The English of President Magufuli of Tanzania

Sijui ana vicheo gani sasa anataka kuleta upumbavu wa vyeo vyake humu Jamii Forum ,kama asipo jihami kwa matusi anakimbilia kupiga watu mikwara wanaume humu ,
ajue hapa watu wanashindana kwa hoja sio matusi wala vyeo
 
Ingawa wanaomponda rais kwa kuongea kiingereza kibovu nao wakitumia kiingereza kibovu vile vile, sitaki kukuunga mkono kwamifano yako. Karibu wote ukiowataja lugha zao zinatumika kimataifa ikiwemo huko UN. Lugha ni mhimu sana katika mahusiano ya kimataifa, ndiyo maana tutake tusitake inabidi tu tuzijue hizo lugha za kimataifa au kama Nyerere alivyokiita kiingereza, "kiswahili cha kimataifa".
Zile earphones zinazowekwa UN na kwenye mikutano mingine ya kimataifa unajua kazi zake!?
 
Kiswahili ni lugha ya kimataifa ndio na nakithamini sana ila Coverage yake haifikii hata robo ya English na je watu tunaodeal nao zaidi internationally katika almost all sphere of life ni watu wanaotumia lugha zipi?

Rais kujua lugha zaidi ya moja na hasa kiingereza ni added advantage.
Aliyekudanganya hivyo ni nani? Nasaka PhD yangu hapa na sijaambiwa kuwa lazima nijifunze lugha ya pili. Na kwa kuenzi Kiswahili, nimepata dili la kuwapiga kozi ya msasa ya Kiswahili madenti wanaokuja huko nyumbani kufanya tafiti zao.
 
MKUU HUO UKWELI HUJAUSEMA NI UPI MAANA HAPA KUNAPANDE MBILI ZINAVUTANA MIMI NAAMINI KUTOKUJUA KIINGEREZA SIO DHAMBI NA WALA HAKUZUII MAENDELEO YA NCHI,WENGINE HAPA WANAAMINI ILI RAIS ALETE AU AONGOZE KULETA MAENDELEO LAZIMA AJUE KIINGEREZA SASA HAPO HAPO HATUJUI UMESIMAMA UPANDE GANI.
Mkuu ni ukweli ndio huo hakuna dhambi kutoweza kuongea kiingereza vizuri. mvutano uliopo ni kuukataa ukweli kwamba raisi wetu haongei kiingereza kizuri. Tukubali na tusiumizwe na hilo kwani tunachotaka watz kwa sasa sio kiingereza bali ni mtu atakayewe kututoa kwenye umaskini huu tulionao ambao hutukupaswa kuwa nao.
 
Nad
wewe ndiye utakuwa mpumbavu na mjinga! Nikuoneshe upumbavu wako kidogo: kiingereza sio lugha rasmi ya serikali ya china na wala haitumiki km lugha rasmi ya kufundishia km hapa kwetu. Hivyo wachina hawalazimiki kuijua. Hapa kwetu kiingereza ni lugha rasmi ya mawasiliano kiserikali na pia ni lugha rasmi ya kufundishia. Hivyo tunategemea viongozi wa serikali waimudu kiasi cha kuridhisha. By the way mleta mada kashauri anolewe vizuri kwenye lugha ili asituaibishe kimataifa. Kiingeteza na kiswahili ni lugha zetu, lazima tuzijue zote. Na lszima ujue kwamba kiingerezs leo sio cha waingereza tena bali lugha ya dunia. Ndio maana hata Kagame francophone, anazungumza kiingereza fssaha!
Umeshawahi kwenda nje ya Tanzania? Because if you had ungetambua kuwa kujiumauma lugha ya kigeni sio big deal. Tatizo baadhi yenu mnaongelea hisia badala ya hali halisi. Sijawahi kuchekwa na Mwingereza kwa 'kumung'unya lugha yao," and by the way, Waingereza wanachukua tahadhari kubwa wanapoongea na foreigners (kwa sababu 'Kiingereza cha maongezi baina ya Waingereza' sio hicho unachoona magazetini. Ushawahi kumwelewa Rooney au Sir Alex Ferguson?
 
ajue hapa watu wanashindana kwa hoja sio matusi wala vyeo
Hicho ndio ajui yaani mtu kama huyu ndio angepewa komandi ya Anga basi tungekoma kila siku MiG-21MFs tulizopewa na Mrusi mwaka 1974 zingekua zinarushwa bila sababu tu kwa kupenda sifa
 
Kwa nchi maskini kama yetu, hatuna teknolojia ya kwetu na tunategemea misaada lazima tukope lugha ya wenzetu ili tuweze kueleweka la sivyo tutajitenga wenyewe...kisa tunaogopa kiingereza ambacho hata wachina wanalazimika kujifunza ili kuuza bidhaa na huduma zao. Rais ashuriwe apate mtaalam wa lugha aboreshe fluency yake katika english ili aweze kuwasiliana vizuri na wadau wa maendeleo na wabia katika biashara...hapo acheni bla bla na ushabiki usiokuwa na maana.
Mkuu mimi nilibahatika kufanya kazi na wachina. Taifa ambalo lilikuwa masikini na kuibuka kusiko julikana. Wale viumbe hawajui ata what is your name. Mawasiliano ni kwa google translate kwisha
 
Lugha itasaidia nini katika maisha yako ...
Mwanasaikolojia mmoja alisema ni rahisi sana kuperform kwa kutumia lugha yako ya kuzaliwa kuliko lugha aliyojifunza
 
AFRICA INATAKIWA IJIKOMBOE KIFIKRA. TUNATAKIWA TUPAMBANE ANGALAU LUGHA MOJA YA BARA LETU ITAMBULIKE KIMATAIFA... NASIKITIKA KWAMBA TUNAJIPAMBANUA KWA LUGHA ZA WAKOLONI WETU>>>aibu
 
I managed to carefully listen to President Magufuli addressing the EAC head of States. His english is neither good nor bad but it can be better.

President Magufuli speaks SwahiEnglish, a language nowhere to find. As a matter of fact, President Magufuli needs a 6 month extra english lessons to catch up with his counterparts in the region.

I understand why he didn't attend the Davos Conference in Switzerland, the fear is enorm if you can't express or hold bilateral sessions with your colleagues in a language that yourself you don't manage.

I also understand why he invited all ambassadors to the state house yet he didn't appear. He ended hiding himself underneath of the state house tables elsewhere in the house.

His level of english communications is too low. This is another major blow for Tanzanians after Kikwete finding himself in the same situation in his presidency.
 
Aliyekudanganya hivyo ni nani? Nasaka PhD yangu hapa na sijaambiwa kuwa lazima nijifunze lugha ya pili. Na kwa kuenzi Kiswahili, nimepata dili la kuwapiga kozi ya msasa ya Kiswahili madenti wanaokuja huko nyumbani kufanya tafiti zao.
Sawa,ikiwa huoni umuhimu wa kujua kiingereza basi endelea chief.
 
Ukweli ni kwamba sie Watanzania tuna kasumba ya kupenda visivyo vyetu kuliko vilivyo vyetu.

Miaka kadhaa huko nyuma, mwalimu mmoja asili yake Wales aliniambia hivi: "ukiongea Kiingereza huku una lafidhi ya kigeni maana yake ni kwamba una lugha yako ya asili zaidi ya Kiingereza, na hiyo ni plus kwa sababu sie Waingereza hatuna muda wa kujifunza lugha za kigeni." Tangu wakati huo nikaachana na jitihada za kusaka lafidhi ya 'Kiingereza cha BBC."

Ni watu wenye matatizo ya akili wanaoweza kusumbuka kumkosoa kiongozi wa taifa lao kwa kuongea lugha ya kigeni kwa mapungufu kidogo. Sio lugha yetu anyway...
Watu wengi inaonekana hawaelewi ukweli kuwa Kiingereza ni lugha rasmi ya Tanzania, kwa jiyo siyo lugha ya kigeni tena. Tatizo ni pale inapoonekana tuna matatizo ya kuimudu lugha yetu rasmi!

Pamoja na kwamba kiingereza hakiweza kumwathiri Rais wetu kiutendaji lakini kuijua vizuri lugha huongeza uhuru wa kujieleza na hivyo huchangia ufanisi.

Ni nadra binadamu kuvipata vyote, na kwa Rais wetu, huu ni upungufu wake.
 
Kha ! Hao wakosoaji wa kikatoliki cha presidaa nao kikatoliki chao za ugoko tupu!
 
AFRICA INATAKIWA IJIKOMBOE KIFIKRA. TUNATAKIWA TUPAMBANE ANGALAU LUGHA MOJA YA BARA LETU ITAMBULIKE KIMATAIFA... NASIKITIKA KWAMBA TUNAJIPAMBANUA KWA LUGHA ZA WAKOLONI WETU>>>aibu
Kuna upotishaji mkubwa sana na kutaka kuwaaminisha watu kuwa Mwafrika akiongea kiingereza ana kasumba. Huu ni umbumbu wa hali ya juu. Maana mataifa mengi sana Duniani zaidi ya Waingereza, wanaongea kiingereza. Je hao wote wana kasumba.

Hata Kiswahili ni mchanganyiko wa kibantu, kiarabu na kihindi. Basi na chenyewe tukiache maana ni kasumba, tuongee tu kisukuma, kizaramo, kingoni, kibena, n.k.

Hata kiingereza ni mchanganyiko au ni zao la lugha za Kigiriki na Kilatini. Kwa hiyo kiingereza ni lugha ya wengi maana imekopa maneno mengi toka lugha za watu wengine.
Tuukubali ukweli kuwa Mtanzania yeyote kutoijua lugha yake rasmi, na tena lugha ya kufundishia masomo, ni kati ya negatives.

Mchina, Mjerumani, Mjapani, Mbrazil, Mrusi, asipojua kiingereza siyo ajabu maana siyo lugha yake rasmi. Tanzania kiingereza ni lugha rasmi.

Kuukubali upungufu wa kutoimudu lugha ya kiingereza kwa Rais wetu siyo udhaifu, na wala hakumwondolei uwezo wake wa kutuongoza.
 
Hacha kushadadia ukoloni wewe....kwani Obama anajua Kiswahili....
Kuna watu wanatia hadi huruma...
Kwa hiyo kingereza kitakuwekea msosi mezani???!!!!
Kweli watu wanadhani kujua lugha ya kingereza ndio ujuvi wa mambo.Hivi nchi zinazo zungumza kingereza kama malawi, zambia etc wametuzidi nini?
 
Zile earphones zinazowekwa UN na kwenye mikutano mingine ya kimataifa unajua kazi zake!?
Ndiyo ninajua na inaonekana wewe una taarifa nusu. Ebu jaribu kugoogle lugha zinazotumika UN halafu utajua kwa nini wanvaa hizo earphone. Tafasiri inayotolewa huko haihusishi Kiswahili. Unajua ni kwa nini pamoja na AU kukubali kiswahili kama lugha rasmi mpaka sasa haitumiki
 
....ifike mahali ukweli usemwe....maana hata JPM falsafa yake ni kuusema ukweli na kuacha unafiki.....Ni kweli JPM kiingereza kinampiga chenga kwa kiwango kikubwa....na mleta mada ana hoja hapa....na kwa kweli ni vema JPM atumie kiswahili popote atakapokuwa anahutubia...hata nje ya nchi..anaweza kumtumia hata mkalimani ataeleweka zaidi...na si aibu kwani marais wengine wanafanya hivyo....na itakuwa njia mojawapo ya kukitangaza kiswahili akifanya hivi...lakini akilazimisha kuongea kiingereza kwa kweli ni aibu...na haitazuia kejeli dhidi yake toka nje.....mleta mada ana hoja ya msingi...
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom