The FALL oF UDSM?

Kwikwikwi, hapo niko puzzled mkuu. Mtoto wa high school au first year hapa viwanja anaweza kuacha masomo na kuanzisha Microsoft, napter au facebook. Na mtu anaondoka na first class bongo anashindwa kutengeneza spoku ya biskeli.

Hapo sasa.....na ukifikiri sana mwishowe utarudi kulekule kwenye kauli mbiu yangu ingawa najua kwa wengi ni vigumu kukubali
 
Hilo ni kutokana na msukumo wa siasa uliopo. Ukiisha, hadhi ya UDSM itaendelea. UDSM ina historia ndefu na ningependa kila mmoja wetu apitie pale.
 
Companero:

Marekani kuna public schools: State Universities na Community colleges. Vilevile kuna private universities. Mtu anayesoma community colleges anaruhusiwa kuhamisha credits zake na kujiunga na university. Kwa Tanzania mtu amechukua diploma ya engineering ya miaka mitatu kutoka katika chuo cha ufundi lakini hawezi kuhamisha credits zake za masomo. Na matokeo ni kurudia masomo.

Hujajibu swali, ngoja nilirahisishe: Je, hizo State University hazipewi mshiko wa kufa mtu na Serikali zao/yao? Je, sasa haziweweseki pia kwa kuwa mtafaruku wa Uchumu dunianiani unasababisha hilo fungu lipungue? Je, vyuo vya Umma Tanzania venyewe havistahili ruzuku hiyo pia?

PS. Kama suala ni competition tayari kuna vyuo binafsi vya kumwaga Tz ambavyo vinastahili kuleta hiyo competition dhidi ya vyuo vya umma!
 
Hapo sasa.....na ukifikiri sana mwishowe utarudi kulekule kwenye kauli mbiu yangu ingawa najua kwa wengi ni vigumu kukubali

Mvumbuzi wa Mpemba Effect hawezi kutengeneza spoku ya baiskeli kama anavyodai Zakumi? Halafu first class wangapi anawajua kuwa hawawezi? Kaulimbiu yako inabidi irekebishwe na kusomeka hivi: MIAFRIKA NDIVYO ILIVYO INAPOKUBALI KUWA KAMA ILIVYO MAHALI ILIPO!
 
vyuo vyetu ubabaishaji..hata UD ni chuo changu nimesoma lakini walimu hawafanyi research! Wanataka waitwe maprofesa bila kufanya utafiti..sasa huko UDOM ndo itakuwa balaa zaidi...

Tatizo kubwa wengi tunadhani University ni majengo na magari ya kifahari. University ni RESEARCH! na kama UD iki-invest katika research haina haja ya kushindana na mtu..matunda yanaonekana. UDOM ni kelele tuu za siasa..hawana lolote....hebu tuwekane sawa hapa....tuache kushabikia maneno..we need hivi vyuo vifanye utafiti. I repeat..publication records za walimu UD zimeshuka sana tena sana! Hivi UD wana Journals ngapi ambazo ziko internationally cited?? I doubt kama kuna publication za vitabu kama vitano kila mwaka pale UD....I am not sure...

Hivi kweli Kama ile taasisi ya Mkandara ya REDET ndo ilitoa ule utafiti wa juzi..kwamba JK atashinda kwa 71%...jamani mnadhani kweli wana credibility tena? I for one I used to respect Mkandara, but I am sorry to say, I no longer take him serious... Naona ni politician tuu mwenye njaa zake...

Huwezi kuniambia eti chuo hakina pesa wakati VC na maofisa wakubwa mnaendesha magari ya kifahari...why not use the money to buy books? Ok..hamuwezi tembea kwa mguu..basi nunueni magari cheap! Bongo siasa tuu.. hata hao wasomi unaowaona..ni waganga nja tuu..wanachumia matumbo yao... ...

JK...make use of them to get what you want and dump them! wamesoma lakini hawatumii akili zao..

Jana kuna jamaa mmoja ali graduate UD aliniambia kuwa katika kozi yao ya miaka minne, vitabu ambavyo walimu waliwashauri wasome katika ngazi mbalimbali vilikuwa ni zaidi ya arobaini. Ila mpaka anamaliza alisema vitabu visivyozidi vinne. Hakuwa kuingia library kluazima kitabu chochote maana nyenzo pekee ilikuwa madesa.
Wanafunzi wa aina hii baadae kwa kutumia GPA zao za madesa ndio wanakuwa walimu. Tutegemee nini? Kama wakisogea mpaka wakawa maraisi au wabunge au makatib wakuu tutegemee nini?
Guys elimu yetu yote ina kasoro kubwa tusijidanganye kuwa mambo yako sawasawa. Vinginevyo tuendelee kujenga majengo mengi na kutengeneza wataalamu ambao sio wabunifu na wasio na msaada wowote kwa Taifa hili.
Mfano wa madudu ya kisomi tunayofanya ni Research center inayoitwa REDET> Duuu! Kama vile hawajasoma
 
Source Prof Mkandara

Leo Mkandara ameudhihirisha umma kuwa sasa UDSM wanatembeza bakuri cake wanayopewa haitoshi kutoka serikalini, mpaka sasa cake wanakula UDOM. hii imesababisha mgogoro mkubwa katika colledge tofauti tofauti(coet etc). Akiongea katika TBC1 leo Prof mkandara amesema UDSM walikuwa wanapokea cake kubwa lakini kwa sasa inaenda UDOM

1.kwanini serikali imekitupa udsm?
2. kwanin serkali haijali raslimali watu?
3 Miaka 50 chuo kinaenda nyuma sio mbeli

penye ukweli nakosoa serikali yangu

Poleni sana
 
Chuo kimeshindwa kutoa product tulizotegemea miaka 50 no improvement tunatoa watu ambao hawana msaada kwa taifa zaidi ya kulinyonya taifa wameshindwaje kujisimamia miaka 50 kwa nin serikali isifikirie kuwekeza sehem ambayo inafikiri itakuwa productive kuliko kuendelea kumlisha ng'ombe ambaye hatoi maziwa tunayo yataka? wanafanya research ambazo hazina effect katika jamii yetu wanaweka makabatini tu.mtoto miaka miaka 50 hatembei.saiz ana mdogo wake ndio anayestahili msaada zaidi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom