Dunia yetu ni sayari pekee yenye uhai ktk mfumo wa jua..............kuna zaidi ya galaxy billio 100 pmj na nyota kbao lakin ni galaxy chache tu zilizo gunduliwa na baadhi kupewa majina kama vile spinit.... Ambapo kuna baadhi ya galaxy kuzifikia ita kuchukua miaka kbao kufika.............na kunasayali kibao zilizo nje ya mfumo wa jua letu na zenye kuvutia kwa rangi nzuri kuliko ata dunia yetu lakini hakuna ata kiumbe ata mmoja.............................tusiende mbali kuna sayari ya Jupiter ni kubwa kuliko sayari yeyote ktk galaxy yetu(milky way) , pia kuna miezi kbao inayo izunguka Jupiter km vile Callisto, lo,europa pmj na Ganymede .......je aliyeiumba Jupiter ni tofauti na aliyeiumba dunia? Dunia yetu ni kama kapunje ka mchanga kaliko ufukwen mwa bahari ya hindi... Lakini wanaoishi ndani ya dunia wamejisahau ....MUNGU bado anataka kutuonesha kuwa yupo pia ndiye aliyeiumba dunia, jua,venus,pluto, Jupiter, mars, na vitu vingine vilivyo fichwa ........ndiye anayeifanya venus ionekane sayari inayo ng'aa kulko sayari yeyote ile lakini bado MUNGU kaipendelea dunia kaipatia maji ya kutosha,oxygen,milima,misitu ili mladi tusipate shida lakin bado tuna tamani kwenda sayari ya mars uku tukiwa tumebeba maji na oxygen kwenye makopo..........si makosa kujifunza kuhusu mambo ya kiulimwngu kuhusu mwili wa mwanadamu na asili ya ulimwengu ila tukumbuke kuwa kuna muumba wa hivi vyote maana yeye ndiye mwanzilishi wa hii elimu .....tusiwe wafuasi wa Darwinism theory pasipo kujua hatima ya maisha yetu... je tukifa tunaenda wapi ? Hilo ni swali ambalo hakuna ajuaye Ila amini kuwa haya mambo yote yanayotokea ulimwenguni hayakuja kwa bahati mbaya au kwa bahati nasibu kama alivyo elezea dokta Darwin kuhusu asiri ya mwanadamu....................nmemtumia Darwin kama spaceman ila nadharia za Darwin bado zina enziwa na wasomi mgando ambao bado elimu haija wakomboa.........ebu jalibu siku moja ukae peke yako sehemu iliyo tulia anza kujifikilia ww kuhusu atma yako after death, anza kufikilia namna dunia jinsi ilivyo usiku na mchana,maji ya bahari, mtoni,ziwani,milima, majangwa,mimea, kisha peleka mawazo yako ktk mwili wako ulivyo undwa ,macho,moyo,ubongo,tumbo linavyo fanya digestion ya chakula kila sku.....hadi sasa unaweza kusoma hii text lakin bado unadai wew ulikuja kwa bahati mbaya unamuunga mkono Charles darwin........ulimwengu unavitu vingi sana kuliko hata unavyo vifahamu lakini Mungu kaichagua dunia kuwa mahali pekee kwa ajili ya kuishi mim na wewe ............................unaruhusiwa kuto povu lolote lile ata la unga
 

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Messages
8,183
Points
2,000

KENZY

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2015
8,183 2,000
hili langu sio povu..
Mpaka hapa tulipoleo hakuna chenye uthibitisho dhahiri kuwa chenyewe ndo chanzo cha kila kitu!.. unavyosema kuwa tutafakari namna vitu vilivyo kisha tuhitimishe kuwa mungu ndo kaumba huo ni ukilaza!.
na ndio maana huyo mnaemuita mungu mnashindwa kumdhihirisha kwamaana ni mungu wa kufikirika(mnamfikiri kuwa yeye ndo kaumba)
lkn udhihirisho ndo neno kuntu na ndio maana huwa mnawaambia watu waamini tu!.

ulimwengu ni kama kitabu kikubwa sana ambacho lugha zake zote bado hatujazijua,taratibu tunaendelea kuzisoma huku tukipukutisha ulimbukeni na kung'amua mambo tofauti tofauti.. let the nature talk
 

BOSHOA

Member
Joined
Feb 9, 2013
Messages
67
Points
95

BOSHOA

Member
Joined Feb 9, 2013
67 95
hili langu sio povu..
Mpaka hapa tulipoleo hakuna chenye uthibitisho dhahiri kuwa chenyewe ndo chanzo cha kila kitu!.. unavyosema kuwa tutafakari namna vitu vilivyo kisha tuhitimishe kuwa mungu ndo kaumba huo ni ukilaza!.
na ndio maana huyo mnaemuita mungu mnashindwa kumdhihirisha kwamaana ni mungu wa kufikirika(mnamfikiri kuwa yeye ndo kaumba)
lkn udhihirisho ndo neno kuntu na ndio maana huwa mnawaambia watu waamini tu!.

ulimwengu ni kama kitabu kikubwa sana ambacho lugha zake zote bado hatujazijua,taratibu tunaendelea kuzisoma huku tukipukutisha ulimbukeni na kung'amua mambo tofauti tofauti.. let the nature talk
ni kweli mungu hakuumba ila MUNGU ameumba na wewe ni kazi ya mikono yake
 

BOSHOA

Member
Joined
Feb 9, 2013
Messages
67
Points
95

BOSHOA

Member
Joined Feb 9, 2013
67 95
*Isaya 40:28*
[28]Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake *hazichunguziki*.

*Warumi 11:33,36*
[33]Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake *hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!*
[36]Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.

*Isaya 45:9,12,22*
[9]Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unafanya nini? Au kazi yako, Hana mikono?
[12]Mimi nimeiumba dunia, nimemhuluku mwanadamu juu yake; Mimi, naam, mikono yangu mimi, imezitanda mbingu, na jeshi lake lote nimeliamuru.
[22]Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.

MUNGU yupo na mimi ni kazi ya mikono yake, nitamtukuza na kumuabudu milele yote amina!
 

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Messages
8,183
Points
2,000

KENZY

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2015
8,183 2,000
ni kweli mungu hakuumba ila MUNGU ameumba na wewe ni kazi ya mikono yake
umeona hiyo ndo hoja ya msingi ati mungu na MUNGU ni tofauti,nikikwambia uitamke kwa herufi ndogo na kubwa utaweza..? au ndo ujanja ujanja uso na hatua yoyote mnajitahidi kuonyesha utofauti lkn mnatambua dhana inayoongelewa hapo ni moja tu! shangaza sana nyie..
ati namimi ni kazi ya mikono yake! kumbe anamikono hlf tena mwasema hajawahi onekana! mkuu we amini unachokiamini that is what i can say to you,kwasababu ubongo wako umekubali mapokeo hayo tokana na ujazo wa ufahamu wako na mazingira.
 

Pendael24

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2014
Messages
2,479
Points
2,000

Pendael24

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2014
2,479 2,000
Kusema kwamba hakuna Mungu ni uwongo.

Ambacho kinaweza kusemwa ni maelezo kuhusu huyo Mungu hayakueleweka vyema.

Pengine wale waliopokea maelezo yahusuyo Mungu walipokea kwa kiasi cha uelewa wao,lugha yao,utamaduni wao,na mazingira yao.

Sasa kuyatafsiri hayo katika zama hizi ndio imekua shida.

Kuyaleta hayo maelezo kuhusu Mungu kutoka zama zile na kuteta katika utamaduni wa sasa,elimu ya leo,mazingira ya sasa,na imani za kileo ndio imeshindikana.

Mkristo amepewa Biblia kama kitabu rejea kuhusu Mungu na ha kuruhusiwa kutafuta maelezo yahusuyo Mungu nje ya kitabu alichoelekezwa.

Hicho kitabu cha Biblia ni mikusanyiko wa maandishi ya watu mbali mbali na kila mmoja akiwa na akili yake na halafu pia alicho kiandika alisimuliwa na huyo msimuliaji ama aliota au alipata maono, tena ndani ya kifungo cha utamaduni wake mazingira yake na uelewa ulio saizi yake.

Huyo msimuliajia alimsimulia mwandishi nae akaandika,katika mazingira na uelewa na nia yake na kusudio lake, akaja mtu kukunya maandishi hayo akayachambua lipi liwe lipi lisiwe, katika lugha yake na katika nia yake,akayafunga katika kitabu kimoja kikaitwa Biblia.

Leo nije mimi mchaga na kichaga changu na kiswahili cha kuokoteza na elimu ndogo ya msingi tena ya kuunga unga, nikachambue maelezo ya kusuyo Mungu yalioandikwa kiyunani na kiebrania, tena cha kale,yakatafsiriwa kilatini yakaletwa kiingereza na kuleta pia kiswahili na kila lugha mtafsiri alikua na nia na kusudio lake, sitaelewa kwa wepesi .

Labda kama Mungu angefanya kama zamani kama tulivyo elezwa kwenye hivyo vitabu kua aliwatokea watu.


Lakini iwe iwavyo yupo Mungu yaani Mungu yupo ila maelezo yake ndio yanakinzana.
 

dmatemu

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2008
Messages
754
Points
500

dmatemu

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2008
754 500
Unapoona tv, redio, gari, ndege, meli, pikipiki nk, huna haja ya kuuliza chanzo chake. Unajua automatically kwamba zimetengezwa (na binadamu) tena kwa ustadi na mpangilio Mkubwa.

Vivyo hivyo, unavyoona dunia, mwezi, nyota na sayari nyingine, viumbe wa aina aina, wenye rangi na wanaovutia, wakubwa kwa wadogo, vilivyo katika mpangilio na ustadi mkubwa, kisha ukashindwa kujua ama ukagoma tu kwamba hakuna aliyevipangilia, duh inahitaji imani sana kuamini unachoamini.

Unapoona kuna mpangilio sehemu, intelligence ndio chanzo cha huo mpangilio, sio chance. Chance has never been a source of fine tuning. Kuthibitisha hilo, chukua vyuma vyuma kisha UNGANISHA BY CHANCE upate meli au ndege au gari. Hata ufanye mara trillion trillion, bila intelligence, hutapata meli wala ndege wala gari.

Uhai haijatokea by chance. Uhai uliumbwa na a very intelligent designer, (sio lazima umuite Mungu), lakini uwepo wa maisha na mpangilio duniani unathibitisha bila shaka yoyote uwepo wa huyo designer

Nawasilisha
 

Mr Easy

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2016
Messages
1,209
Points
2,000

Mr Easy

JF-Expert Member
Joined Jan 16, 2016
1,209 2,000
Siku nyingine unavyoandika mambo mazito kama haya, epuka kutulisha maneno eti mimi na wewe hatujui umri wa jua.
Watu wanajua umri wa jua na muda uliobaki ili lifike kikomo. Halafu NASA wa wapi waliosema jua linapita west to east!
Dogo andiko lako lina makosa kibao, huwezi kutuambia eti Jupiter ni kubwa kuliko sayari zote katika galaxy hii ya milkway, are you serious kijana!
 

Forum statistics

Threads 1,367,646
Members 521,789
Posts 33,405,794
Top