THE RETURN OF XANDER CAGE: Filamu mpya inayosubiriwa kwa hamu duniani kote

Steven mushi mushi

JF-Expert Member
Jul 25, 2016
533
739
Hii ni filamu mpya kabisa inayosubiriwa na wapenzi wa filamu duniani kote. Filamu hii inatarajiwa kutolewa rasmi tarehe 7 January 2017. Ni filamu iliyochezwa na mastaa wakubwa wa filamu duniani kitu ambacho kimeifanya filamu hii iwe gumzo kote ulimwenguni,

Mastaa walioshiriki kuiandaa filamu hii ni Vin Diesel (Nyota wa filamu kutoka marekani, kwa wale wanaofuatilia filamu ya fast furious watakuwa wanamfahamu vizuri huyu jamaa ), Donnie yen ambaye ni nyota wa filamu kutoka nchini china, Tony jaa ambaye ni nyota wa filamu kutoka nchini Thailand,

Deepika padukone ambaye ni nyota wa kike wa kihindi miongoni mwa mastaa wengine wengi walioshiriki katika kuiandaa filamu hii. Na filamu hii kwa sasa unawezasema ndio habari ya mjini kutokana na kuanza kuonyeshwa kwa baadhi ya vipande vya filamu hii na tayari wachambuzi wa mambo wameshatabiri kuwa kuna uwezekano filamu ikavunja rekodi ya mauzo duniani.

Basi kama wewe ni mpenzi wa filamu usikose kujionea filamu hii ambayo ni moto wa kuotea mbali kwani ndani yake kuna aina tofauti za mapigano kuna action, kungfu na nyinginezo. THE RETURN OF XANDER CAGE coming soon 7 January 2017.
 
Ndiyo ile inayoitwa XXX. ...???...maana nimemuona Tony jaa kwenye mitandao ya kijamii akionyesha picha zake nyingi tu. ...
 
mimi katika muvi ambayo nimewahi kuona ina mkono ni THE RAID REDEMPTION ya singapore!ile muvi ni balaa wallah yule dogo anapiga mkono kinyama
Kuna nyingine inaitwa bodyguard 2016 ya kichina hii na yenyewe ni hatari kama hujaiona hebu itafute uiangalie
 
Donnie yen hatari sana juzi ameshirikishwa movie ya star wars rogue one dah anapiga mkono hatari aka ip man
 
Back
Top Bottom