The Police force needs reform | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The Police force needs reform

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by chalamaganza, Jun 9, 2011.

 1. c

  chalamaganza Member

  #1
  Jun 9, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Members
  Napenda kutoa hoja kwamba kunahitajika kurekebisha jeshi la police liende na wakati. Ukitazama jinsi ambavyo jeshi la poice linavyofanya kazi hasa katika mambo yanayohusu haki ya kidemokrasia ya kuandamana kwa amani kunaonyeha jinsi utendaji wao bado upo katika kivuli cha mawazo ya police wa kikoloni ambayo ni kuzuia fujo. wakati umefika waelewe kuwa moja ya kazi zao ni kulinda usalama wa raia ili wafanya mambo yao kwa amani kama maandamano n.k ambayo ni haki yao.

  Lazima tukumbuke kwamba 'state violence and reppression' ilikuwa ni kazi ya police wa kikoloni ambao hawakutaka watu watoe mawazo yao e.g kudai uhuru. Sasa inapofikia nhi yetu in miaka 50 ya uhuru bado jeshi la poilice linafanya mambo ya kufanana na wakati wa ukoloni ni hatari na aibu. ninashindwa kuelewa kwa mfano, ni kwa sababu gani lazima watu wanaotaka kuandamana kwa amani (chama chochote au kikundi chochote) lazima waombe kibali police?
  Kazi ya police katika nchi zenye demokrasia ya kweli ni kulinda hao watu wanaotaka kuandamana kwa amani ili wawe huru na wafikishe ujumbe wao kwa umma. Ninapenda kutoa mawazo kwamba turekebishe mafunzo ya police yaendane na matakwa ya demokrasia, police wawe walinzi wa usalama wa raia na siyo kuonekana kama maadui kutokana na baadhi ya vitendo mfano yaliyotokea Musoma, Arusha nk. Uslama wa nchi ni jukumu la watu wote siyo wale wenye magwanda tu. Na ni lazima kweli polce wawe huru siyo kuonekana kama chombo cha serikali iliyo madarakani.
  Chalamaganza
   
 2. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  police ni kama wale wanyama tunaofuga nyumbani kwa ajili ya ulinzi yani wewe ukisema shikaaa.., nao wanakamata bila kujua ni mhalifu au vinginevyo, ... yeye anachojali ni amri aliyopewa na bosi wake tu
   
Loading...