The truth about beauty peagents | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The truth about beauty peagents

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by cheusimangala, Apr 11, 2010.

 1. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  TOPIC: THE TRUTH ABOUT BEAUTY PEAGENTS

  Thanx guys 4 ur views. have bin thinking then i realised dat i started too far dats y most of u didn't understand. Here am back with a new topic, i believe with timt u will understand. I won't give up; i will keep educating u on whats going on around us. Hakuna genuine beauty peagent here in tz, na kama ingekuwepo, basi tungeona matunda yake! Jiulize tangu miss tz imeanza mmeona matunda gani au wameisaidia jamii vipi zaidi ya skendo chafu tupu? ni wa ngapi wako indipendent? usinipe jibu. je mnajua waandaaji wa mashindano ya urembo, si matajiri ila ni watu tu wa kawaida wanaotafuta maisha? now, mnajua kuwa wako mkao wa kipesa zaidi kuliko kuthamini hao warembo wanaowatumia kupata pesa? je mnajua kambini warembo tunafundishwa pozi, urembo na kujiweka matawi; hatufundishwi kutafuta maisha kupitia nafasi hiyo! mnajua kama wengi tunashiriki umiss tukiwa wadogo na tunatoka ktk familia duni, sometimes vijijini, tukitafuta kutoka kwa kujua business ni genuine? mnajua kama tunatafutiwa mabwana na wanakamati kwa vigogo? ndo skendo mnazosikia kila siku! mnajua kama ushindi unanunuliwa? mnajua kwamba tukiwa kambini vigogo huja kutuangalia na kupata opportunity ya kuchagua wanayemtaka? mnajua ukikataa unaweza kuchafuliwa ktk vyombo vya habari na hata kuvuliwa taji au kufukuzwa kambini? mnajua huwa tunasaini mikataba na beauty peagents na huwezi kuitumia hiyo opportunity bila ruhusa yao? wakiamua kukuchunia huwezi kufanya lolote lile mpaka utakapovua taji! mnajua kama unafanya wanachotaka si unachowaza! ur under control! nawapa mfano; mnajua mkasa wa miss tz mwaka huu? au mnaamini mliyosoma magazetini? Miriam alipofika dar, kigogo mmoja akamtaka; miriam kaconvisiwa na wanakamati amkubali ili amsaidie na kumpa ushindi. too much pressure, ikabidi akubali. hapo hapo, alikuwa na boyfriend wake kitambo ila akaamua kuwa na kigogo pia huyo boyfriend wake. kigogo alimpa mashart kwamba hataki kumsikia na mtu mwingine na kumuahidi ushindi; na kweli alimpa ushindi! na kumpiga soap soap sana pia kumpangishia nyumba mikocheni. Parties daily, na kumfanyia maandalizi yote ya kwenda miss world mpaka ticket ya ndege na si kamati ya miss tz! maana ni jukumu lao ila tu nataka upate picha ya hii game inavyochezwa. Miriam, chini chini akawa anaendelea na boyfriend wake kwa madai hakumpenda huyo kigogo na huyo kijana alikuwa anajua miri yuko na kigogo mpaka alikuwa anakwenda kulala kwenye hiyo nyumba aliyokuwa kapangishiwa miri na kigogo, hadi na ufunguo mmoja miri alimpa. Hakuna siri duniani, kigogo akapata taarifa na akaamua kutuma wapambe wafuatilie. ndani ya masaa 48 miri akafumaniwa kinondoni kwenye baa moja akiwa kapumzika na bwanake wakati huku kamuaga kigogo anaenda msibani. ILINIUMA sana jinsi alivyotupiwa mizigo yake nje na huyo kigogo! na kigogo akaamua kuitisha kikao na kamati ya miss tz na kutaka arudishwe mwanza hataki kumuona hapa mjini. Palikuwa hapaoshi, miri akaamua kumwambia kigogo huyo kuwa hampendi ila anampenda sana boyfriend wake. Kigogo akadai huyu miri kwa nini leo ajifanye mjanja na kumkataa baada ya kumgharamikia sana na kumpa umiss? kigogo akaanza kumuandalia soo..... katafuta wapambe, kuwalipa ili wafuatilie nyendo za miri na boyfriend wake..na kupanga kuwafanyia soo huku polisi wakiwa wametonywa. ndo siku hiyo miri yuko out na bwanake, mara vurugu isiyoeleweka, fujo kutoka kwa hao wapambe na dakika chache polisi haooo. dili ikachongwa watozwe hela kubwa ya mdhamana ili washindwe kulipa, wawekwe ndani. ndo kisa cha miri na bwanake kuwekwa ndani. mnajua kama kaka yake miri alienda kumbembeleza kigogo huyo ili amtoe dada yake? inasikitisha sana! niulize ndugu zangu, huo ndo ukweli wa huo mkasa, je wengi wenu mlikuwa mnajua? je beauty peagents zinasaidia nini, na matunda yako wapi? habari zote mnazojua kuhusu umiss zina ukweli wake tofauti na mnavyojua! BEHIND BARS, thats where the truth is... next time


  nimeikuta ktk blog ya HARUSI YANGU.cheusi.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Natamani kuwaambia pole hao warembo ila hawastahili.
  Hayo ndo malipo yakutaka umaarafu na pesa za mteremko!!
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Habari ya kusikitisha, hapa nilipo machozi yananilenga. Yaani kwa kifupi NIMEGHADHABIKA SANA!

  Hii habari inanikumbusha na ile ya akina Mr. Sugu, na nyinginezo..Sielewi hili genge la wahalifu linalotumia burudani, urembo na michezo kujinufaisha ni lini litamulikwa na vyombo husika. Inasikitisha.

  Lakini ni kipi huyo 'mrembo' hakukitegemea? au hakusikia kauli ya JK 'Kula uliwe'? Hii ndio 'bad romance' alokuwa anaing'ang'ania. 'Bad romance' ime-backfire.

  Hivi vyombo vya kusimamia haki za wanawake na watoto viko wapi? au na wao ni wachumia tumboni tu.

  Wajameni twafa!
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  huu ni udaku pe se.....................
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Lil,

  Sidhani kama wanatakiwa kulaumiwa kiasi hicho. Sina hakika kama wote wanakuwa na taarifa kwamba watakutana na mambo ya namna hiyo. Na kama alivyosema mleta mada, hawa bado wanakuwa ni watoto wadogo, wenye kiu ya kujiletea maendeleo. Wanaotakiwa kupewa lawama ni wale ambao wamepata hayo matatizo halafu wanakaa kimya. Hata mimi sikujua kama kuna uchafu wa ajabu kiasi hiki. Kwa hiyo ningeweza kumruhusu binti yangu au kumshauri ndugu aingie kwenye hayo mashindano. Kwa wale wenye taarifa kama hizi basi ni vizuri waziweke wazi ili watu wajue kinachoendelea. Hii itasaidia kukomesha huo ufisadi na uhuni kwa watoto wetu!
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Dunia ya sasa ime-adopt mfumo wa kila individual kutaka kuwa mbele ya mwingine, na mtu asipokuwa mbele ya mwingine yaani 'hajisikii'. Huu ndo mfumo wa kutaka ku-compete ktk kila kitu, na mzizi wake haswa ni ubinafsi.Huyo binti for whatever the reason alishiriki kwenye hayo mashindano akiwa na motives za kibinafsi ktk mashindano ya kibinafsi. Ukishaingia kwenye mashindano ambayo kuna mshindi mmoja tu huezi uka-limit mbinu za kibinafsi ambazo lazima zitakuwa na muelekeo wa kibinafsi na kunapokuwa na ubinafsi uhalifu shurti ubishe hodi.

  Pengine hakuwa informed kama ulivosema kuhusu hao wanaoitwa 'vigogo' na mtandao wao wa kihalifu, lakini hiyo haiondoi share yake ya lawama.
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  aaah hii habari imenishtua sana...kumbe mambo ndio hivi...kweli Tanzania bila ukimwi haiwezekani...people are very dirty
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hata mimi sijasema hawana lawama. Kwa hiyo nakubaliana na wewe kwamba wanastahili lawama kiasi fulani.

  Hata hivyo kuna baadhi ya washiriki wanakutana na hayo mambo baada ya kuingia kwenye mashindano. Na hapo ndipo hoja yangu inapolalia. Kama wangeingia kwenye mashindano hali wakijua kuwa kuna mchezo mchafu basi lawama zingekuwa kwao, kwani wangekuwa wamejitakia wenyewe kwa sababu ya tamaa zao au malengo binafsi. Kuna dada mmoja toka mikoani alikutana na hivyo vituko na kukata tamaa ya mashindani, hadi hakuweza kuingia kwenye 10 bora ingawa alikuwa na uwezo/vigezo. Mimi naona sasa ni muda muafaka kuweka haya mambo wazi ili wazazi wasiruhusu watoto wao kushiriki kweye huu uhuni au wale watakaoshiri wawe wamejiandaa kwa hayo mambo.
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nimekuelewa..mkulu..

  Nadhani jamii nzima inatakiwa iwe makini na kuchukua hatua. Kuanzia watoto wa kike wenyewe, walezi na wazazi, media, na mwisho vyombo husika vya dola. Wahanga pamoja na kushiriki kwenye kosa, wangekuwa vinara wa ku-create awareness, ingeweka impact sana. Hivi wanavoendelea kujificha ndio tabia inavozidi kuota mizizi.
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  AK huu si udaku ni habari zakweli ndani ya urembo ..zinasikitisha sana ..sijui hata kwenye mashindano makubwa ya dunia mambo huwa ndo haya haya ?
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  FL1,

  Siamini kama kwenye mashindano makubwa ngazi ya dunia huu upuuzi upo. Kama ungekuwepo watu wangeshauweka wazi (expose) na wahusika wangeshachukulia hatu siku nyingi. Kunaweza kuwepo siasa au michezo mingine isiyofaa (kama vile upendeleo) ila siamini kama kuna ufuska, na kwamba watoto wa watu wanachaguliwa changuliwa kama dagaa au watumwa. Ni jambo la kusikitisha sana. Naamini huu ufisadi wa kuwafanya watoto wetu mitambo ya ngono unatokea hapa Tz tu.
   
 12. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  nadhani kwenye mashindano makubwa inakuwa ngumu na pale wanaangalia vigezo vya kweli sio huku kwetu, embu angalia kama Wema Sepetu, unaweza kuniambia alipita kihalali? kwa mtazamo wangu mimi kwa mwaka ule alitakiwa awe Jokate maana hata kichwani kuna kitu
   
 13. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Tamaa iliua fisi, siku hizi watu wanapenda sana njia za mkato za kujipatia fedha na kupenda sana maisha ya juu ilhali huna kipato au shule ya kukufikisha hapo ulipo. haya ndo MALIPIZI yake!
   
 14. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kwenye mashindano makubwa hakuna huu upuuzi labda ubaguzi wa rangi ndio umekuwa ukisikika.
   
 15. bht

  bht JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Lakini hawa 'watoto' jamani ndo utoto na kutaka huo umiss to the exten that you dont even care about your dignity?
  Kuna vitisho vinaambatana na such proposals?
  Hawawezi hata ku-open up such ana issue to someone close to them like a mother, sister au mwingine yeyote?
  It is so unfair kw amijitu ya namna hito kuwa-deprive hawa watoto maisha yao yenye heshima.
  Shame on them na kuna siku tu yaja watagusa siko.................!!
   
 16. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  hili tatizo ni la pande 3,kwanza kabisa vyombo husika vya serikali vilitakiwa kung'aza jicho kali ktk hii fani hasa ukizingatia inamhusu mtoto wa kike,lkn kama ni kweli yaliyosemwa,inaonesha vigogo hawa wananguvu za kufanya vyombo husika vya kiserikali vifumbe macho.
  pili.kamati y miss tanzania ilitakiwa iyaendeshe mashindano haya ktk njia zitakazomlinda na kumnufaisha miss na taifa kwa ujumla.
  tatu,hawa wadogo zetu nao wasikwepe lawama maana wana uwezo wakusema hapana to ufirauni huu lkn kwa vile wanataka kuwa matajiri overnight basi wanajikuta wakitumbukia ktk matatizo.
  miss ndiye mwenye jukumu la kujilinda na kuvikataa vitendo vichafu,sasa kama huyo miriam atakwepa vipi lawama za kukubali kuwa na likigogo si ajabu hata halipigi mswaki huku akijua halipendi.
  bwana hawa mamiss pia tusiwatetee sana kwanza wengine wakubwa tu tumelingana nao wanajifanya watoto wakati akili zimeshakomaa,maana kama wao watavikataa hivi vitendo basi mchezo utaisha hata kama serikali na kamati ya miss tz itakuwa bado imeamua kufumba macho.
   
 17. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yani Tz imeoza kila kona. Hii sio nchi kabisa. Ni jalala!! I wish we could clean up and start afresh! Cha kusikitisha maskini ndo wanaonewa! Siku moja, watalipa yote!!
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Apr 12, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nimekupata DC.
  Ila swali langu ni kwamba wakishagundua kua hali yenyewe ndo hiyo ya nipe nikupe kwanini wasijitoe???Kama mtu anaona sawa kujitoa mhanga ili ashinde utamsaidia vipi?
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Apr 12, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Lil,

  Sidhani kama kuna haja ya kuhangaika na mtu mzima aliyefanya maamuzi huku akijua kila kitu (informed decision) kuhusu jambo analolifanya na madhara yake. Ndio maana hakuna mtu anayesikitika sana (ingawa ni vibaya pia) kwa vitendo vinavyofanywa na machangu.

  Mimi naguswa na kusikitika ikiwa baadhi ya watoto wetu wanakutana na hayo mambo baada ya kuingia kambini. Kwani wakati huo kila binti anakuwa tayari ameshaweka malengo.na labda kuanza kuota ndoto za kushinda. Kama siyo imara, binti wa namna hayo anakuwa rahisi kurubuniwa. Mfumo mzima wa haya mashindano inabidi upigwe chini ili tuanze upya au tuache kabisa.
   
Loading...