'The Hidden Tanzania', Part Two ya Royal Tour

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
Rais Samia Suluhu Suluhu amesema sehemu ya pili ya filamu ya “The Royal Tour” inatarajiwa kutoka hivi karibuni lakini itakuja kivingine ikilenga kuonyesha maeneo ya utalii yaliyojificha yaliyopo Tanzania.

Filamu hiyo ambayo ni mwendelezo ya kwanza itapewa jina la “The Hidden Tanzania”.

Rais Samia aliyekuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Sabasaba mkoani Njombe, leo Agosti 10, 2022 amesema awamu ya pili ya filamu hiyo itaonyesha vivutio ambavyo havikuonyeshwa kwenye awamu ya kwanza.

“Waandaaji wameipa jina la “The Hidden Tanzania” yaani maeneo mengine ya Tanzania yaliyojificha, ni kwenda kuyachukua na kuyaonyesha kwamba Tanzania mbali ya tuliyowaonyesha bado kuna mambo haya,” amesema Rais Samia.

Kumekuwa na malamiko kwamba filamu ya “The Royal Tour” imesahau vivutio vilivyopo mikoa ya nyanda za juu kusini, ikiwemo mikoa ya Njombe, Mbeya, Songwe, Iringa na Songea.

Wakazi wa Njombe wamemuomba Rais Samia Hifadhi ya Taifa ya Kitulo kuiingizwa kwenye mradi wa kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW).

Akjibu hoja hiyo, Rais Samia amesema awamu ya pili ya filamu ya “The Royal Tour” itahusisha hifadhi hiyo kwa hiyo wasiwe na wasiwasi.

“Mikoa hii ya nyanda za juu kusini itaingia kwenye awamu ya pili ya “The Hidden Tanzania” tuonyeshe vivutio vyetu na watalii waje wengi zaidi,” amesema Rais Samia.
 
Back
Top Bottom