smaki Mimi nataka kujua izo habari za shetani kufukuzwa ni Nani mwenye hakika nazoMkuu, Emalard umenikumbusha kauli ya shetani, eti anawambia waliokuwa Malaika wa mbinguni ''Mungu mjanja sana amejirundikia madaraka, ni mbaguzi amewapendelea wanadamu walioumbwa kwa tope tu yaani madongo.ujue yeye ameumbwa kwa mwanga, utla violet). Eti Mungu kwa hakika anataka tuwasujudie, msikubali hata sisituna weza''. Theluthi 3 ya malaika wote wakahasi wakamkubali na kumfuata Shweitani mpaka leo, sasa wewe leo hii umerudia yale yale ya mkuu wa ulimwengu alosema bila kujijua dhidi ya muumba wake, umeyatoa wapi kama siyo matunda yake .lazima alikunong'oneza ''kaseme tu''
Humu ndani kuna watu weeengi sana naweza kuwajua kirahisi tu, nani ndiye wa shetani na nani siye wa shetani, sasa basi jiulize asili yako wewe ni wapi?
Waafrika bwana unaweza kudhani amekuja na mada nzuri lakini huidhia kujadiri uchawi, iganga, majini na mauzauza tu.Nianze kwa kusema nakumbuka nikiwa bado mdogo mdogo, nilikuwa na sifa moja kubwa sana mtaani kwetu ya ubishi.
Hata kama ulete fact za kiwango gani lakini niki-stickkatika msimamo wangu ni hapo hapo hamuwezi kunibandua hata mngekuwa mia.
Lakini kuna jambo moja aliligundua mzee mmoja siji kumsahau katika maisha yangu yote ningali bado mdogo kabisa miaka 8.
Aliniita na kuniambia
""Nikiamua kuwa na maarifa naweza kuwa nayo, nakuambia hivi si kwamba nimekuona unamaarifa bali nimegundua unaweza kujaza maarifa ukitaka, sasa nakupa kazi jifunze ulimwengu uliofichika ulivyo hautapata nafasi ya kubishana na wengine kamwe'''
Mzee nilimuelewa japo kwa ufupi sana, labda kutokana na umri wangu ulivyokuwa na kuambiwa jambo lililokuwa juu ya uwezo wa frikra zangu.
Nikiwa na miaka 14 ndipo mzee aliweza kunipa kitabu kilichokuwa na Tittle Hii
"Comfort That Kills" Nikitabu chenye page 36 tu lakini ndicho kikabadili ukurasa wangu wa maisha na kunipa hamu zaidi ya kuujua ulimwengu uliofichika.
Nilikisoma kwa kufanya mirejeo mingi sana katika kamusi ya kufasiri maneno ya Kiingereza kwenda kiswahili,
kwanza kilikuwa na maneno mengi ya kiingereza cha zamani sana, kilinipa shida kidogo lakini niliweza kukielewa na kufunguliwa ukurasa mpya wa kusoma Maandishi.
Si kwamba sikuwa msomaji toka mwanzo ila nikwamba usomaji wangu uliegemea sana katika kusoma hadithi za nadharia zaidi zilizoandikwa na waandishi mbalimbali mahiri.
Sasa hapo ndipo nikaaznza kuufukunyua ulimwengu uliofichika kwa fujo zote.
Sio katika Upande wa Dini au Historia tu, bali niliweza kuyajua mabo mengi sanakwa muda mfupi.
Na kadri nilivyozidi kusoma ndivyo nilivyozidi kujua na kutambua ya kuwa katika asilimia 100% huenda nimeijaza asilimia 0.001%(Kwa wasomaji wavitabu wananielewa vizuri hapa maana kadri unavyosoma ndivyo unaona hauna kitu na unahitaji kujaza vitu)
Nilikuwa napitia Thread Za mtu mmoja humu(jina kapuni)
Niligundua jambo moja wengi wanaompinga katika thread zake ni wale wanaoangalia muvi na video za youtube juu ya uhalisia wa ulimwengu tunaoishi, lakini hawezi kuwa na mrejesho hata mmoja juu ya maandishi aliyoyasoma.
Huyu jamaa ameandika vitu vingi ambavyo huenda sikujua kama naweza kukutana na mtu kama huyo hapa, lakini ndipo nikajua kumbe JF ina watu wengi sana wa kila namna (Viva JF)
Sijaja Hapa kuueweka hadharani ulimwengu uliofichika ila ukihitaji kuujua unajulikana kabisa, tena kwa urahisi sana.
Labda unaweza ukakosa Mzii mahala pa kuanzia lakini nakupa kidogo jambo moja.
Jaribu kujifunza mambo kama haya hapa.
Kwa watu wa Imani hasa wakristo na waochimba masuala ya tulikotoka,kwanini iko hivi,kwanini iko vile,imekuwaje,ilikuwaje,jaribu kupitia mambo haya.
-Ni vitabu gani vilimeondolewa katika Biblia
Unaisoma Biblia Leo lakini inavitabu zaidi ya vitano havijawekwa humo
Tafuta kwanini havimo, vinafundisha nini, nk
-Ni nani alikuwa mmiliki wa kwanza wa America(Usiniambie wahindi wekundu nabaadhi ya maneno yaliyopo kajifunze ulimwengu uliofichika)
Naomba niishie hapo kwa Leo, lakini nikipata mda mzuri na nafasi nitaweza kuleta hoja mbalimbali juu ya ulimwengu uliofichika kwa kadiri ya jinsi nitakavyokuwa na muda.
Updates Ipo Page #30 Kitabu Chenye Utata (Kina Uwezo Wa Kujua Wakati Wako Ujao)
Upadates Ipo Page Ya #95 Nguvu Za Asili Alizonazo Mwanadamu Kumshinda Mchawi
Upadates Ipo Page Ya 128 Nguvu Za Asili Alizonazo Mwanadamu Kumshinda Mchawi Sehemu Ya Pili Na Mwisho
Waafrika bwana unaweza kudhani amekuja na mada nzuri lakini huidhia kujadiri uchawi, iganga, majini na mauzauza tu.
FUNGUKA MKUU TOA KAMWANGA KIDOGO MPAKA TUPATE HIVYO VITABU SI LEO. CHONDE CHONDE KAMANDAKuishi Katika Kusudi for 100%
Ishi Kiuaminifu na Mungu Wako MkuuFUNGUKA MKUU TOA KAMWANGA KIDOGO MPAKA TUPATE HIVYO VITABU SI LEO. CHONDE CHONDE KAMANDA
Hata maprofesa wetu wengi ktk ulimwengu uliofichika wako empty kabisa
KinaitwajeMkuu hicho kitabu nakifahamu na nilipewa na jamaa yangu bure kabisa miaka ya 2004. Nilikisoma jinsi ya kukitumia. Lakini niliogopa baada ya kuambiawa na mzee fulani aliyekua ni mchungaji mkogwe kwamba kila unapokitumia unapunguza umri wako wa kuishi. Ilibidi nimtafute alienipa nimrudishie. Bila mafanikio kwa sababu alihamiswa kikazi kweda mkoa mwingine nilikificha kabatini mpaka 2012. nilipoonana nae na kumrudishia. lakini kiuhalisia ni kama kitabu cha kupigia bao. hakifai kwa mtu mwenye imani yake ya Dini. kina mambo mazito. Wala mtoa mada hujakosea. Nilikua nawakusanya jamaa zangu kwenye Kahawa tunaanza tunaanza kutazamiana namba na maelekezo yake kwenye majedwali yake, hakikosei. yaani jioni tumetoka tu shuleni tayari dakika sifuri kundi la majamaa wananisbiri nje tuende kijiweni. Leo nikikumbuka dah !!
Wakuu, kwa anaye hitaji softcopy ya Kitabu hiki cha Napoleon, hii hapa link ya kudownload kwenye Google drive kuna mshkaji wang mmoja anayo softcopy amekuwa mwema kushare link :
Sijui iko sahihi:
wewe lijamaa unaongea maneno ya dhahab kabisa mm ni muislam ila maneno yako hayana mushkeli kabisa endelea kutuelimisha kijanaUmesema Vema Broo Nikweli kabisa na ndivyo kupitia Biblia inavyosema na ndio uhalisia wenyewe.
Ila kuna jambo nilazima ulijue
Kupitia shetani ni lazima ujifunze na kupitia Mungu nilazima ujifunze
Lakini ulazima wakujifunza upo nikwawale ambao hajazaliwa moja kwa moja na bahati hiyo yakuwa activated
Mfano Kuna mtu anazaliwa akiwa tayari ni mchawi na kuna mtu anazaliwa akiwa tayari ni chaguo la Mungu.
Akizaliwa akiwa mchawi hana msaada wa kujifunza uchawi tena bali atazidi kukua katika hali ya uchawi hadi uzeeni na kifo chake.
Na mtu akizaliwa katika hali ya kuchaguliwa na Mungu moja kwa moja utashangaa jinsi ambavyo anakuwa anatembea katika utukufu wa Mungu pasipo hata kufundishwa na mtu wa kupitia madarasa ya mafunzo ya biblia.
Atalieleza vyema neno la Mungu hata kuzidi wachungaji na maaskofu.
Lakini sasa tofauti na hapo ni lazima mtu mwingine achukue nafasi ya pekee kutafuta ile iliyo kweli ya Mungu au shetani.
Mfano Mtu unapaswa kusoma Neno la Mungu kila Siku, Kuomba Kila Siku tena pasipo Kukoma.
Kwahiyo Zile nguvu za Rohoni Zipo katika Nyanja Kuu Mbili Kuzaliwa nazo katika Asili Ya Pili Kujifunza.
Angalia Uhalisia Wa Kibinaadamu Hapa Ambao shetani anautumia na Mungu anautumia Pia.
Kua kitu kinaitwa Hisia
Mtu ambaye anaweza kuzimosa vizuri sana hisia zake ndio wale tunasema anamachale(Au Anandoto)
Unaweza ukawa unataka kwenda mahali lakini nafsi yako ikawa nzito sana ukaamua kulazimisha baadaye unapatwa na jambo baya huko kisha unajilaumu ""halafu moyo ulisita kweli kwenda huko lakini nilipuuzia""
Sasa vitu kama hivi nizawadi ambazo mwanadamu anapewa na Mungu bure kabisa ila sasa niwewe ujue kuitumia ipasavyo.
Kuna mahali Unasoma katika Biblia Anakuambia "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" Maana yake wokovu tunao nguvu tunazo Uzima tunao lakini maarifa ya jinsi gani utembee katika hayo yote ndio inakuwa vigumu.
Ndio maana kuna mtu anaweza kuomba kwa siku saba akajibiwa na mwingine dakika tu na akajibiwa.
Kinachokuwepo hapo ni viwango vya jinsi gani maarifa yako yamefunguka kujua namna ya Kumtafuta Mungu.
Kwahiyo Kuna upana sana namna ya kujua na kutafuta mambo ya sirini.
Hata katika dini Sio wote watafanikiwa kuzijua siri za wokovu japo kila mtu anaweza kuokolewa
Ni lazima mtu uwe na juhudi za ziada tena ndipo unaweza kuujua ukweli halisia nini Mungu anataka tufanye.
Kuna wakati hatuishi kwa kuzijua na kuzitambua sheria bali tunaishi kama watumwa tukiwa tumejibebesha sheria(Na hata katika Neno la Mungu Vivyo Hivyo)
Mkuu hivo vitabu uneweka PDF kabisaana jinsi ya Ku download inasumbua kwa sisi wenye tecno
Mkuu, weka majina ya vitabu watu watafute.Hakuna shaka mkuu sema asilimia kubwa ya vitabu nilivyo navyo ni hard copy
nitajitahidi nikiwa nazipata soft copy nitazileta humu
Mkuu hicho kitabu nakifahamu na nilipewa na jamaa yangu bure kabisa miaka ya 2004. Nilikisoma jinsi ya kukitumia. Lakini niliogopa baada ya kuambiawa na mzee fulani aliyekua ni mchungaji mkogwe kwamba kila unapokitumia unapunguza umri wako wa kuishi. Ilibidi nimtafute alienipa nimrudishie. Bila mafanikio kwa sababu alihamiswa kikazi kweda mkoa mwingine nilikificha kabatini mpaka 2012. nilipoonana nae na kumrudishia. lakini kiuhalisia ni kama kitabu cha kupigia bao. hakifai kwa mtu mwenye imani yake ya Dini. kina mambo mazito. Wala mtoa mada hujakosea. Nilikua nawakusanya jamaa zangu kwenye Kahawa tunaanza tunaanza kutazamiana namba na maelekezo yake kwenye majedwali yake, hakikosei. yaani jioni tumetoka tu shuleni tayari dakika sifuri kundi la majamaa wananisbiri nje tuende kijiweni. Leo nikikumbuka dah !!
Ni kweli kijana huru Mungu ni mbaguzi, ndivo alivo ameamua hivo hatabadilika. Kitanda cha baba silalii hata kwa dawa na chumbani kwake siingii hovyo, mpaka kwa ruhusa maalum je huo ni ubaguzi au ni nidhamu?Duh
Kwa iyo kama Mungu anamuumba mwanadam anamleta duniani alafu anampenda huyu na kumchukia mwingine huo si ubaguzi???