Moja ya the so called maajabu yake ni kuwa pamoja na umaarufu wake, picha him haina nyusi. Lakini pia ilisadikiwa ilichorwa na Mtaliano maarufu aliyekuwa anaitwa Leonardo da Vinci. Mwanamke aliyechorwa inasadikika kuwa ni Lisa Gheraldini mke wa Francesco del Giocondo ambae alikuwa mfanyi biashara tajiri wa hariri (silk merchant) na inasadikiwa ilichorwa kati ya mwaka 1503 na 1506. Neno Mona ni la kitaliano lina maana ya Ma'am, au madam au my lady kwa kingereza. Moja ya sifa adimu za Leonard da Vinci ni kwamba inasadikiwa alikuwa na uwezo wa kuandika kwa mkono moja na kuchora kwa mkono mwingine kwa wakati mmoja!