The middle class card

mshamba mchangamfu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
338
91
Mimi si mfuatiliaji sana wa maswala ya siasa ila kwa tukio la hivi karibuni la viongozi wa Chadema kutakiwa kulipa faini ya Tsh. 350mil nadhani kila mtanzania kwa nafasi yake amekuwa akilifuatilia hili

Nilijiulizwa maswali kazaa wakati nikishusha ka eagle baridi ili nikajilaze na uchovu wa siku kwanini Chadema wameamua kuchangisha hizi Tsh.350 mil?

Ina maana hawana kwenye account ya chama hizi hela ? Je washtakiwa mmoja mmoja kwa nafasi yake anakosa kujilipia?

Mtu kama Mhe. Mbowe amekuwa akisifika huku kwenye ma bar wa kuwa na ukwasi wa kutosha tu, kwanini nae atake kuchangiwa na wapiga debe wa Ubungo au wale wajasiriamali wa Mabibo?

Lakini miongoni mwa vitu vilivyo nishangaza ni muitikio wa watu kwenye hili la kuchangia mpk naandika hapa update nilizonazo Chadema walikuwa wamebakiza Tsh.90mil tu kuhakikisha viongozi wote wapo huru na baadhi tayari walikuwa wameshatoka

Kwa mazingira ya the all issue sina shaka kuwa watu wengi waliguswa na wamejitolea kwa hali na mali ila sidhani kama utapingana na mm kwa namna kampeni hii ilivyoendeshwa wachangiaji wakubwa ni hawa watu wanaoitwa middle class kwa nchi zetu za LDC mtu kuwa middle class ni kama tu unauwezo wa kupata $2

-$20 kwa siku lakini hili ndo kundi la watu ambao wana elimu, wana uwezo wa kupata huduma nzuri za afya wao na familia zao (ambazo si kubwa sana kimuundo) na wanakazi au biashara za kuhakikisha vipato vyao na hawa kihistoria ndio wamekuwa wakianzisha au kusupport sana mageuzi ya kidemokrasia je chadema walitaka tumia karata ya hawa watu?

Au hawa kuwa kweli na hizo pesa?Maana Chadema walianza kuonekana irrelevant kwenye siasa za nchi hii.
 
Kumbe AC zote zilifungwa na serikali ili wakaozee jela,cha ajabu kilichotokea sasa mpaka wanaona aibu
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom