THE DIASPORA! Life is a gamble; win some, lose some

THE DIASPORA! Life is a gamble; win some, lose some

Hello Europe, Hello European Sex!

Basi wakaenda Paris, babu io bahili wala nini, anamnunulia chochote atachotaka. Kampeleka mpaka designer shops, most expensive French designers, kama Dior, Channel, Christian Louboutin kiukweli alirudi na vitu vya kweli balaaaa. Ukisema hio pochi nzuri utasikia Euro 800, Hio ni Dior 2012 collection hizo sijui CL collection gani. Most of the items kwa kabati yake ati ni Designer! Na mzungu alivo mshenzi alikuwa ana order encripted version, inakuwa na initial zao wote. ZE. Na wale mnaohisi ni feki haiwezi kuwa feki sababu huwezi ku encript fake shit hata iwe fake of the first grade.

Jewerly ndo balaaa. Alimnunulia tuhereni tu ma euro mangapi sijuiiii. Mikufu ndo usiseme. Mgahawa gani Paris hakuingia. Hii migahawa ya kwenye movies hiii, karibia yoteee aliingia na alivomshenzi na picha kapiga kibaooo. Sema nyingi babu yupo. Alikuwa akipiga peke yake babu ananunaaa. Kuanzia Le Meurice, La Cordonnerie, Reed Restaurant, Le Cinq mpaka unachoka kusikiliza. Ila anakwambia wafaransa wabaguzi hatarii. Kuna siku alitangulia yeye kwenye mgahawa, hakuhudumiwa mpaka mzungu alipokuja ndo wahudumu kuanza kujichetua, na tip alioacha mzungu aliibeba. Alikuwa anawakomoa, yeye black lakini ndo kavaa Dior, chini CL za hatari, wenyewe wazungu afu mbwa kachokaaa. Wanamuuliza are you American? Anakomaa nope, im African.

Kukaa na mzungu ndo kujua kuwa yule mzungu kumbe mkewe alifariki mda sanaa na cancer, afu ana wanae 2 mmoja wa kike, mwingine wa kiume, wote wameoa na kuolewa hukooo. Mmmoja yupo London, mwingine yupo Newyork. Mara moja moja wana anaendaga kuwatembelea, ila wajukuu zake ndo wana mskype mara kwa mara. Na zamani alikuwa cyclist champion wa tournament kibao, ana makombe yake ya kutoshaaaa. So ni retired cycling pro, alivokuwa bado kwenye game alikuwa na sponsors kibao za kampuni mbali mbali, akiwa brand embassador wao. Na yeye ni mdutch by origin, hapo Denmark kahamia tu. So kampuni nyingi za ki dutch ndo zilikuwa zina msponsor na kufanya nae kazi.

Hata alivokuwa nae walienda kwenye nchi nyingi sanaa za ulaya, unakuta hizo kampuni zina Alumni, mara sijiu veteran events hivooo. Hapo kulipiwa full board, 5 star hotels, all over Europe, what more could she have asked for? Shoping ana swap tu kadi ya babuuuu. Afu kama shetani tu, hakuwaza kama bongo kaacha maisha, na iko siku atarudi afanye chochotekitu cha maana, walaaaaaaaaaa. Walizungukaaaa, mnoo mnoo. Mara utamuona yupo Sweeden, mara Norway, mara Amsterdam, Mara Berlin, mapaka London alitia maguuu, sio mara moja mara kibao kwenye mechi za Manchester. Maana mdau ni mnaziii wa team ya Man U hakunaa mfanoooo. So kama mara 4 hivi alienda kushuhudia mechi kali za Man U liveeeeeeeeee, 2 Old Traffold, moja Stanford bridge, Na ingine Emirates Stadium. Hii ya Emirates satdium alinipa offer kila kitu maana mie mdau wa arsernal damuuuu, sema Visa nikakosaaa. Niliumwa wiki mbili, malaria kali sanaaaa kisa tu kukosa Visa ya UK, mpaka tiketi ilikuwa booked. Daaaaah! Sitokuja kusahau maishani mwangu. Alishawacheki Barca na Madrid live, viwanja vyotee, Catalonia pale Camp Nou na Santiago Bernabeu, na yeye ni mnazi vibayaa mnoo wa Team la mfalmeee, tem la matajiriiii Real Madrid.

Ssa shule ikawa imeishaaa rasmi, akatakiwa arudi bongo, yeye akajitia Daz Mama, aka overstay kule, akawa sasa akahamia kabisaaa Deer River Estate kwa babu, wakawa wanaishi pika pakua, wanangoja event za makampuni wasafiri all over europe. Kiukweli alipata sanaaa tabu huko Deer River Estates manake ni sehemu ya wazungu wale matajiri afu wabaguziiii mbayaaaaaaaaa. Akawa hata akienda kwenye Club ya hapo anakaa mwenyewe tuuuu, hamna anaemsemesha, mara wamfanyie ukatili kumnyima kutumia pool, mpaka amuite mzungu aje atukaneeee matusi ya nguoni na kutishia kukatisha membership publicly. Basi wanamruhusu kishingo upandeee, Akiingia yeye kwenye pool wazungu wote wanatoka. Sasa shoga wa mieee, akawa anawakomesha anashinda humo humo kama kibokooo. Wazungu wakachoka wakaamua kuingi nao. Akawa anaenda kila siku, mpaka vitoto vikawa vinamsemeshaaa, sasa anajua kucheza na watoto, anawasimulia story anaweza ku wakeep busy. Mar mama zao wakaanza kumpenda, manake wakifika pale wanamuachia watoto wanapiga umbeaaaa, na kujipooza. Wakawa tu wamemzoea, wakapunguza ubaguzi kidogo, wakaanza kumualika party zao.

Sex life na babu mwanzo haikuwa kivileee, coz babu mwenyewe nguvu 2 tu, kidogo tu kachokaaa hoi. Akawa anampa mambooo ya kizaramo babu akadataaa hatariiii. Ndo kisa cha kumuhamishia huko Deer River Estate, ili mambo ayape uzuriiii. Na anasema alikuwa anampa dozi nene. Anampeleka peleka mpaka mzungu analia kama mtoto mdogo. Sasa challange ikaja kwenye suala zimaaa la wazungu wadadisi, kadri unavomuongezea ubunifuuuu ndo ananogewa nakuta kubuni vyake zaidi na zaidi. Mara amletee hii midoli, hii mi didlo, oooh najua sikuridhishiii, so itabidi nikuridhishe na hizi didlo, you wil enjoy! Hahahaaaaaaaa! Akawa hataki, mzungu anambembelezaaa weweeeeeeee! Mmmmh! Mara amwambie tujaribu Tigo, anataka aonje tigo kabla nguvu hazijamuishia kabisaaaa. Hahahahaaaaaaaaaa! Akamgomea kumpa Tigo. Basi akaenda Online kuandika anataka msichana black ila awe tayari kutoa Tigo. Akampata jimama la ki nigeria, akawa anachat nalo. Jimama nene hatariii, lina tigoooo zilizojazia balaaaa. Akawa ndo ana mcheat nalo! Sasa jjimama linauzaa, chochote anachotaka mzungu twendeee. Ile midoli aliyoidengulia siku tu kastukia haipoooo! Tobaaaaaaaaa! Ndo kwenda kumpekua kwenye laptop yake, ndo kakutwa convo na hio jimama la kinigeria.

Wakagombana vibayaaa vibayaaaaaaaa. Mzungu kaomba msamaha. Akamwambia hivi unajua Africa kuna AIDS? Akastukaa what AIDS? Akamwambia google. Mungu wacha atetemekeee, chezea UKIMWI weweeeeeeeee. Akamwambia sirudii tena kucheat tusihi tu kwa kuamiiana. Bibie akamuomba ruhusa aje bongo mara moja mama yake anaumwa afu atarudi denmark. Akakubali ila akampa wiki tu. Na tiketi aliompa go and return, return yake exactly after 1 week. Pakia designer staff, kila kitu kaja bongoa. Kufika huku kamgeuzia kibao, oyaaaaaaaaaaaa, mi huko sirudi ngoooooooooooooooooooo! Mzungu kalamikaaa, kambembelezaaa, kamuombaaa, yeye ndo ikawa kashaamua kubakia bongo for good!

JE MAISHA YA BONGO ATAYAWEZA BAADA YA BATA REFU HILO LA KUFA MTU!

ITAENDELEA.
 
Shoga na umbea wangu wote sikijui hicho kibabu cha KJ!!!
Hebu tupiamo tupicha au nipe a/c ya insta nikajionee hayo maajabu ya Dunia na mie....lol
Imeendelea huku
 
Mange anapenda sifa kuliko kuangalia mustakabali wa maisha yake.
Angejichukulia kibabu na show of angefanyaje?
Shoga hebu tuyaache haya tusije kumtibua nyongo Lara (si unajua tena?) akaacha kutumalizia story maana ninavyoisubiri kwa hamu acha kabisa.
Hahahaa ngoja tuishie hapa tusimtibue kubwa la maadui
 
I cannot stand being mistreated.

Ingekuwa mimi nisingekaa hata dakika mbili kwenye hiyo pool.

Why people go where they're not wanted!!!!
 
Shoga na umbea wangu wote sikijui hicho kibabu cha KJ!!!
Hebu tupiamo tupicha au nipe a/c ya insta nikajionee hayo maajabu ya Dunia na mie....lol
Haha,katika pitapita zangu niliona masikini anachambwa kisa mange nikachungulia account yake hakuwa private nikamuona babu ake....kwani michambo ya kichwa panzi ulikua huipitii shoga?
 
Hahahahaaa nimechekaje jamani?Eti akawa anajiloweka kwenye maji (swimming) kama kiboko....lol
Haya mamito lara 1 nasubiri muendelezo.
 
Haha,katika pitapita zangu niliona masikini anachambwa kisa mange nikachungulia account yake hakuwa private nikamuona babu ake....kwani michambo ya kichwa panzi ulikua huipitii shoga?
Sijui nilikuwa napitia?Maana juzi kati hapo almanusra nistaafu umbea!
Ngoja nipekue mafaili.....
 
Hello Paris!

Akawa kanicheki skype nimpe akili. Nikamuuliza huyo babu anaishi wapi? Akamtext akamwambia anaishi Deer River Estates. Yaani kuona hio Estates nikajua tu sio mzungu boyaaa. Nikamwambia sikia, mimi huko sijawahi kufika, huenda nisifike maisha haya wala yajayo, lakini nachojua mimi, mzungu yoyote anaeishi Estate sio wa kumchezea. Hio estate sio unakuta eneo lina heka na heka . Ooooh! We kaa tu kiboyaaa. Bongo kazi huku hamnaaa, humuoni Killi na mzungu wake babuu, ana range, ana jagguar. Humuoni Bahati na mzungu wake. Nani anakuona huko bwanaaaaa. Vijana wataishia kukopa kama wa Morrocan. Hahahahaaaaaaaaa. Akasema kweli ngoja nijipostion kwa hili libabu.

Akawa anachat nalo, ana chat nalo. Kwanza kwenye profile yake kaweka hobby Travelling the world. Advertise la kwanza meeting date kamwalika ERA ORA, akahisi tuuu, hii sehemu huenda ikawa si ya kitoto. Akaamua kumuuliza yule Mfaransa. I have a dinner date, mfaransa akadakia oooh! Finally seeing someone down town? Fellow Nigger? Hahahahaaaaaaaaa! Akamwambia no, someone Denish. Ooooh! Commoner? Mfaransa ana mbwembwe huyo. Akamwambia i dont know! Akamuuliza i was wondering if you know this restaurant ERA ORA? Mfaransa akastukaaaa, akasawajika uso, akwambia no way no day, he is definately playing a prank on you. He just wants to embarrass you. No niggers in ERA ORA. Hahahaaaaa!

Akawa anamwambia but he invited me, mfaransa anagoma, he cant invite you, not possible, ERA ORA is for the rich folks. Baadae mfaransa akamuuliza give me the address of the guy. Akamtajia Deer River Estates, akamuuliza what? No way! He is really rich isnt he? Huuuuh! I get to be French, and you Nigger get to get the rich guy right under my nose, what a fu.cking life. Okay you cant go to ERA ORA being a nigger and wearing those rags of yours. Jamaniiiiiiiiiii! Kua uyaone, anavumilia tu maadamu apewe pointers. We ned to go shopping for brands. Sasa shoga bahili, akaishia kununua vitu Zara tu baasi.

Akaanza kuambiwa na mfaransa, your future came earlier than you expected so start practising the Fork and knife. Anajobolewaje na mfaransa sasa. Ahaaaaaaaaa, hushiki hivo, effortlesss. Glass ya wine hushiki hivo, vidole viwili tu. Napkin unaweka hivi. I should be the one going on a date like this not you nigger my friend. Hahahaaaaaaaaaaa! Ila akawa anaconcentrate kama caluculus. Siku ya date mfaransa ikabidi amuazime pochi yake ya Gucci. Analamika, take care of it, that is just 2011 collection, maneno kibaoooooooo. And dont look cheap, they wont open the door for you.


Akatinga ERA ORA, na pamba designer mwanzo mpaka mwishooo. Yule kaka wa mlangoni akawa anasita sita japo kamfungulia. Akamuoneshea kitu cha GUCCI, kidogo akakisoma maana nayo ni Italian Restaurant, so gucci original wakimuona wanamuelewa. Akaulizwa reservation? Akajibu yes, table flani. Akaelekezwa. Ashapewa A,B,C ukifika Koti litapokelewa, ukikaa jitandaze napkin, pochi wek wapi, hivooo. So ikawa piece of cake. Basi yule mkaka anae mpeleka anamuuliza are you American? Akamjibu NO, im African! Akamuuliza Nigerian? Akaamua tu kumwambia yes.

Kafika kamkuta babu keshafika, wakasalimiana, aka kaa. Akafanya taratibu zote za ibaada ya wazungu wakuone una class. Basi yule babu ikabidi amuuliza you said you are African and ...? Akamjibu i have class? Mzungu akacheka. Akamwamia 50yrs of Independence. Ukaja mda wa Kuoda, anatamka vizuri kabisaa si unajua tution ya mfaransa na wafaransa kwa kula ni balaaaa. Yule mzungu aka impressed. Akasema honestly when you told me you from Africa, nikajua i will have to train you from 0. Akamwambia i know some things.

Basi akawa anamuuliza about Africa, akamwambia ashaenda S.A, basi shogaa ndo kurudisha Geography ya A levelmezani. Kujitia Limpopo river, kafika lini? Ngorongoro Creater, Serengeti, Victoria Falls Zambia huko, Pyramid of Egypts, Sahara Dessert, Klahari Dessert. Anajifanya na yeye ni extensive traveller. Mzungu kawa impressed balaaa. Maana travelling ndo hobby yake kubwaaa. Mda wa kuondoka akamwambia i enjoyed your company a lot., cannaomba tukutane tena next weekend hapo NORMA Restaurant.

Mfaransa mekaa ameuliza, how did it go? Akamwambia, na kuwa next week ni Norma! Mtumeeee1 Macho yalimtoka si kidogo. Akaanza you know what will be good is for you to introduce me to this man, so he can introduce me to his friends. Iam your friend nigger. Hahahaaaaaaaaaaaa! Kimoyo moyo akamwambia we niite Nigger, ila namaliza migahawa yote ya ghali Copenhagen. Basi wakaenda Norma huko, kama kawa aliazima kile ki Gucci. Wakala dinner fresh kabisaaa, ndo yule babu akamwambia mimi next weekend naenda Paris, kuna mbio za baiskeli, naenda kushiriki, it is my hobby, you can accompany me, we can go together. MASHIKOLO MAGENI NDANI YA PARIIIIIIIIIII! Ni nomaaaa.

Akaniskype, you wont believe it, Z mimi, huyu huyu Z, ndani ya Paris! Mmmmmh! Nikamwambia shoga nenda, ponda raha kufa kwaja. Cheze ki passport kuongezewa muhuri. Basi mfaransa ndo aka rest in peace kabisaaa. Anamwambia if he takes you to New York i will have to die and come back to life. Anamtajia ukifika Paris, nenda huku na huku. Siku ya siku huyooooooooo, Paris na babu yake.

ITAENDELEA KESHO.
hapa ndo ninapowapendea wazungu yani anakupa details zote na tuition ya bila ada kiroho safiiiiii angekuwa mswahili sasa mapinduzi hayachezi mbali he he he he
 
Haha,katika pitapita zangu niliona masikini anachambwa kisa mange nikachungulia account yake hakuwa private nikamuona babu ake....kwani michambo ya kichwa panzi ulikua huipitii shoga?
Kuhesabiwa chips

Bye
 
Asante lara 1 kwa story zako wewe ni mmoja wa watu walionifanya nijiunge humu Jamii forum.jamani salama...ndugu yenu nawasalimu..
 
Hello From Bongo, Football Adiction!

Sasa karudi bongo, wabongo ni wale wale, jua ni lile lile. Akawa anafanya kazi kwa wa dutch flani, coz yule babu alimgundisha ki dutch sanaa tu. Akawa anabonga ki dutch. Sasa maisha yakawa so boring, amerudibongo kakuta watu wote wana relationship zao. Wako busy na mambo yao. Dior, Cl, Gucci dont mean shit. Sawa watu wana admire nice handbag, umeipata mwenge au karume? Hahahaaaaa! People got no respect for fashion in Tz. Sanasana siku moja tu alikutana na my sis wa Mwanza nae alikaa sanaa nje ndo akawa ana sujudu the value of fashion she was wearing. Wengine mburaaaaaaah, wamevaa nguo za buku buku siku zinaenda mazeee.

Ikawa ndo tukaenda Albasha posta pale, nikamwambia kuna Lebanese cuisine, akafurahi, sasa mi kwenye menu nikaoda chochote, honestly niliangalia cha bei ghaliii, si ofaaa, yeye akaoda sijui kitu gani akasema alikula ufaransa kilikuwa kitamu sanaaa. Mburaaaaaah! Kwani aliweza hata kula basi. Uma moja tu, hamu ikamuisha, mi naona ni tamu balaaaaaa. Namwambia kula bwana hii bongo utakufa njaaa. Akasema aliepika hajui kapika nini.

Nikamwambia twende basi Osaka sushi pale ziko mwaaah! Kidogo ndo akala kwa kumezea na maji, akasema ile sio sushi ni mfano wa sushi. The only thing alichokiwa anapenda toka moyoni ni Margarita za Samaki samaki na Princess Cassino. Na Pizza za new york Pizza. Yani nilikuwa na kibarua cha kuzinguka nae migahawa ya bongo yooote. Uzuri sio bahili analipia. Anzia Karambezii, Ducle Cafe, Napoleon, red onion mpaka chineze restaurants hizi Ming dynasty, mpaka Saverios, Hotel hizi Serenaa, sijui Double tree, Giraffe, nothing was close to Copenhagen, Paris, Berlin, Amsterdam. Ule uvumi wa bongo kama ulaya ni uongo mtupuuuuu. Bongo ni bongo na ulaya ni ulaya.

Akaamua kusahau mambo ya Ulaya na kuishi kama mmbongo. Zile designer staff kazigawa gawa, tukawa sasa bega kwa bega mr. Price na Kkoo kwenye lunyaaa. Basi ikawa kapunguza na being a snob, ile kujifanya dunia nzima kafika yeye akaacha, akawa hata hasemi kama katoka ulaya wala nini. Na nikamwambia if you keep being a snob you wont get a dick in town, we mwanaume kumsimjlia umekuwa dada yake vasco da gama unafikiri hataacha kukimbia yeye Dubai tu anaisikia kufika bado sanaaaa. Akawa hasemi, basi mda mwingine mnakutana na mtu kufika hapo Dubai maneno yanamtoka kama nini anamchora tu.

Huku na huku cause ni adict wa soka akaanza kufatilia timu za hapa Bongo, mimi mnazi wa Yanga damuuu na Mtibwa Sugar, manake kuna kipindi mzee wangu alishafanya kazi Mtibwa, so yeye siku zote ni Mtibwa Sukari, Z yeye ni Simba damuuu. Siku ikichezwa Simba na Yanga lazima tutinge uwanjani na jezi, full kushangilia. Huku na huku ndo kipindi sasa mchezaji mmoja wa Simba X, alikiwa ndo striker namba 9 mgongoni ndo ana tamba ni balaaaa. Homa ya jiji si kidogooooo. Umeonaaa. Akawa anasema huyu 9 kama namuelewaaaa, akijichanganya kwenye 18 zangu nampa kipapa bila chengaaa si kwa magoli yaleeeee. Hahahaaaaaa! Nikawa namwambia achana nae huyoooo, mashikolo mageniii, boya sanaa afu anapenda sifa za kijinga kichiziii. Na hio gari alilonunua hatunywi maji. Mshamba flani hiviii ila kwa yale mambo yetu ya marijuanaaa nasikia ni mteja ni balaaaaaa. Nikamwambia badala ushobokee vitoto mulito kama Niyonzimaaa, unahangaika na kikongwe huyoooo. Ananiambia mi basi tu nimemuelewaaaa. Hahahaaaaa.

Sasa siku hio walikuwa na road show, ikawa haibambi walaa nini, kuko Zeeeee, akaniita mwanangu njoo ufanye amsha amshaaaa, uwe Mc road show imenoki. Nikamwambia naja. Huyooooo, nikaibuka, ilikuwa Buguruni. Aaaaaah nikazimua kwanza na kitu cha arusha, nikaonaaa umati mweupeeeeeeeee. Nikamwambia Dj niwekee Hadija Kopa Top in Town kwanzaaa ndo twende sawaaa. Uswahili weka taarabu, utajazaaa hatari, na mizuka utaipata ya kutoshaaaa. Nikaamsha amsha paleeeee, na mambo yetu tena waswahiliii, taratibu mtizame anaekukanyaga ndo anakuchukulia mumeeee! Halòoooooooo! Nikapata shangweee za kutoshaaa. Basi yule Mc wao walio kuja nae aka pitch walichopanga ku pitch, tukaendesha maswalina majibu na kugawa zawadi za kutoshaaa, road show was a success.

Sasa kazi ya road show isikie tu, inachoshaaa ni balaaaa. Sasa baadae tumechoka mpaka vinenaaa, tukaanza story za game ya Mtibwa na Simba. Basi story story mimi namponda kishenziii 9. Mara steady show mmoja mkaka akasema mbona namba 9 fresh tu, tunakaa nae kitaaa, anakujaga maskani kishenziii, hata ukitaka namba yake nakutafutia. Mtu fresh vibayaaa mnooo. Mmmmmmh! Ndo bibie kuuliza sasa yuko exited. Kweli unamjuaaa? Akajibu namjua nje ndaniiii. Akamwambia nitafutie hio namba yake. Mmmmmmh! Mi niakona kabisaa tunakoelekea sikoooo. Basi akamwambia poa. Kesho akaja nambia ile namba nimeipataaa, ngoja tumchokoze tuone itakiwaje maana ma star wa kibongo nao. Akamtumia sms Mambo! Ikajibiwa Poa! Weweeeeeee! Basi akaanza mimi naitwa flani ni shabiki wako nambari mokooo, nakukubali vibaya mnoooo, bila wewe Simba hamna kitu, ile game ya juzi, yule mkabaji wa Costal union mgosi wa kaya boya tuuu. Bongeee la sms. Akajibu hiii kweli dada yangu unaujua mpiraaa, nimefurahi sanaaa kukufahamu tuwe marafiki.

Basi ukaanza huo urafiki wa simba na Swala, ikawa sasa mechi za simba tunaingia bureee, ndioooo.Isicheze simba kama adhabu lazima twende, ikicheza hata Moro lazima twende, Tanga twende ilikuwa shughuli. Siku hio wakawa wemshinda ubibgwa wanfanyiwa Party. Tukapata mualiko wa hio party nayo. Huku na huku siku hio akaambiwa njoo Kibadamo, akaenda, wakafanya yao kwa raha zao, mtu mzima haulizwi. Ila akamwambia yeye ana mke na mtoto 1.

Huku na huku siku yaanza maongezi kuna mchezaji mwinhine wa Simba ni Hb vibya mnooo, tukamsifiaaa, mtoto ana asili ya kipembaaaa. Hahahaaaaa! Kama shetani akamuingia, akaiba namba yake kwenye simu ya 9. Akaanza kumchatisha nae. Nae huyu hapaaa nyavuniiii. Dada angu unaujua mpira sanaa tuonane. Kuonana akatembea nae tenaaa. Looooh! Ikawa anawamiliki wote timu moja na hawajuani. Huyu akitoroka mazoezini leo, huyo kesho kitwaaa. Ila ikaja tu akampenda sanaa HB maybe cause ni mtu wa pwani, manake wanajme wa pwani ndo ugonjwa wake. Akamdatisha Hb vibaya mnooo.

Sasa mtaani wakaanza kunongonaaa, mbona nyie mabinti hatuwaelewiiii, maana mara tunamuona namba 9 anakija lwenu, mara yule mpembaaa, bado Kochaaa tu kuingia hapo kwenu, ndo kusema kuna kambi isoo rasmi ya simba ama? Hahahahaaaa! Uswahilini napo kwa kufatiliana. Manake Prado la flani linapaki hapo, na Gx 100 ya flani inapaki hapo. Na juzi yule kijana wa kipemba kaja na Kasejaa, kuna nini? Mbona hatuwasomi. Hahhaaaaa! Yatawashinda.

Ikawa wakija wanapaki barabarani. Na mpemba nae kaoa atiiii ana watoto 2. Ila 9 ndo alikuwa anamwagia mihelaaa. Aaaaaah! Mpemba free P, tu hata hivo hakuwa na mkataba mnono kama namba 9. Ndo nilipojua wacheza mpira hamna kituuuuu. Paka ni paka akiona samaki lazima alie nyauuuu hata awe maaarufu vipi.

Huku na huku akaniambia mi maisha yamenichoshaaaa. Nataka nifanye makaratekaaa nirudi njeeee, hapa bongo design kama pamenishindaaa, nasikia wizarani kuna sponsor ship za china nime apply! Zikitiki naibukia uchinaniiii. Akawa anaendelea nao wote kama kawaidaa. Baadae namba 9, akawa hana msimu mzuriii, nafikiri na hela ikakata akawa hayupo nae tenaaa. Akabakia kijana wa kipembaaa peke yake.

Majibu yakaja kapata chuo Beijing, anatakiwa akareport. Basi akamuga mpemba, huyoooo akawea pipa ,paka Beijing mojaaaa.
ITAENDELEA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom