The English of President Magufuli of Tanzania

Sijui ana vicheo gani sasa anataka kuleta upumbavu wa vyeo vyake humu Jamii Forum ,kama asipo jihami kwa matusi anakimbilia kupiga watu mikwara wanaume humu ,
ajue hapa watu wanashindana kwa hoja sio matusi wala vyeo
 
Zile earphones zinazowekwa UN na kwenye mikutano mingine ya kimataifa unajua kazi zake!?
 
Aliyekudanganya hivyo ni nani? Nasaka PhD yangu hapa na sijaambiwa kuwa lazima nijifunze lugha ya pili. Na kwa kuenzi Kiswahili, nimepata dili la kuwapiga kozi ya msasa ya Kiswahili madenti wanaokuja huko nyumbani kufanya tafiti zao.
 
Mkuu ni ukweli ndio huo hakuna dhambi kutoweza kuongea kiingereza vizuri. mvutano uliopo ni kuukataa ukweli kwamba raisi wetu haongei kiingereza kizuri. Tukubali na tusiumizwe na hilo kwani tunachotaka watz kwa sasa sio kiingereza bali ni mtu atakayewe kututoa kwenye umaskini huu tulionao ambao hutukupaswa kuwa nao.
 
Umeshawahi kwenda nje ya Tanzania? Because if you had ungetambua kuwa kujiumauma lugha ya kigeni sio big deal. Tatizo baadhi yenu mnaongelea hisia badala ya hali halisi. Sijawahi kuchekwa na Mwingereza kwa 'kumung'unya lugha yao," and by the way, Waingereza wanachukua tahadhari kubwa wanapoongea na foreigners (kwa sababu 'Kiingereza cha maongezi baina ya Waingereza' sio hicho unachoona magazetini. Ushawahi kumwelewa Rooney au Sir Alex Ferguson?
 
ajue hapa watu wanashindana kwa hoja sio matusi wala vyeo
Hicho ndio ajui yaani mtu kama huyu ndio angepewa komandi ya Anga basi tungekoma kila siku MiG-21MFs tulizopewa na Mrusi mwaka 1974 zingekua zinarushwa bila sababu tu kwa kupenda sifa
 
Mkuu mimi nilibahatika kufanya kazi na wachina. Taifa ambalo lilikuwa masikini na kuibuka kusiko julikana. Wale viumbe hawajui ata what is your name. Mawasiliano ni kwa google translate kwisha
 
Lugha itasaidia nini katika maisha yako ...
Mwanasaikolojia mmoja alisema ni rahisi sana kuperform kwa kutumia lugha yako ya kuzaliwa kuliko lugha aliyojifunza
 
AFRICA INATAKIWA IJIKOMBOE KIFIKRA. TUNATAKIWA TUPAMBANE ANGALAU LUGHA MOJA YA BARA LETU ITAMBULIKE KIMATAIFA... NASIKITIKA KWAMBA TUNAJIPAMBANUA KWA LUGHA ZA WAKOLONI WETU>>>aibu
 
 
Aliyekudanganya hivyo ni nani? Nasaka PhD yangu hapa na sijaambiwa kuwa lazima nijifunze lugha ya pili. Na kwa kuenzi Kiswahili, nimepata dili la kuwapiga kozi ya msasa ya Kiswahili madenti wanaokuja huko nyumbani kufanya tafiti zao.
Sawa,ikiwa huoni umuhimu wa kujua kiingereza basi endelea chief.
 
Watu wengi inaonekana hawaelewi ukweli kuwa Kiingereza ni lugha rasmi ya Tanzania, kwa jiyo siyo lugha ya kigeni tena. Tatizo ni pale inapoonekana tuna matatizo ya kuimudu lugha yetu rasmi!

Pamoja na kwamba kiingereza hakiweza kumwathiri Rais wetu kiutendaji lakini kuijua vizuri lugha huongeza uhuru wa kujieleza na hivyo huchangia ufanisi.

Ni nadra binadamu kuvipata vyote, na kwa Rais wetu, huu ni upungufu wake.
 
Kha ! Hao wakosoaji wa kikatoliki cha presidaa nao kikatoliki chao za ugoko tupu!
 
AFRICA INATAKIWA IJIKOMBOE KIFIKRA. TUNATAKIWA TUPAMBANE ANGALAU LUGHA MOJA YA BARA LETU ITAMBULIKE KIMATAIFA... NASIKITIKA KWAMBA TUNAJIPAMBANUA KWA LUGHA ZA WAKOLONI WETU>>>aibu
Kuna upotishaji mkubwa sana na kutaka kuwaaminisha watu kuwa Mwafrika akiongea kiingereza ana kasumba. Huu ni umbumbu wa hali ya juu. Maana mataifa mengi sana Duniani zaidi ya Waingereza, wanaongea kiingereza. Je hao wote wana kasumba.

Hata Kiswahili ni mchanganyiko wa kibantu, kiarabu na kihindi. Basi na chenyewe tukiache maana ni kasumba, tuongee tu kisukuma, kizaramo, kingoni, kibena, n.k.

Hata kiingereza ni mchanganyiko au ni zao la lugha za Kigiriki na Kilatini. Kwa hiyo kiingereza ni lugha ya wengi maana imekopa maneno mengi toka lugha za watu wengine.
Tuukubali ukweli kuwa Mtanzania yeyote kutoijua lugha yake rasmi, na tena lugha ya kufundishia masomo, ni kati ya negatives.

Mchina, Mjerumani, Mjapani, Mbrazil, Mrusi, asipojua kiingereza siyo ajabu maana siyo lugha yake rasmi. Tanzania kiingereza ni lugha rasmi.

Kuukubali upungufu wa kutoimudu lugha ya kiingereza kwa Rais wetu siyo udhaifu, na wala hakumwondolei uwezo wake wa kutuongoza.
 
Hacha kushadadia ukoloni wewe....kwani Obama anajua Kiswahili....
Kuna watu wanatia hadi huruma...
Kwa hiyo kingereza kitakuwekea msosi mezani???!!!!
Kweli watu wanadhani kujua lugha ya kingereza ndio ujuvi wa mambo.Hivi nchi zinazo zungumza kingereza kama malawi, zambia etc wametuzidi nini?
 
Zile earphones zinazowekwa UN na kwenye mikutano mingine ya kimataifa unajua kazi zake!?
Ndiyo ninajua na inaonekana wewe una taarifa nusu. Ebu jaribu kugoogle lugha zinazotumika UN halafu utajua kwa nini wanvaa hizo earphone. Tafasiri inayotolewa huko haihusishi Kiswahili. Unajua ni kwa nini pamoja na AU kukubali kiswahili kama lugha rasmi mpaka sasa haitumiki
 
....ifike mahali ukweli usemwe....maana hata JPM falsafa yake ni kuusema ukweli na kuacha unafiki.....Ni kweli JPM kiingereza kinampiga chenga kwa kiwango kikubwa....na mleta mada ana hoja hapa....na kwa kweli ni vema JPM atumie kiswahili popote atakapokuwa anahutubia...hata nje ya nchi..anaweza kumtumia hata mkalimani ataeleweka zaidi...na si aibu kwani marais wengine wanafanya hivyo....na itakuwa njia mojawapo ya kukitangaza kiswahili akifanya hivi...lakini akilazimisha kuongea kiingereza kwa kweli ni aibu...na haitazuia kejeli dhidi yake toka nje.....mleta mada ana hoja ya msingi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…