The Magic Ring

RIWAYA…..THE MAGIC RING ( 14 )
MTUNZI….. HUSSEIN O. MOLITO
+255 (0)718 97 56 59
Iliandaliwa mikakati kabambe ya harusi yetu . kila kiumbe wa huko alipata taarifa juu ya harusi yetu iliyopangwa kufungika siku tatu mbele.
“Edward akisikia atachanganyikiwa eeh?” nilimuuliza mpenzi wangu tulipokua katika maandalizi ya mwisho ya harusi.
“kuna hatari ya kupoteza maisha kabisa kama atachukulia hii ni malipizo kwa aliyonitendea.”aliongea mpenzi wangu kinyonge. Baada ya kumtazama alitabasamu na kuwa mpole tena.
Siku iliyosubiriwa kwa hamu ilifika na wote tuliudhuria kwenye ukumbi mkubwa wa Damina uliokua ukitumika kwa mikutano mikubwa au harusi kubwa. Viumbe wote walipenda kuhudhuruia harusi hiyo ya kihistoria iliyohusisha binaadammu na jini huyo aina ya Fundy.
Ilikua ni ajabu sana kwa watu hao waliohudhuria baada ya kuniona nikiwa nimevaa mavazi yao na kunikaa ivizuri kabisa.
Mkuu wa majini alisimama na kuanza kuhutubia viumbe hao waliokuwepo humu ndani. Walikua maelfu kwa maelfu huku wote wakitumia lugha moja tu.
“sasa tunatakiwa tuwe kimya kwa ajili ya kumruhusu Jaji wetu aje awafungisha ndoa hawa wapendanao.” Aliongea mkuu wa majini na kuwafanya watu wote waliohudhuria hapo kutulia kimya.
Alikuja jaji kama vile tupo mahakamani na kunisogelea pale nilipo.
“upo tayari kumuoa Rosemary Pentzel?”
Aliniuliza hilo swali lililonifanya niitikie haraka.
“nipo tayari.”
Nilijibu na kumfanya Yule jaji arudie kuniuliza swali hilo mara tatu. Baada ya kujibu kua nimekubali na nipo tayari. Alihamia kwa mke wangu mtarajiwa.
“nipo tayari”
Alijibu pia mara tatu na kusababisha taratibu zingine ikiwemo matambiko kuendelea.
Ilituchukua masaa matatu katika kukamilika kwa viapo na mambo yote ambayo nilikua siyajui ila nililazimika kufanya ili nisije kuharibu mambo.
Tulipitishwa kwa wazee waliokua wamekaa kwenye meza kuu na kupewa Baraka zao. Baada ya hapo tulirudi mbele ya jaji na yeye akahitimisha kwa kuwatangazia viumbe waliokuwwemo humo kuwa tumeshakua kitu kimoja.
Shangwe, vigeregere na vifijo zilisikika kutoka kila pande huku viumbe wote wakisifia jinsi tulivyokua tumeendana.
Tulitoka ukumbini taratibu na baada ya kufika nje ya ukumbi. Tulimuona Edward akiwa na mke wake huku wakiwa wameshika maua.
“kuanzia leo, sina ugomvi na nyinyi. Naomba mnisamehe na mpokee maua yetu kama ishara ya kutengeneza amani kati yetu.”
Aliongea Edward na kutukabidhi yale maua. Tuliyapokea na kukumbatiana nao kuonyesha kua hatukua na kinyongo nao.
Muda mfupi baadae, wallikuja wanyama wawili wakubwa wanaofanana kabisa na farasi. Ila walikua wamebeba kijumba kizuri kilichokua na magurudumu makubwa. Tulipanda ngazi na kuingia kwenye kijumba hicho tayari kwa ajili ya kwenda kula fungate.
******************
Nilishtuka kutoka kwenye usingizi mzito ambao hata sikujua nilitumia muda gani kulala. Baada ya kupapasa huku na huko ili nimuangalie mke wangu. Sikuweza kumuona. Niliamka na kuita huku nikikagua chumba mpaka chooni ambapo sikumuona pia.
Nilirudi kitandani na kukuta kikaratasi.
“najua utajiuliza kwanini nimeamua kukuotesha ndoto kama hii. Ila ukweli ni kwamba. Japo hivi sasa nimerudiana na mpenzi wangu Edward, ila nahisi bado ana uhusiano na mwanamke mwengine. Yote hayo ni makisio tu. Ila ukweli ni kwamba. Nimetokea kukupenda sana Deo. Na kama nikibainisha kua kuna ukweli juu ya hisia zangu kua mpenzi wangu ananisaliti, basi nitarudi kwako na kuifanya ndoto hii kua ya ukweli kabisa…wako akupendaye, Rosemary.”
Kikaratasi hicho kilinifanya nishushe pumzi. Sikua nawaza kabisa kua ushindi ule ni ndoto.
Nilikikagua kile chumba na ndipo nilipohakikisha kua nilikua kwenye chumba nilichopewa na Al-hadad.
Kabla sijakaa vizuri, simu yangu iliita. Nilipoangalia jina kwenye kioo cha simu yangu. Lilisomeka jina la Martha. Niliipokea haraka na kumsikiliza.
“unakuja saa ngapi baby?”
Aliongea hivyo baada ya salamu.
“jioni.. au usiku kama vipi.” Nilijibu huku nikiwa nafikiria ile picha ya jini kichwani kwangu.
“poa… I love you.”
Alimaliza hivyo nami nilipomjibu, nilikata simu.
“Hizi ndoto zingine jamani, mungu aniepushie mbali.”
Niliongea hivyo na kwenda kuoga. Niliporudi, nilishangaa baada ya kuona chumba changu kinanukia harufu nzuri ya Yule jini. Hapo ndipo nilipoamini kua, japo kua hayupo na mimi. Ila kuna ukweli kua nitakuja kuishi maisha yote ya ndoto niliyoishi na yeye.
MWISHO WA SEASON 1………………………
 

Martha kajitakia mwenye... kilanga kimemponza...

Pete kwanza kaichukua kinguvu kwa jamaa yake, alafu bado anaenda kuiuza bila ridhaa yoyote...


Cc: mahondaw
 
Hapa kuna harufu ya jamaa kuanzisha mapenzi/mahusiano na jini...

Watakuja kupendana hawa, alafu vita ije kuanza kati ya binadamu na majini...


Cc: mahondaw
 
Sasa je... nilijua tu, watatakana...

Ona sasa jini Rosemery tayari kaangukia kwenye penzi la binadamu...


Cc: mahondaw
 
Duu! Wapo faster... mara hii washafanya matusi na kutambishana kwa wazazi...


Cc: mahondaw
 

Duu!

Huyu jini mwanamke anapenda ngono... keshapigwa mkuyenge tena...


Cc: mahondaw
 

Kumbe masaa yote haya Deo alikua anaota kuhusu jini Rosemary...

Sasa hizo sehemu za malavidavi, hakujichafua kweli, kwa sababu mechi za kwenye ndoto zinakuaga siyo mchezo...

Cc: mahondaw
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…