The traveller diaries

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,260
9,705
Katika harakati za kutafuta maisha, mwishoni mwa miaka ya 90, niliamua kuondoka nyumbani na kuzamia bila passport wala ela ya kutosha.

Lengo lilikuwa kufika Italy au Spain kwa maana maisha ya nyumbani yalikuwa magumu na sikuona namna ya kutoka kimaisha.

Hivyo nimeamua kuwa nawapa mikasa kadhaa niliyokumbana nayo.

SHIRIKISHA WATU WA KARIBU UNAPOKUWA NA TATIZO.

Mwaka 2000, ulinikuta nikiwa Libya katika mji wa Tripoli.

Safari yangu ya kufika Libya haikuwa rahisi kwani nilipata majanga mengi kiasi kwamba kuna wakati nilikata tamaa na kuomba malaika mtoa roho aje anichukue. Si kwamba huo mwaka 2000 nilikuwa nina maisha mazuri hapo Tripoli, lakini walau nilikuwa na sehemu ya kulaza ubavu wangu japo kula kulikuwa kwa mashaka.

Nikiwa na marafiki wawili tuliokutana katika harakati za kusafiri ambapo mmoja alikuwa raia wa Cameroon huku mwingine akiwa ametoka Burkina faso, tulikuwa tukiishi geto ambalo huyo wa Cameroon alikuwa amefanikiwa kulipia kodi baada ya kufanya biashara flani haramu na kufanikiwa kupata kiasi flani cha pesa.

Kwenye geto letu hakukuwa na kitu zaidi ya magodoro mawili, sufuria tatu, vikombe vinne, sahani kadhaa na ndoo za kuhufadhia maji.

Tv na redio kwetu ilikuwa ni anasa kweli kiasi kwamba hatukuwa na wazo hata la kumiliki hivyo vitu kwa muda huo kutokana na kutokuwa na pesa ila pia pale tulikuwa tumeweka kambi kwa muda tulitafuta njia ya kuendelea na safari ili kufika Ulaya. Siku moja ninaamka asubuhi kama kawaida, ninafumbua macho, sioni mwanga bali giza limetawala.
Napekecha macho nikihisi labda hayajafunguka vizuri lakini bado sioni chochote.
Nanyanyuka napapasa ukuta nikitafuta zilipo ndoo za maji nanawa uso lakini bado sioni kitu.

Naanza piga kelele nikiwaita wenzangu, hofu inanijaa mwenzenu ndiyo nimekuwa kipofu au nimekumbwa na nini. Inapofika mchana, wenzangu wananikokota mpaka hospital kumwona daktari wa macho.

Ananipima kwenye mashine ya lens lakini sion chochote licha ya kubadili lens kadhaa.
Narudi nyumbani baada ya kupewa dawa ambazo ninatumia kwa muda lakini matokeo siyaoni macho yanabaki vile vile.

Wiki mbili zinapita nikiwa nimeshakata tamaa kabisa na kujiona nimekuwa kipofu ugenini.
Siku moja anakuja kijana mmoja anaitwa Piere nilikutana naye Mali, naye ni traveller kama mimi. Ananikuta nikiwa katika hali mbaya sana, anashangaa kilichonisibu.
Ninamwambia hali halisi, ananibia Boby, shika hizi dawa, ananisha kikanja cha mkono wa kulia na kuniwekea tembe mbele za bidonge. Meza moja sasa hivi na nyingine usiku, kisha ananipatia kiasi kidogo cha pesa ananiaga kuwa ana wenzake usiku huo huo wanasafiri.

Ninamshukuru na kumeza tembe moja hapo hapo kabla hajaondoka japo nilikuwa nimeshakata tamaa ya kuona tena. Baada yakama saa mbili toka nilipomeza hiyo tembe ya kidonge, mara ninaanza kuona nuru. Ninahisi kama ninaota, nanyanyuka nakuanza kupiga kelele siamini kilichotokea. Kweli "Man and God meet in a Common Ground".
Usiku nameza tembe iliyobaki ma kesho yake macho yangu yanakuwa sawa na ile hali ya kuuma kama yana mchanga inapotea.

Najifunza ukiwa na shida wambie watu huwezi jua ni yupi atakusaidia.

TUKIO LINGINE.
Mwaka 1997, nilikuwa Mali, tulikuwa watu wanne, huyo kijana aliyenipatia dawa ikaniponya macho, mwenzangu Mghana almaarufu kama Alhaj na Mcameroon mmoja kwa jina Fokka.

Tulitoka Mali tukaingia Algeria, na kama kawaida ya wasafiri kafiri, kila dili lilikuwa halali kwetu ili mradi tupate pesa ya kuzidi kusonga mbele. Mimi na Fokka tukapata deal flani ambalo tulimcheza raia mmoja wa Ufaransa tukapata pesa ndefu. Lakini bahati mbaya likaenda ndivyo sivyo tukakamatwa na ikawa habari kubwa tukatangazwa kwenye vyombo vya habari vya Algeria. Ili tusiingie sote gerezani ikanibidi mimi nimtetee Fokka nifungwe mimi, nikiwa na lengo kwa Fokka akiwa nje anaweza nisaidia kuliko sote tufugwe.

Na kweli nikapigwa kifungi cha miezi sita gerezani. Fokka alivyoachiwa sikuwahi kumuona wala hakuwa kuja kunintembelea. Maisha ya gerezani yalikuwa magumu sana na ukiwa ugenini huna hata marafiki hakuna mtu wa kukutembelea hata akuletee sabuni. Baada ya miezi sita, walinirudisha Mali maana walidhani mimi ni raia wa mali. Siku moja nikaenda kuoga kwenye dimbwi la maji ambako watu wanaogelea. Baada ya siku nne toka nimeoga kwenye lile dimbwi, nilipienda haja ndogo baada ya mkoji ikafuata damu.
Nikashangaa na kuogopa sana. Ikanibidi niende hospitali nikapewa dawa na kuanza kutumia lakini hali ile iliendelea.

Nikaenda hospitali nyingine nikapewa dawa bado hali hiyo ikaendelea. Lakini mimi lengo langu lilikuwa ni kwenda Guinea Conakry, ili nipate passport ya huko itakayo nisaidia kuelekea nchi za America ya Kusini. Kulikuwa na vita huko lakini sikujali lengo tu nifike huko. Nikowa naumwa hivyo hivyo nakaanza safari mpaka Senegal, nikaingia Gambia, then nikaingia Guinea Bissau na kufika Guinea Conakry. Hapo imeshapita kama miezi sita bado nakojoa damu. Nikafanikiwa kupata passport, nikasafiri mpaka Burkinafasso kule nilisikia kuna wenzangu wako huko.

Nilipofika hali yangu ikawa imedorora sana nikahisi huu ugonjwa utaniua. Nikakutana na kijana anaitwa Prince ambaye tulikutana Togo siku za nyuma, nikamueleza tatizo langu.
Huyo kijana alikuwa na kaka yake ajulikanaye kama Andre Korie, yeye alikuwa mtu mzima na alikuwa ameshasafiri sana kuliko sisi sote hivyo alikuwa mzoefu sana wa majanga. Kwa hiyo Prince akashauri nikamweleze tatizo langu kaka yake, nilipomweleza akasema hilo tatizo dogo sana. Nikamwambia tatizo dogo wakati nimeenda hospitali zaidi ya nne na inaelekea miezi nane siponi kila siku nakojoa mkojo ukiisha inafuata damu.

Akaniambia sikia, akaniandikia jina la dawa kwenye karatasi akaniambia nenda kanunue.
Nikaenda na kununua hiyo dawa nikuandikiwa 1*2 kwa siku sita. Ajabu siku ya tatu tu damu ikaacha kutoka. Kwa experience niliyopitia, kuwambia watu wa karibu majanga yako muda mwingine inasaidia sana.

Tukutane tena kwa visa vingine vya kijana wenu Msafir..
===========================================

Jana niliandika sehemu ya kwanza katika visa nilivyokutana navyo kwenye harakati za kutafuta maisha kwa kuzamia.
Mwaka 1996, nilikuwa Chad, pale nilikaa kama miezi mitatu nikitafuta msaada wa kuingia Libya maana sikuwa na passport.
Siku moja akaja mtu akaniambia kuna gari inaelekea Libya itaondoka usiku kwa kupita njia za panya maana itakuwa imebeba wahamiaji haramu.
Mtu mmoja kumpeleka mpaka Tripoli ilikuwa wanataka CFA 300,000 ambazo kwa sasa kwa pesa ya Tanzania ni kama 1,200,000.
Hiyo pesa sikuwa nayo, ila nikamwambia jamaa anipeleke kwa hao watu.
Alinipeleka nikaonana na mhusika nikaongea naye na kumwambia kuwa nina CFA 180,000 tu.
Akasema kwa pesa hiyo ataniacha mji mmoja unaitwa Kufra, ni mji mdogo uko Libya katika jangwa.
Mimi nikasema sawa tu kwakuwa nitakuwa nimeingia Libya, kumbe sikujua najipeleka motoni.
Maandilizi ya safari, sahau vyote lakini siyo maji, inabidi kubeba maji mengi maana safari inachukua zaidi ya week kwa kukatisha jangwani tena kupitia njia za panya na dereva anasafiri kqa kufuata nyota.
Mchana kuna joto kali sana na muda mwingine mnaweza kukumbana na kimbunga cha mchanga.
Ni safari ngumu sana watu wanafia njiani na ikitokea gari likapata hitilafu, basi jua una 80% ya kufa huko maana usitegemee utapata msaada kwa maana ni njia za panya hakuna magari yanapita huko labda wawe wanaosafirisha wahamiaji haramu.
Safari ilianza usiku, kwenye gari tulikuwa watu 16, ukiongeza dereva na msaidizi wake jumla 18.
Tulisafiri usiku kucha huku mchana tukitulia jangwani kusubiri giza, maana walikuwa wanafuata nyota.
Katika safari hiyo kulikuwa na jamaa flani anaitwa Deusdon, ambaye naye alikuwa ametokea nilikotokea mimi kwa hiyo tukawa marafiki tukawa tunaitana kaka.
Kila abiria alikuwa na maji yake na chakula chake yani ukiishiwa maji hakuna wa kukupa maji utakufa tu mwenyewe.
Baada ya siku 13, tukafika kwenye huo mji wa Kufra, ulikuwa mji mdogo sana kwa kipindi kile sijui kwa sasa, na kwakuwa uko kwenye jangwa hakuna lolote na mimi kama nilivyokwisha sema nikaambiwa safari yangu inaishia pale.

JEHANAMU HUENDA IKO DUNIANI PIA.

Yule mwenzangu Deusdon, alikuwa ana pesa, nikamuomba anilipie nikifika Tripoli nitatafuta pesa yake nimrudishie kwa maana sikuwa nafikiria kuwa Kufra ni jangwa ila baada ya kuona hali ya pale nikajua nitafia pale.
Deusdon akagoma kabisa, mmoja ya wale watu tuliokuwa nao akamwambia unamuacha hapa ndugu yako afe, atakufa huyu hata wiki hawezi kumaliza.
Na kweli wakaniacha pale gari likaondoka.
Sikuwa na pesa sikuwa na chochote na maji yalikuwa yamebaki kama lita moja.
Siku ya pili tu nilikuwa nimeshakata tamaa nimeshanywea nikiwa najiona nakufa wazi wazi.
Nilikuwa nikilala nje, mchana joto kali na usiku kwenye jangwa kuja baridi kweli kweli.
Baada ya siku nane nikawa nimeshaona hakuna namna nitakufa tu, na mbaya zaidi usiku wakati nimelala nikang'atwa na ng'e wa jangwani wana sumu kali.
Kesho yake niko hoi hata kunyanyuka siwez natamani Malaika mtoa roho aje anichukue.
Macho yameshaanza kupoteza nuru, sina maji sijala nina njaa kweli, mara akaja bibi mmoja akanisogelea.
Akawa anazungumza lugha ambayo mimi sikuwa ninaielewa sijui ni Kiarabu au lugha gani.
Akamwita mtu mwingine wakanibeba wakanipeleka kwenye nyumba yake.
Akaanza nitibia jeraha lililosababishwa na ng'e pia akanipa maji na kuninywesha dawa iliyosababisha nitapike.
Tumboni hakukuwa ni kitu nusura nitapike utumbo.
Nikapitiwa usingizi nakulala. Bibi alinihudumia vizuri kama baada ya wiki nikapona kabisa na nguvu ikarudi.
Siku moja akaja kijana ambaye naye kumbe alikuwa anatafuta ela ya kwenda Tripoli, ila yeye alikuwa Mlibya, tukawa marafiki sana nikawa nazunguka naye mara nyingi.
Kuna siku akasema kuna choo kinahitaji kutapishwa kimejaa, choo chenyewe cha shimo.
Nikakwambia sawa tukapige kazi, kwenda tukashauriana kwamba tuchimbe shimo lingine pembeni, halafu tutoboe tundu ili uchafu uhamie kwenye shimo jipya.
Na kweli kazi ya kuchinba shimo ikaanza.
Joto kali lakini hatujali tukachinba shino kama futi nane kwenda chini na futu nne upana.
Tulipotoboa tukakuta kumbe yale mavi yamekauka kabisa yani kutokana na joto la jangwani.
Solution ikabidi tuanze kuyacota na ndoo tunayahamishia huku kwenye shimo jipya.
Kufikia jioni kazi ikawa imekwisha tukapewa pesa yetu.

MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI

kesho yake sina hili wala lile, anakuja jamaa anadai kwamba kuna mtu kapigwa na kutupwa kule jangwani lazima atakufa anatuhumiwa kwa kuiba ela.
Kusikia hivyo nanyanyuka namuuliza wapi ananielekeza, navua shati nalilowesha na maji nalifunha kichwani, ninatoka mbio mpaka nilipoelekezwa.
Jua kaki joto kali mpaka jangwa linakuwa kama linapiga kelele, kufika nakuta mtu mwili wote umetapakaa damu hajitambui.
Kumsogelea na kumtazama, Mungu wangu kunbe ni Deusdon.
Najiuliza huyo si inabidi awe Tripoli kafikaje tena hapa.
Namnyanyua namweka begani nakimbia naye kurudi kwa jamaa yangu.
Nafika namwagia maji, ela niliyolipwa kama ujira wa kutapisha choo naenda nunulia dawa na bandage.
Natibu madonda yake na namfunga bandage.
Baadae anarudiwa na fahamu anashangaa kunikuta mimi ndiye niliyemwokoa.
Aliona aibu sana akanishukuru na kuonba sana samahani.
Akaniambia waliponiacha pale wakaendelea na safari gari liliharibika njiani kabla ya kufika Tripoli.
Kwa hiyo walikaa wakisubiri gari lingine au aliyefuata spare arudi.
Baadae yeye na jamaa mwingien walipata gari iliyokuwa inaelekea Chad hivyo wakarudi nayo mpka Kufra.
Sasa yeye na huyo mwenzake waliwaibua watu flani pesa nyingi na katika kuwasaka ndipo akakamatwa yeye na kupigwa kisha akatupwa jabgwani, lakini ela hawakuipata na akaniahidi kwamba iko mahali salama atanilipia nauli ya kunifikishq Tripoli na atanipa hata pesa ya ziada.
Baada ya siku tatu tulipata usafiri tukaelekea Tripoli..

Tukutane tena katika visa vya kijana wenu Mr Traveller.
Part 1 inapatikana hapa The traveller diaries
 
Nitakuwa hapa ila isiwe tu ya kutunga.

Ulifikaje west Afrika kutokea Tanzania maana naona stori imeanzia katikati?
 
Mkuu ilikuaje ukapita kote huko miaka hiyo ilikua rahisi kwenda Italy kwa kutumia visa na passport za babu wa magomeni maana passport zilikua na Picha za kubandua na visa za ujanja ujanja zilikua nyingi maana kabla ya Osama kukaguliwa ilikua sio sana kama kipindi hiki...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom