OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 437
1. Mizengo Pinda ni Nani?
Ocampo four na Pinda ninayemjua .
Mizengo Pinda ni kiongozi aliyejipatia umaarufu kwa kujiita mtoto wa mkulima, ambaye kwa sasa ni wazi kageuka kuwa mpiga dili mkubwa wa mjini. Baada ya kuona biashara yake ya awali ya kufuga nyuki hailipi ni wazi sasa amegeukia dili kubwa kubwa kama za IPTL/ESCROW. Pinda ni mwenyeji wa mkoa wa Katavi, na ni mhitimu wa shahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam 1974. Pinda amepata kuwa msaidizi wa Rais kuanzia 1982 hadi 1992 na baadaye kuwa karani wa Baraza la Mawaziri mwaka 1996-2000 na kisha aligombea jimbo la Mpanda 2000 na kupata ushindi.
Sifa kubwa na ya pekee ya Pinda ni UDHAIFU na kwa kweli kajizoolea umaarufu kwa hii sifa ya udhaifu mpaka mitaani kabatizwa jina la Mzee wa kulia lia. Huitaji kuwa na akili nyingi au uwe Professor kugundua ya kwamba Pinda ni dhaifu, na udhaifu wake haukuanza leo, amekuwa akishindwa mara kadhaa kuchukua hatua hata katika jambo linalogusa maslahi ya Umma moja kwa mmoja na kwa ujumla wake.
Ni Pinda huyu huyu katika kipindi chake tumeshuhudia kushamiri kwa baa la njaa, mgao wa umeme usio na kikomo, mara zote kukwama kwa bajeti za wizara ndani ya Bunge, kutokea kwa operation tokomeza binadamu (badala ya operation tokomeza majangili), mara zote amekuwa akishindwa kuchukua maamuzi magumu kwa watumishi wazembe na wa ovyo ovyo hasa wakurugenzi wa wilaya kisa tu wanamchangia katika kampeni zake kupitia ile akaunti ya NYAU, tumeshuhudia mauhaji ya wakulima na wafugaji yakizidi, tumeshuhudia kipindi ambacho serikali inalia, wananchi wanalia, wahisani wanalia, wadau wa maendeleo nao pia wanalia.
2. Mizengo na ESCROW Saga
Pamoja na udhaifu wake, kulia lia kwake ni jambo la wazi kwamba swala la ESCROW ndiyo mwisho wa Pinda (The fall of Pinda). Ni vigumu sana kumtenganisha Pinda na swala la ESCROW. Pinda kama mtendaji mkuu alikuwa anajua mchakato mzima wa uhamishaji wa fedha hizo katika akaunti ya Tegeta ESCROW, na kama halikuwa hajui basi tunazidi kuamini kuwa udhaifu wake umemfanya tena asiweze kugundua jambo linalogusa maslahi ya umma kama hilo, na mbaya zaidi alidiriki kudanganya wananchi tena kupitia chombo tukufu la Bunge ya kwamba fedha za ESCROW siyo fedha za umma wakati ripoti ya CAG limethibitisha pasipo shaka ya kwamba fedha hizo ni za umma.
Mitaani kuna minongono ya kwamba fedha hizo za ESCROW zinatumika katika kampeni za kumsaidia Pinda, na hata wachangiaji wakubwa wa kampeni hizo ni wahusika wenzake katika swala la ESCROW ambao nio bwana Muhongo na katibu wake M aswi. Kampeni meneja wa Pinda Bwana Masaburi Didas, amekuwa akiwezeshwa sana na hilo kundi ambapo kwa mwezi kapangiwa kupewa bajeti ya Million 460 kwa ajili ya kufanya operations. Ocampo four nimeshuhudia mara mbili fedha zikiingizwa katika akaunti ya Masaburi Namba 01j0045743161 (Hizo code mtajua ni Bank gani) tarehe 16/8/2014 na tarehe 23/10/2014 muwekaji akiwa kijana wa Maswi anayejulikana kwa jina la Mole.
Sakata hili la ESCROW limepelekea wahisani na wadau wa maendeleo kukata misaada ya fedha ambayo tafsiri yake ni kwamba mipango yote ya bajeti mwaka 2014/2015 itakwama kwa zaidi ya asilimia 75%. Ndiyo maana leo hii hakuna dawa katika hospitali zetu, watumishi tokea mwezi wa tisa hawajalipwa, wabunge wiki ya tatu hawajalipwa posho, wahandisi wanadai fedha nyingi sana na wengine wametoka site, huduma za msingi kama maji, elimu, umeme zinayumba, hakuna fedha za kulipa MSD, walimu wanakatwa fedha za kujenga maabara (wakati fedha za ESCROW zingeweza kujenga maabara kila kijiji, nchi nzima). Wahisani wamezidi kusisitiza kamwe hawatalegeza msimamo mpaka waone hatua zikichukuliwa naomba kunukuu There is no new development on this issue, so there is no change to our answers and stand Donor spokesperson Sinnika Antila..
NB: Pinda kweli kama unapenda wananchi na kama una huruma na watoto wa wakulima tafadhali sana chukua hatua na hatua bora kwako kwa sasa ni kujiuzulu, tayari ushachafuka na kamwe huwezi kusafishika machoni mwa watanzania.
Mytake: Ni wazi Pinda kalemewa, kashfa hii ya IPTL imemtikisa, hana pa kutokea, maana yuko kwenye wakati mgumu sana, yuko kwenye hati hati, ufisadi unazidi kutamalaki, na hata katika kashfa ya ujenzi wa bomba la gesi toka Mtwara kwenda Dar es Salaam ambayo imevunja rekodi ya ufisadi amekuwa akitajwa tajwa .. Pinda muda ndiyo huu, hakuna muda mwingine tena wa kujiuzulu ..
Asante
Ocampo four