The most popula ccm leader | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The most popula ccm leader

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kashaijabutege, Feb 22, 2011.

 1. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Makamba adaiwa ‘kuua majirani zake kwa kiu’ Send to a friend Monday, 21 February 2011 20:55 0diggsdigg


  [​IMG] KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba

  Elizabeth Suleyman
  KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, anadaiwa na wakazi wa Wazo Hill, jijini Dar es Salaam kujiunganishia maji nyumbani kwake yaliyopaswa kusambazwa kwa wakazi wa eneo hilo.
  Hata hivyo, Makamba amepuuza madai hayo akisema ana haki ya kuunganishiwa maji kama Mtanzania, ili mradi afuate taratibu na awe analipa ankara.Mwajuma Omari, mkazi wa eneo hilo, alisema wamekuwa wakitaabika kwa kukosa maji, kwa sababu bomba walilokuwa wakitegemea maeneo yao limeunganishwa kwa Makamba.
  “Hivi sasa tunataabika na hatuji hatima yetu, ukiwaeleza Dawasco wanadai wataunganisha mabomba mengine na kuendelea kuchimba visima,” alisema Omari.Mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye hakutaka kutajwa, alisema toka enzi za Mzee Rashid Kawawa, wakazi wa eneo hilo walikuwa wanategema maji yanayotoka kwenye mabomba hayo.“
  Tumekuwa tukijiuliza, iweje Dawasco waunganishe mabomba hayo kijanja kwa Makamba na kutufanya tukose maji kwa kulazimika kutumia ya kisima?” alihoji.
  Akizungumzia suala hilo ofisini kwake jana, Ofisa Uhusiano wa Dawasco, Merry Lyimo, alipuuza malalamiko ya wakazi hao kuwa hayana msingi wowote na kwamba, mabomba waliyofunga kwa Makamba hayahusiani na wakazi hao.
  Lyimo alisema walifunga bomba hilo kwa Makamba muda mrefu, hivyo malalamiko ya wananchi hao yakosa nguzo ya kusimamia. “Mbona wanamlalamikia yeye tu! Kwa sababu kama ni mabomba hayo tumeyafunga kwa watu wengi na kama hawana maji, Dawasco imejizatiti kuwawekea kisima ili wasikose kabisa,” alisema Lyimo na kuongeza:
  “Hatujaona sababu za msingi za wao kulalamika... Makamba ni mteja wetu wa muda mrefu na tayari ameuganishiwa maji, hivyo wanapaswa kusubiri, mradi endelevu wa kuwaongezea visima vingine ili wasikose maji.”
  Akizungumza kwa simu kuhusu malalamiko hayo, Makamba alisema yeye ni binadamu kama walivyo wengine, ana haki zote za kuunganishiwa maji.“Hao waliokueleza malalamiko hayo… siwezi kuyajibu ni vema ukaenda kwa walioniunganishia bomba la maji,” alisema Makamba na kuongeza:“Kigezo cha kuwa Katibu Mkuu wa CCM hakimaanishi sina haki ya kupewa maji, hivyo siwezi kuzungumzia hilo kawaulize Dawasco.”
  Alisema aliomba kuunganishiwa maji tangu mwaka 1994, akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na alifuata taratibu zote.
   
 2. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kwanza Makamba anakubali kwamba ameunganishiwa maji... lakini pili anasahau kwamba hayo atakua ameunganishwa kwa sababu ya cheo/nasafi yake na si vinginevyo......
   
 3. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo hao DAWASCO wameona waanze kuunganisha kwa Makamba sio?....hii inji hii?
   
 4. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  makamba ungewatolea nje bomba wachote bure majirani zako wasingelalamika , iweje we mtaa mzima ndo upate maji tuu? hata kama ni ufalme siohivo. huo ni uchawi, ushetani, roho mbaya, ila sishangai kama watanzania mmeshatugeuza ndondocha wenu! hata hili kwako sishangai, muogope mungu mafisadi hadi rohoni!!!
   
 5. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kwa mtazamo wangu,wewe kama kiongozi ukisikia raia wanalalamika kuhusu jambo fulani,inatakiw a uangalie njia mbadala za kutatua tatizo lake na si kuwajibu kama vile hujasoma !! majibu ya mkuu yanaonyesha kaishia darasa la sifuri naweza kusema hajui hata kwanini ni katibu wa sisiemu! we kama kiongozi wasaidie kuwaelekeza hao ili kuondoa tatizo lao na sio kusema ati kawaulize Dawasco!! kwanza hiyo ni jeuri,jibu hili halionyeshe busara,hayo ni majibu ya kigadafi gadafi!! mi nashindwa kuelewa viongozi wetu kwanini hawana busara! wanadhani kila kitu ni ubabe,hivi kweli hata Mitume wa Mungu (a.s) wangelikuwa kama viongozi wetu wa leo,watuwangeam ini kweli wayasemayo?

  mi nadhani kuna haja ya kujifunza na kujua nini maana ya uongozi!wengine wanavamia tu madaraka na vyeo!! mi bora tu nife bila kuwa kiongozi kama hali yenyewe ndio hivyo!!
   
 6. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Makamba wagawie na wenzako maji, hawa ni watanzania wenzanko na pia kuna wanaCCM wenzako hapo mtaani kwako? Mnafisadi hadi maji jamani, ya dowans yanatosha na huyo jamaa enu anayedai mmiliki si amekuja na hataki kuonekana hadharani!Tanue ni tu maana siku zinakuja ambazo mtatafutana msionane!
   
 7. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  mambo mengi hugundulika pale kiongozi anapotoka madarakani kama tulivyoona raisi wa tunisia aliyeondolewa madarakani baada ya maandamano. kwenda kufungua safe yake kilischoonekana hata shetani ukimuhoji atakana kuwa yeye hakumtuma. vilevile Makamba hilo ni dogo tu lililojulikana kwa sasa, isije baadae wakakuta mkono wa albino kwenye safe yake hilo walaa halitaushangaza umma wa tanzania
   
 8. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Aisee Merry Lymo KILAZANyie DAWASCO huyu ofisa uhusiano wenu ni mbuzi kabisa,anajibu malalamiko ya wateja kama hakwenda shule,mlimwokot a wapi huyu?Kweli Makamba ni raia kama wengine,hivyo nae anayo haki ya kupata maji. Tatizo ofisa uhusiano wenu hajui kujenga hoja,anajibu kama anatoka chooni vile!wateja wanalalamikia kukkosa maji yeye anasema haoni sababu za msingi za wao kulalamika.....ana akili kweli huyu? binadamu ataishi pasina huduma ya maji...kwanini asilalamike kama anaona watu wanaunganishiwa maji kwa upendeleo?Kwanini wao wakae wasubiri hadi watakapochimbiw a visima ilhali familia ya mtu mmoja/wachache wakiogelea kwenye maji kama bata?Au Makamba ndiye alimpigia debe mtu kilaza kama huyu kupata ajira DAWASCO?
   
 9. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Hata Egypt ilianzia huko, "kupuuza malalamiko ya wananchi wengi".

  1. kuna tija gani kwa Dawasco kutumia 'resources' zake kumpatia maji Makamba ilhali wananchi wengine hawana hitaji hilo muhimu kwa uhai?

  2. Kwa nini kama Dawasco wameweza kuwa na 'resources' za kumuunganishia maji Makamba wasifanye hivyo kwa wananchi wengine?

  3. Dawasco wangewajibika vipi iwapo wananchi wote wa Wazo-hill wangekuwa Makatibu-wakuu wa CCM (Taifa)?

  4. Iweje Makamba apewe maji ya bomba na wananchi wengine waambiwe watachimbiwa visima?
   
Loading...