The king makers

Habibu B. Anga

JF-Expert Member
May 7, 2013
6,557
25,716
Sasa, unaweza kupata nakala za Kitabu changu cha "NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI NA UJASUSI".
kitabu kina kurasa 442 na ndani yake kuna makala 17.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 50,000/-

Pia waweza kupata kitabu changu cha "OPARESHENI ZA KIJASUSI ZILIZOFANIKIWA ZAIDI"
Kitabu hiki kina kurasa 214 na ndani yake nimechambua Oparesheni 6 tofauti.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 15,000/-

Wasiliana nami kwa namba 0759 181 457

Au bofya link hapa chini kunitumia ujumbe moja kwa moja whatsApp

THE KING MAKERS
SEHEMU YA KWANZA


Kampuni ya Samsung inakadiriwa kuchangia 17% ya GDP ya nchi ya Korea ya Kusini, na pia inachangia 20% ya mauzo yote ya nje (exports) za nchi ya Korea Kusini.

Wanaijeria kumi matajiri zaidi wakiongozwa na Aliko Dangote wanakadiriwa kuchangia takribani 12.5% ya pato la Taifa la Nigeria, ambapo Dangote pekee na makampuni yake anakadiriwa kuchangia zaidi ya 7.4% ya GDP ya Nigeria.

Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group) inakadiriwa kuchangia karibia 3.5% ya pato la Taifa la Tanzania.

Je, umewahi kujiuliza watu wa dizaini hii (Samsung, Dangote, Mo Dewji n.k.) wanaushawishi kiasi gani katika kuamua nani aongoze nchi na namna gani nchi iongozwe.??


SEOUL, KOREA YA KUSINI
Mwaka huu kunatarajiwa kuanza kwa kesi kubwa inayotabiriwa kuwa itateka ulimwengu na hata kupewa hadhi ya Kesi Ya Karne (Trial Of The Century).

Kesi hii itamuhusisha moja ya watu muhimu zaidi nchini humo, mtu ambaye anaelezwa kuwa na nguvu zaidi na ushawishi hata kumshinda Rais wa nchi hiyo na jarida la Forbes linamuorodhesha kama yuko nafasi ya 35 katika orodha ya watu wenye ushawishi zaidi duniani.. Kesi hii itamuhusu Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Samsung, Bw. Jay Y. Lee ambaye ni mtoto wa Lee Kun-hee mwenyekiti na mmiliki wa Makampuni ya Samsung.

Kesi hii inakuja wakati ambapo Jay Y. Lee anaandaliwa kurithishwa Uenyekiti wa Samsung kutokana na afya ya baba yake kuzorota tangu mwaka 2014 alipopata mshtuko wa moyo.

Kwa sasa inakadiriwa na wachambuzi wengi wa masuala ya uchumi kwamba thamani ya Samsung imefanikiwa kuipita thamani ya mpinzani wake mkubwa kampuni ya Apple kutoka nchini Marekani. Hata 'market share' ya kampuni ya Samsung inakadiriwa kuwa ni kubwa kuishinda ile ya Apple.

Kesi hii inatishia kutokea kwa anguko kubwa la kampuni ya Samsung kutoka kwenye "utukufu" wake na hata kuleta mtikisiko kwenye uchumi wa Korea ya Kusini.

Hakuna jambo jipya sana alilolifanya Lee mpaka kupelekea kushtakiwa kitu ambacho kilikuwa kinaonekana kuwa hakiwezekani, kwani familia ya Lee ni moja ya familia ambazo ni "untouchable" ndani ya Korea ya Kusini.
Lakini ubaya alioufanya katika suala la safari hii ni kutishia maslahi ya kibiashara ya kampuni za Marekani zilizowekeza ndani ya Samsung.

Kesi hii na skandali hii inaelekea kuwa skandali ya kusisimua zaidi kuwahi kutokea mashariki mwa Asia na itachukua miaka mingi sana kutokea tena skandali yenye kumuhusu moja ya watu 'wazito' zaidi duniani.

SS2.jpg

Jay Y. Lee CEO wa Samsung Electronics na Makamu Mwenyekiti wa Samsung |Group akiwa amekamatwa wiki mbili zilizopita

Kiini cha kesi yake kinahusishwa na uhusika wake kwenye skendali iliyopelekea Bunge la Korea Kusini kumuondoa madarakani Rais wa Korea mwanamama Park Geun-hye, mwaka Jana mwezi Desemba tarehe 9.

Uamuzi huo wa Bunge umethibitishwa Jana tarehe 10 March, 2017 na mahakama Kuu ya Korea Kusini, na hivyo kumuondoa rasmi madarakani mama Park Geun-hye.

Skandali hii inathibitisha tuhuma za siku nyingi zinazoelekezwa kwa kampuni ya Samsung kuifanya nchi ya Korea ya Kusini kama mali yao binafsi, kwa kuiweka serikali nzima mikononi mwao na kuhakikisha hakuibuki makampuni mengine yatakayoweza kushindana nao kibiashara.

Sasa ili nchi ya Korea kujisafisha taswira yake katika kwenye ulimwengu wamekubali kum-sacrifice rais wa nchi.. Sasa je, wataenda mbali zaidi na kui-sacrifice kampuni ya Samsung na Viongozi wao??

Na je nini hasa kimetokea mpaka kusababisha mkwamo huu na mtikisiko katika nchi ya Korea na Asia Mashariki kwa ujumla??

Hii mada ni moja ya mada zilizo complex zaidi na yahitaji kutuliza kichwa hasa kuielewa kwa undani wake, na kuona uhuondo wake na labda na sisi kujifunza kitu.. Kwa hiyo nitajitahidi kuenda hatua kwa hatua.. Taratibu.!!

Now, let's start from the begging..

Mwaka 2014 baada ya Mwenyekiti wa Samsung Bw. Lee Geun-hye kupata mshtuko wa moyo na afya yake kuanza kuzorota, yakaanza maandalizi ndani ya Samsung ili kuweza kumrithisha Uenyekiti mtoto wake mkubwa wa Kiume Jay Y. Lee (au Lew Jae-yong kwa kikorea).

Kipindi hiki Jay Lee alikuwa ni Chief Operating Officer wa Samsung Electronics, na kabla ya hapo alikiuwa ni Vice President wa Idara ya Strategic Planning ndani ya Samsung tangu mwaka 1991.

Hivyo basi ili kutengeneza mazingira mazuri ya kumrithisha Uenyekiti, kwanza akapewa nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa Samsung.
Hatua ya pili ndio ilianzisha utata wote mpaka kupelekea kuondolewa kwa rais wa nchi madarakani na hatimaye juzi kukamatwa kwa Jay Y. Lee mwenyewe.
Hatua hii ilihusisha kuunganisha ya kampuni mbili, yaani Kuunganisha kampuni ya Samsung C&T na kuunganisha na kampuni ya Cheil Industries, kampuni zote hizi zinamilikiwa na Samsung.

Ili kufanikisha hii 'merger' ndipo ambapo Jay Y. Lee na Samsung wakaanza kumtumia Rais Park kuwasaidia kutumia mamlaka yake kama rais kuhakikisha muunganiko huu wa kampuni hizi mbili unatokea.

Hapa ndipo giza lilipoanza kutanda na 'bundi' kutia kwenye kampuni ya Samsung na nchi ya Korea.!!

Kwanza kabisa, swali la kujiuliza… iweje wamiliki wa kampuni watafute msaada wa Rais ili kusaidia kuunganisha kampuni zao wenyewe??

Ili kujibu swali hili na kuelewa chanzo cha skandali hii ili tuweze kwenda vizuri, inatupasa kwenda kwenye shina kabisa la mfumo complex wa kibiashara wa makampuni makubwa ya nchini Korea.

Chaebol
Nchini Korea Kusini kuna mfumo wa uenselshaji makamupi makubwa ambao wenyewe wanauita Chaebol. Kwa tafsiri rahisi ya Chaebol tunaweza kuifananisha na "Conglomerate" kwa kingereza.

Yaani inakiwa ni mkusanyiko wa makampuni mengi ambayo yanakuwa chini ya umiliki wa kamupini moja, tofauti tu na nchi nyingine ni kwamba Chaebol inakuwa chini ya umiliki wa familia ambayo ndiyo inakuwa inatoa Mwenyekiti wa Makampuni hayo.

Mfano wa Chaebol kutoka Korea Kusini, ni kampuni kama Samsung, Hyundai, LG, Doosan na GS Group.

Sasa licha ya kusema kwamba kampuni hizi "Chaebol" zinakuwa zinamilikiwa na familia, ajabu ni kwamba unaweza kukuta familia hiyo labda inamiliki hata 1% pekee ya hisa za Kampuni lakini kunakiwa na mfumo 'very complex' unaowawezesha familia hii kuwa na 'absolute power' ya kuendesha kampuni na kurithishana.

Mfano kwenye Chaebol ya Samsung, Familia ya Lee wanamiliki hisa chini ya 4% ya Samsung yote, lakini wao ndio "wamiliki" wa Samsung, na wanarithishana kampuni na uongozi wa juu kuanzia Babu mtu, Baba na sasa hivi anataka kurithishwa mtoto Jay Y. Lee.

Sasa, kabla sinaeleza ni namna gani familia ya Lee imeifanya Korea Kusini kama mali yao binafsi, na namna gani ikaja kuzuka skendali iliyopelekea kuondolewa madarakani Rais Park na kupelekea CEO wa Samsung Jay Y. Lee kukamatwa juzi, ni vyema kueleqa kwanza ni namna gani mfumo wa umiliki wa Samsung ulivyo complex na unavyowafanya Lee Family kuwa na 'absolute power' ya kampuni.

Wengi wetu tukisikia Samsung tunaelewa kwamba ni kampuni ya Utengeneza simu, TV, na vitu vingine vya elektroniki.
Lakini uhalisia ni kwamba, Samsung Electronics ni kikampuni kimoja ndani ya kampuni 78 zilizo chini ya Samsung Group.

Mfano ndani ya Samsung group kuna Chiel Industries (kampuni ya utengenezaji nguo), Samsung C&T (kampuni ya ujenzi na Trading), Samsung Life (kampuni ya Bima), Samsung Heavy Industries (kampuni ya kutengeneza meli), Samsung Electronics (Kampuni ya kutengeneza simu n.k), Samsung Securities (kampuni ya biashara za hisa), Samsung Card, Samsung Fire & Marine na kadhalika na kadhalika.. Kama nilivyosema jumla ziko kampuni 78.

Sasa kampuni hizo kwa pamoja ndio zinaunda Samsung Group.
Umiliki wa kampuni hizi ni moja ya mifumo tata zaidi na complex katika nyanja ya biashara.

Kuelewa kwa undani juu ya namna makampuni ya Samsung yanavyomilikiwa inahitaji labda kuandika makala nzima na zaidi.. Lakini hapa nitajitahidi kueleza japo kwa muhtasari ili kuweka msingi imara wa mjadala tunavyoendelea huko mbele..

Kwa hiyo nitajaribu kuonyesha ni namna gani Lee Family wananufaika na mfumo huu complex ili kuendelea kuwa na absolute power ya kuimiliki na kuiongoza Samsung.

Cheil Industries ndio 'holding company' katika Samsung group.
Familia ya Lee inamiliki 31% ya hisa zaChiel Industries.

Sasa tuchukue kwa mfano Samsung Electronics, moja ya 'lulu' za Samsung group (inachangia 70% ya mapato ya Samsung Group). Cheil wanamiliki 4% ya Samsung Electronics. Pia Samsung Life wanamiliki 7% ya Samsung Electronics. Wakati huo huo Samsung Fire & Marine wanamiliki 1.3 ya Samsung Electronics.

Hii inawapa Lee Family jumla ya 12-13% ya umiliki wa Samsung Electronics.
Ukijumlisha na 3.44% ya umiliki wao wa moja kwa moja wa Samsung Electronics unawapa jumla ya umiliki wa 18% ya Samsung Electronics.

Kwa kuzingatia kwamba Samsung Electronics wana "Hisa hazina" (Treasury shares) ambazo hizi kawaida hazina haki ya kupiga kura kwenye maamuzi ya kampuni, kwahiyi hii inazifanya 18% ya umiliki wa Samsung Electronics wa Lee family kuwapa 22% ya kura kwenye maamuzi ya kampuni (22% voting shares).

Mtindo huu huh pia unatumika kumiliki makampumi mingine ndani ya Samsung Group.

Tuchukue mfano wa 'lulu' nyingine ndani ya Samsung Group, kampuni ya bima ya Samsung Life. Lee Family yenyewe inamiliki 20% ya Samsung Life. Wakati huo huo Cheil Industries (ambayo inamilikiwa 31% na Lee Family) wanamiliki 19% ya Samsung Life.

Ukijumlisha na hisa zinazomilikiwa na Samsung cultural Institute, jumla unapata 47% ya umiliki wa Samsung Life uko kwa Lee Family.

Au tukichukua mfano mwingine, Samsung Fire & Marine, Lee Family wenyewe hawamiliki hata 1% ya hisa wao kama wao lakini Cheil Industries (ambayo 31% inamilikiwa na Lee Family) wanamiliki 15% ya Samsung Fire & Marine.

Sasa turudi kwenye mfano wa Samsung Electronics ambayo ndio lulu ya Samsung Group. Tuseme kwamba maamuzi yanataka kufanyika kuhusu jambo Fulani na kura inabidi ipigwe.
Lee family wenyewe tayari wana 22% ya 'voting shares' kama nilivyoeleza.

Papo hapo pia kuna Mamlaka ya Huduma za Mafao (NPS - National Pension Services) wanamiliki 8% ya Samsung Electronics. Sasa NPS ni Idara ya serikali ambao ni vibaraka wa Lee Family, kwa hiyo kwenye maamuzi yoyote lazima wawe upande wa Lee Family.

Hii inafanya Lee family kuwa na 30% ya voting shares na 70% inayobakia inakuwa kwa mamia ya wanahisa wengine.
Kwa hiyo ni wazi kuwa Lee family ndio pekee wenye Sauti kubwa ya pamoja kwenye maamuzi yoyote yale.

Mfumo huu tata ndio umekuwa ukitumiwa na Lee Family kuiendesha Samsung Group tangu enzi za babu yao Lee Byung-chul, na sasa baba Lee Kun-hee na mtoto anayetaka kurithishwa Lee Jae-yong (Jay Y. Lee).
Mfumo huu umekuwa ukifanywa uwe complex zaidi kila mwaka na Lee Family.

Ndipo hapa tunafika mwaka 2014 ambapo Baba mtu Lee Kun-hee akapata mshtuko wa moyo na ikaanza kuwekwa mipango ya kumrithisha Jay Y. Lee.
Ndipo hapa ambapo ukapensekezwa mpaka wa kuunganisha (merger) kampuni ya Cheil Industries na Samsung C&T ili kuweza kumpa Jay Y.

Lee ushawishi zaidi katika kampuni ya Samsung Electronics ambayo kampuni ya Samsung C&T wanamiliki hisa nyingi tofauti na Cheil Industries ambayo ina hisa kiduchu (ambayo Lee family wanamiliki kwa 31%).

Hapa ndio vita ilikoanzia.
Suala hili lilipingwa vikali na Bilionea wa kimarekani Paul Singer ambaye kampuni yake ga Elliot's Associates inamiliki 7% ya Samsung Electronics.
Ikabidi Rais wa Korea Kusini, mama Park Geun-hye apigiwe simu.

=======

SEHEMU YA PILI


Katika sehemu ya kwanza ya makala hii nilieleza ni namna gani ambavyo familia ya Lee wanatumia mfumo tata wa “Chaebol” kudhibiti umiliki wa himaya ya makampuni ya Samsung.

Mwaka 2014 Mwenyekiti wa makampuni ya Samsung Bw. Lee Kuha-hee alipata mshtuko wa moyo.
Afya ya Bw. Lee Kuan-hee imekuwa ya mgogoro tangu mwaka 1999 alipofanyiwa oparesheni ya mfumo wa ya mfumo wa upumuaji.
Kwa kipindi Kirefu miaka yote hii ilikiwa inampasa Bw. Lee aende kukaa nje ya nchi kwa kila kipindi cha baridi kinapofika nchini Korea.

Shambulio la moyo la mwaka 2014 lilikuwa kubwa zaidi na hatarishi zaidi lililosabisha alazwe kwa miezi kadhaa kwenye kituo maalumu cha afya cha Samsung, Samsung Medical Center.

Hali hii ilipunguza kwa kiwango kikubwa uwezo wake wa ufanisi katika majukumu yake ya kila siku kuiongoza Samsung kama mwenyekiti.

Ndipo hapa ambapo ukaonekana ulazima wa kuanza kumuandaa mtoto wake Jay Y. Lee ili aweze kuchukua mikoba ya baba yake kama mwenyekiti.

Sasa, kwa kuwa Jay Y. Lee alikuwa bado ni kijana wa miaka 45 pekee, ukaonekana ulazima wa kumuongezea nguvu katika kampuni za Samsung Group kwa kumpa ushawishi zaidi katika kampuni lulu ya Samsung Electronics (flagship company) ambayo mpaka sasa ndiyo kampuni inayochangia 70% ya mapato ya Samsung Group.

Hivyo basi ukaonekana ulazima wa kuipa nguvu na ushawishi zaidi familia ya Lee ndani ya Samsung Group, na mchezo mzima ukapangwa kama ifuatavyo;

(Katika vipengele ambavyo hutanielewa tafadhali rejea sehemu ya kwanza ili ujikumbishe maelezo niliyoyatoa kuhusu ‘mzunguko’ wa umiliki wa Lee family kwenye makampuni ya Samsung).

Tuendelee..

‘Mchezo’ ulikuwa umepangwa ufanyike kama ifuatavyo..

Jay Y. Lee yeye menyewe binafsi ana hisa 1.4% tu ya Samsung Electronics.
Lakini kampuni ya Samsung C&T wana hisa karibia 3.3%.
Wakati huo huo kampuni ya Cheil Industries wana hisa zisizozidi 1% katika kampuni ya Samsung Electronics. (Kwa mwaka huo 2014).

Sasa tukumbuke kuwa katika kampuni zote 78 zilizo chini ya mwamvuli wa Samsung Group, kampuni ya Cheil Industries ndio kampuni ambayo Familia ya Lee wana kiwango kikubwa zaidi cha hisa na ndiyo wanayoiyumia kama ‘holding company’!
Lakini kampuni hii kwa kipindi hicho ilikiwa na disadvantage moja, walikuwa na hisa chache ndani ya Samsung Electronics kama nilivyoeleza hapo juu.. Hii maana yake kwamba ilikuwa inafinya ushawishi wa familia ya Lee kwa Samsung Electronics.

Lakini wakati huo huo kuna kampuni nyingine Dada ya Samsung C&T ambayo Lee Family hawana hisa nyingi, lakini wana advantage ya kuwa na hisa nyingi ndani ya Samsung Electronics.

Ndipo hapa ambapo ukatangazwa mpango wa wa kuziunganisha (merger) kampuni za Samsung C&T na Cheil Industries.

Uamuzi huu ulikuwa na faida kwa kiasi Fulani lakini pia ulikuwa na hasara kubwa.



FAIDA

Kama deal hii ingefanikiwa basi ilitegemewa kuleta faida kubwa kwa wana hisa wa Chiel Industries hasa hasa Lee Family.
Hii ni kwasababu, Mosi; kwa kipindi hiki hisa za Kampuni ya Cheil zilikuwa na thamani ya chini ukilinganisha na hisa za kampuni ya Samsung C&T.
Pili; wana hisa wa Cheil Industries pia walitegemewa kunufaika na umiliki wa 3.3% wa hisa za kampuni ya Samsung C&T kwa Samsung Electronics.
HASARA

Hasara kubwa ilikuwa inaenda kwa wana hisa wa Samsung C&T kwa sababu hisa zao zenye thamani kubwa kwenye kampuni yao na hisa zao kwenye kampuni ya Samsung Electronics, zilikuwa zinaenda kumilikiwa kwa pamoja kati yao na Wana hisa wa Cheil Industries.
Nitoe mfano rahisi ili kuakisi hiki ninachokijadili ili tuelewe kwa ufasaha zaidi.

Tuchukulie kwa mfano kuna baba mwenye watoto wawili, James na Michael.

James anafanya biashara ya kuuza magari, na amefanikiwa kuwa na Yard yake ya magari ambayo ina magari ya kila aina.

Papl hapo, Michael anafanya biashara ya kuuza baiskeli, na ana duka lake la kuuza baisikeli.

Unaweza kuona kwamba James ana biashara yenye thamani kubwa kuliko Michael.

Sasa itokee siku moja, baba yao awaambie kuwa wanapaswa kuunganisha biashara zao.

Unaweza kuona kwamba muunganiko huu wa kibiashara utakuwa na faida kwa Michael anayeuza baisikeli kwani sasa pia atakuwa anamiliki biashara ya magari, lakini kwa upande wa pili muunganikl huu utakuwa na hasara kubwa kwa James ambaye kwa sasa biashara yake ya magari inakuwa sio yake peke yake, pia anakuwa anaimiliki na Michael.

Hivi ndivyo ilivyokuwa katika merger ya Samsung C&T na Cheil Industries.
Muunganiko huu ulikuwa na hasara kwa wanahisa wa Samsung C&T lakini ulikiwa na faida kwa wana hisa wa Cheil Industries hasa hasa Lee Family.

Sasa,

Kama nilivyoeleza kwenye sehemu ya kwanza ya makala hii, moja wapo ya wanahisa wakubwa wa Samsung C&T alikuwa ni Bilionea wa Kimarekanj Paul Elliot Singer, mmiliki wa kampuni ya uwekezaji ya Elliott’s Associates, huyu alikuwa na hisa 7.1%.

Kitokana na hii merger ya Cheil na SS C&T kuwa na hasara kwa wana hisa wa SS C&T, Paul Singer akaanzisha kampeni kali ya kupinga azma hii ya kutaka kuziunganisha kampuni hizi.
Pia akapinga vikali utaratibu wa Lee Family kujilimbikizia nguvu na ushawishi ndani ya Samsung Group pasipo kuzingatia hasara wanayopata wana hisa wengine.

Familia ya Lee nayo ikaanzisha kampeni kali ya kumchafua Paul Singer kwenye vyombo vya habari vya Korea wakidai kuwa alikuwa ni mnyonyaji wa magharibi aliyejipenyeza ili kuja kuvuruga desturi za biashara za Korea.

Kwa hiyo kukawa na mchuano huo mkali.

Upande mmoja ukiwa ni wanahisa wa SS C&T wakiongozwa na Paul Singer wakipinga kuunganishwa kampuni hizi na upande mwingine Lee Family wakitumia vyombo vya habari kushawishi wanahisa wakubali kupitisha mpango huo.

Ikapangwa tarehe ya mkutano wa wana hisa wote ili kupiga kura kukataa au kukubali kuunganishwa kwa kampuni hizo.

Tarehe hii ilikuwa ni July 10, 2015 na watu wengi walitegemea wanahisa kukataa kampuni hizi kuunganishwa.
Ili mpango huu wa hii merger iweze kupita ilikuwa inahitajika kukubaliwa kwa si chini ya kura 66.7%.
Baada ya kikao kirefu kilichokuwa na mabishano makali, mwishoni zilipokuja kupigwa kura na matokeo kutangazwa ilionyesha kuwa 69.5% ya wana hisa walikubali kampuni hizo ziungane.

Lilikuwa ni jambo la kushangaza sana, lakini kura ndio zilikuwa zimeshapigwa.. Na Lee family hawakutaka kupoteza muda, wakaziunganisha kampuni hizi mbili na kuwa moja (Samsung C&T ikamezwa ndani ya Cheil Industries, kwa hiyo kwa sasa kuna Cheil Industries pekee yake).

Lakini mwaka Jana, ndipo wafukunyuzi wa mambo wakabaini kuwa Rais Park Geun-hye alihusika kwa kiwango kikubwa kuisaidia familia ya Lee kufanikisha mpango huu wa kuunganisha kampuni hizi.. Kitendo hiki ndicho kilichochangia kuibuliwa kwa skendali iliyosabibishwa mwanamama huyu kuondolewa na bunge kwenye kiti cha Urais..

==========

SEHEMU YA TATU
Katika sehemu ya pili ya mfululizo wa makala hizi, nilionyesha namna ambavyo iliibuka sintofahamu kati ya Samsung Group na wana hisa wake kutokana na mpango wa kuziunganisha (merger) kampuni za Samsung C&T na Cheil Industries.
Katika sintofahamu hiyo, wanahisa wa Samsung C&T walikuwa hawakubaliani na kuunganishwa kampuni yao na kampuni ya Cheil Industries, lakini mpango huo ulikuwa unashinikizwa na Lee family kwa kuwa ulikuwa unawapa nguvu zaidi ya kudhibiti umiliki wa kampuni ya Samsung.

Mwishoni nikaeleza kwamba ulipoitishwa mkutano wa wanahisa.. Majibu yakarudi kwamba mpango huo umepita kwa kura 69.5% kitu ambacho kiliwashangaza wengi.


Niliahidi kueleza uhusika wa Rais Park Guen-hye katika kufanikisha mchakato wa kuunganisha kampuni hivi na kuipa nguvu na ushawishi zaidi Lee Family ndani ya kampuni ya Samsung.

SKANDALI YA CHOI SOON-SIL
Rais Park Geun-hye ni mtoto wa Rais wa zamani wa Korea aliyeitwa Park Chung-hee aliyetawala miaka ya 1970s.

Katika kipindi hiki lilitokea tukio la mauaji ya kupangwa (assassination) ya Mke wa Rais (mama yake Rais Park).

Katika kipin hiki ndipo ambapo Park alifahamiana na mwanamama aliyeitwa Choi Soon-sil.
Huyu alikuwa ni mtoto wa muhudumu wa kiroho (shamakh) aliyeitwa Choi Tae-min ambaye alikuwa kiongozi wa huduma ya kiroho ya Yongsae-gyo (Church of Eterne Life) na mara moja akaanza kuwa na ushawishi mkubwa kwa Park na hatimaye kuwa ‘mentor’ wake.

Kwa hiyo urafiki kati ya Park na binti wa mentor wake (Choi Soon-sil) ukakua kutoka kipindi hicho mpaka alipokuja kuwa Rais mwaka 2013.

Mara tu baada ya Park kuukwaa Urais, huyu rafiki yake Choi Soon-sil ambaye kama nilivyoeleza kuwa alikuwa ni binti wa mentor wake, akaanza kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya serikali ya rais Park japokuwa hakuwa na cheo chochote rasmi.
Yeye ndiye alikuwa na ushauri wa mwisho kwa Rais Park. Yeye ndiye alikuwa mwenye sauti na amri kwa rais park kuhusu masuala yote ya kisera.
Choi Soon-sil akatumia ushawishi wake huo kufanya mambo mengine ya kipuuzi kabisa..

Kwafano alikuwa na binti yake aliyeitwa Chung Yoo-ora ambaye alipomaliza elimu ya sekondari hakuwa na alama zenye kutosheleza kupata udahili wa kujiunga na Chuo Kikuu, alichokifanya Choi Soon-sil akaamuru chuo kikuu cha Ewha Women University kishushe chini sifa zao za udahili ili binti yake aweze kupata admission.

Choi hakuishia hapo tu, kwa kushirikiana na Rais Park, wakaanzisha mashirika ya misaada (Foundations) matatu kwa ajili ya kujipatia fedha kutoka kwa matajiri wa Kikorea.
Mashirika hayo yalikuwa ni, Bu-il Foundation ambalo lilihusika na elimu, pia kulikuwa na Mir Foundation ambayo ilihusika na masuala ya utamaduni, pamoja na K-Sports Foundation ambayo ilihusika na michezo.

Turejee kwenye ‘merger’ ya Samsung..
Baada ya kutoka sintofahamu kati ya wanahisa wa Samsung C&T na Familia ya Lee, ndipo hapa rafiki wa Rais Park, mwanama Choi Soon-sil akafanya mawasiliano na familia ya Lee na kuwa eleza kuwa rais ana uwezo wa kuwasaidia kwenye hilo.
Wakafanya makubaliano ya siri ni namna gani Rais atasaidia na familia ya Lee wakaweka ahadi yao ni namna gani “watamshukuru” rais akisaidia kufanikisha hilo.

Niwafahamishe kwamba katika kipindi hiki 11% ya hisa za kampuni ya Samsung C&T zinamilikiwa na shirika la serikali la mafao NPS (National Pensions Services). Asilimia hizo za hisa zinawapa NPS 27% ya kura za maamuzi (voting shares).
Kwa hiyo alichokifanya Rais Park ni kumuamuru waziri wa Afya ambaye ndiye wizara yake ndio inasimamia shirika hilo, kumuagiza Mkurugenzi wa NPS ahakikishe kuwa siku ya mkutano wa upigaji kura Tarehe 10 July, ahakikishe anapiga kura kuunga mkono kampuni hiyo kuunganishwa na Cheil Industries.

Kwahiyo asilimia hizi za kura za NPS, ukiunganisha na kura zinazotokana na hisa za familia ya Lee wenyewe zikaleta kama 55% ya kura na ukijumlisha na kura za marafiki zao wachache wenye hisa Samsung C&T ndipo zikaleta 69.5% ya kura za NDIYO kukubali kampuni kuunganishwa.

Kwa hiyo hivi ndivyo ambavyo mpango huu ulifanikishwa na kuhakikisha Familia ya Lee inaendelea kufanya ushawishi wake ndani ya Samsung Group unakuwa thabiti zaidi lakini wakati huo huo wanahisa wao wakapata hasara kubwa.

Licha ya mpango huu kufanikiwa mwaka juzi 2015, wafukunyuzi wa mambo wakaendelea kudadisi ni nini kilimfanya rais Park kuingilia kati kuwasaidia Familia ya Lee kuunganisha kampuni za Samsung C&T na Cheil Industries..

Baada ya ufukunyuku na upekuzi wa muda mrefu, ikaja kubainika kwamba.. Familia ya Lee ilimuhonga Rais Park kiasi cha fedha za kikorea Won Bilioni 77.4 (zaidi ya dola milioni 60 za Marekani) kupitia mashirika yake ya Mir Foundation na K-Sports Foundation.
Baada ya taarifa hizi kuwekwa hadharani, ndizo zikawa chanzo cha kuibuka kwa kashfa maarufu ya “The Choi Soon-sil Scandal” ambayo ilikuja kuwa chanzo cha maandamano ya wananchi nchi nzima kupinga utawala wa Rais Park Guen-hye.

Baada ya maandamano kupamba moto na umaarufu wa Rais Park kudorora kwa wananchi, hatimaye Tarehe 9 December 2016, bunge likapiga kura ya kumuondoa madarakani Rais Park.

Juzi Tarehe 10 March, Mahakama ya katiba ikahalalisha uamuzi huo wa bunge na kumuondoa rasmi madarakani rais Park Guen-hye na nafasi yake kukaimiwa na Waziri Mkuu wake.

Pia wiki iliyopita waendesha mashitaka wa Korea walifungua mashtaka dhidi ya Jay Y. Lee mtoto mkubwa wa kiume wa Mwenyekiti wa Samsung ambaye kwa sasa ni CEO wa Samsung Electronics na Makamu mwenyekiti wa Samsung Group na siku chache zijazo anatarajiwa kupokea mikoba ya baba yale na kuwa mwenyekiti wa Samsung.
Waendesha mashitaka wa Korea walifanikiwa kupata kibali cha kumkamata Jay Y. Lee, na wamemkamata na kumfungulia mashitaka ya rushwa na kwa sasa kesi iko inaendelea mahakamani na ina ‘joto’ la hali ya juu.

Kesi hii imekuwa ni ya kwanza na ya aina yake kufunguliwa dhidi ya mwanafamilia kutoka familia za “Chaebols”, na hii inaakisi kuchoshwa kwa wananchi dhidi ya kiburi na utamaduni wa familia hizi kuiweka nchi ya Korea kiganjani mwao na kufanya kama watakavyo..
Hakuna anayejua.. Labda huko mbeleni, mfumo huu wa Chaebols unaweza kupigwa marufuku kabisa nchini Korea.

Leo nimehitimisha, awamu ya kwanza wa mfululizo wa makala hizi.. Lakini kama nilivyoahidi mwanzoni mwa makala kwamba.. Nitaangazia kila pembe ya dunia kuchambua namna wafanya biashara wanavyoshawishi mifumo ya uongozi wa nchi na ufanyaji maamuzi ya serikali.
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden
bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart
 
Saluti kwako mkuu.. Juzi kati nilikua maeneo yangu ya kujidai hapa kitaani. Kama kawaida nikishakula utirio huku nawaweka chini natoa lecture. Basi mzee mmoja akanifuata nimfahamishe chuo nilichosoma ili ampeleke mwanawe maana najua vitu vingi. nikamwambia ni THE BOLD UNIVERSITY Uganda.
plz usiache kuni tag.
 
Mkuu The Bold umeona wanafunzi wako tupo wengi
Saluti kwako mkuu.. Juzi kati nilikua maeneo yangu ya kujidai hapa kitaani. Kama kawaida nikishakula utirio huku nawaweka chini natoa lecture. Basi mzee mmoja akanifuata nimfahamishe chuo nilichosoma ili ampeleke mwanawe maana najua vitu vingi. nikamwambia ni THE BOLD UNIVERSITY Uganda.
plz usiache kuni tag.
 
Saluti kwako mkuu.. Juzi kati nilikua maeneo yangu ya kujidai hapa kitaani. Kama kawaida nikishakula utirio huku nawaweka chini natoa lecture. Basi mzee mmoja akanifuata nimfahamishe chuo nilichosoma ili ampeleke mwanawe maana najua vitu vingi. nikamwambia ni THE BOLD UNIVERSITY Uganda.
plz usiache kuni tag.
Hahahahahaha!! Daaaahh.. Shukrani sana Mkuu, am humbled
 
Back
Top Bottom