Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 883
Utumwa wa kifikra. Unaweza kuwasiliana na mtu yeyote kwa lugha yako ya asili na kumpatia tafsiri. Ni uzuzu tu uliotutawala kudhani kuongea Kiingereza ndio maendeleo. By the way, Kiswahili ni lugha ya kimataifaHivi mkuu ni nani aliyekuambia Rais wa china hajui kuzungumza kiingereza? Marais wote wa China yaani aliyepita na huyu wa saaa wanazungumza kiingereza kizuri tu ingawa sio native speakers.
Katika dunia ya sasa yenye kuhusisha meetings mbalimbali na international projects NI MUHIMU SANA KUJUA KIINGEREZA ikiwa ni international language na inayozungumzwa na viongozi wa nchi mbalimbali.
Wewe unataka Wakenya waendelee kufanya advert za rasilimali zetu huko nje kuwa ni zao? Jaribu kurefer back kwenye awamu ya tatu Zakhia Meghji alivyokuwa waziri wa Mali asili na Utalii ndio utajua kutokujua kiingereza kilivyotuponza.
Au unataka tuwe tunaletewa mikataba iliyoandikwa kwa very formal english tushindwe kuitathmini na kuichanganua?
Hao investors wanaokuja kuwekeza huku wanazungumza kiswahili?
Wafanyabiashara wa kitanzania wakifanya biashara na customers wa Egland,Ireland,USA,Canada,Jamaika n.k wanatumia kiswahili?
RAIS WETU AHAKIKISHE ANAZUNGUMZA KIINGEREZA FLUENTLY KWASABABU HATADEAL NA SISI WASWAHILI TU.