The Article of Union between the Republic of Tanganyika and the Peoples Republic of Zanzibar

Huyu Mwanakijiji mtoto wa Nyerere kapotelea wapi kwenye hii thread? nataka sababu kwa nini wazanzibar wakiridhia kujiondoa hawataweza!

sasa kuitana majina ndio kunafanya hoja ziwe na nguvu? Wazanzibari hawawezi kuvunja muungano bila kusababisha vita.. nyinyi mnafanya mchezo. Kuna nchi moja inaitwa Tanzania na uhaini au kujaribu kuivunja ni kosa kubwa zaidi dhidi ya jamhuri hiyo. Najua watu mnachukulia kiutani utani tu. Muungano wa Tanzania ni halali kisheria, kihistoria na kimantiki. Na ni kweli wanaoleta fyoko fyoko watatiwa ndani na hautavunjika ati kwa sababu watu wanakasirishwa na mambo fulani. Hakuna muungano mkamilifu duniani na ni jukumu la wananchi na taasisi mbalimbali za nchi hiyo mara zote kufanya kazi ya kuujenga na kuuboresha. NInachosikia watu wanacholalamikia siyo muungano hasa bali ni mambo mbalimbali ambayo tunayita "kero". Sasa badala ya kuwashughulikia viongozi wabovu wasio na maono ya kutatua muungano au kukiondoa madarakani chama ambacho hakina uwezo wa kuboresha muungano watu wanataka kukimbia.

Tuna katabia kauoga kakuogopa kushughulikia matatizo kwa sababu "they are too hard" au hatutaki kuwakwaza. Hili ndilo lililosababisha hata hoja ya Utanganyika kwani badala ya kushughulikia waliovunja katiba kwa kuingiza Zanzibar OIC wao wakataka kuanzisha Tanganyika. Na ndivyo ilivyo sasa, matatizo ya muungano ni yapi - watu wanasema "siupendi"! Asilimia labda 80 wa Watanzania wote hawajawahi kuwa raia wa Zanzibar au Tanganyika!!

Watanzania tuna matatizo sana.. hatutaki kushughulikia mambo magumu tunafikiri kujenga muungano ni kuunganisha michanga tu halatu tunaenda kulala kusubiri ujijenge. Angalia Waingereza wanavyohangaika na muungano wao, angalia Wacanada na suala la Quebec, angalia hata RSA, angalia Mexico, Marekani ndio usiseme kabisa, wao ndugu zao wa KUsini waliamua kabisa kujitenga na kutangaza rais wao! guess what.. they went to war to protect the union!! SAsa sisi Watanzania tukiwaambia tutakwenda vitani kulinda muungano waoga wanaanza "not worthy it!".. ndio aina ya viongozi tulionao!
 
Nani anayehalalisha nchi Mwanakakiji? sema unachosema, kwangu mimi ilikuwa taifa kama watu walikubali Nyerere awe rais wao awaongoze then that is a country, hakuna chombo chcochote cha kuhalalisha uhalali wa nchi.

kama hiyo ndiyo dhana ya uhalali wa taifa kwanini Tanzania siyo halali basi? Maana watu walikubali Nyerere kuwa Rais maana "hakuna chombo chochote cha kuhalalisha uhalali wa nchi"?
 
Wakoloni walipewa nchi zetu kwa kuwaandikisha mikataba machifu wetu na sisi tulikuja kudai kuwa ukoloni mikataba njiyo ni batili. Usilopenda kufanyiwa usimfanyie mwenzio.

Unataka kusema Karume hakuwa na akili timamu wakati anaongoza mapinduzi na wakati anasaini makubaliano ya Muungano?
 
Nilivyosikia kwenye maelezo mkataba ule ulisainiwa kwanza kabla ya kupelekwa bungeni kwa kupitishwa. Na Zanzibar waliulizwa suali masiku baada ya kusainiwa "Jee munaupenda hamuupendi Muungano?????" Na kwa hali ile ilibidi kujibu "Ndiooooooooo"

Na kwenye kitabu cha Jumbe "The partnership" yeye kama Waziri ya Nchi aliulizwa siku moja kabla ya kutangazwa Muungano (April 25): kesho tutaungana Tanganyika na Zanzibar jee umewafiki? Na Jumbe akajibu "Ni vyema"
 
Kisheria kama hakukuwa na ratification kwa Sheria iliyopitishwa na Bunge au BLM, basi kuna 'ratification by acquiscence', ndio maana Articles of Union zimeendelea kufanya kazi tangu 1964 hadi leo!
 
Tumekuwa tukisikia mara kwa mara watu wakiuliza juu ya "uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar" uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini hatujasikia watu wakiuliza juu ya uhalali wa "Taifa" la Zanzibar ambalo lilitokana na Uhuru wa mwaka 1963 toka kwa Mkoloni wa Kiingereza na baadaye Mapinduzi ya Mwaka 1964 yaliyoongozwa na Field Marshal John OKELO toka Uganda au hata uhalali wa lililokuwa Taifa la Tanganyika lililozaliwa baada ya kupatiwa Uhuru toka kwa Wakoloni wa Kiingereza mwaka 1961. Au tuseme yote yaliyotengenezwa na mkoloni ni "halali" na tuliyoyatengeneza sisi wenyewe ni haramu? Nini uhalali wa "taifa" la Zanzibar? Tujadili!
 
Muungano upo kihalali lakini una matatizo ya msingi period!, Matatizo ya msingi ili kutatuliwa kunahitaji re-vamp of the whole system yaani kuuvunja au kupiga kura upya ...wananchi wa pande zote za muungano period!
 
Na kwanini Nyerere alichanganya udongo ule pekeyake? Kwanini Karume hakushiriki katika katika uchanganyaji wa udongo?
 
Kwa mtizamo wangu wa haraka haraka nafikiri mpaka watu wafikie kuhoji uhalali wa muungano ni pale wanapoona, tanganyika kama nchi huru ikipoteza uhalali wake kama taifa lenye dola yake kwa kujiunga na taifa lililokuwa zanziba. Sasa tatizo ni ubabaishaji uliopo katika muungano huu upande mmoja kuwa na serikali yake na raisi wake na bunge lake huku upande mwingine ukikosa haki hizo. Huo ndio utata hata kufikia kuhoji uhalali wa huu muungano. Natarajia wachambuzi wa kisiasa na historia ya nchi yetu watakuja na ufafanuzi yakinifu kwa hili.
 
Walikubaliana Mwalimu awe ndiyo mwadhimishi mkuu wa "ibada" ya kuchanganya udongo wa Muungano. Haina maana kwamba Karume hakuwa anashiriki kikamilifu. La maana ni presence yake na utashi wake kwamba udongo ule uchanganywe kuashiria muungano wa nchi hizo mbili. It was just a sign or symbol.
 
Muungano upo kihalali lakini una matatizo ya msingi period!, Matatizo ya msingi ili kutatuliwa kunahitaji re-vamp of the whole system yaani kuuvunja au kupiga kura upya ...wananchi wa pande zote za muungano period!

Kama upo kihalali, uvunjwe ili iweje?
 
Kwa mtizamo wangu wa haraka haraka nafikiri mpaka watu wafikie kuhoji uhalali wa muungano ni pale wanapoona, tanganyika kama nchi huru ikipoteza uhalali wake kama taifa lenye dola yake kwa kujiunga na taifa lililokuwa zanziba. Sasa tatizo ni ubabaishaji uliopo katika muungano huu upande mmoja kuwa na serikali yake na raisi wake na bunge lake huku upande mwingine ukikosa haki hizo. Huo ndio utata hata kufikia kuhoji uhalali wa huu muungano. Natarajia wachambuzi wa kisiasa na historia ya nchi yetu watakuja na ufafanuzi yakinifu kwa hili.

Nini uhalali wa "taifa" la Zanzibar tangu kupata Uhuru toka kwa Mwingereza, 1963 hadi Mapinduzi ya Mwaka 1964? Uhalali wake unatokana na kura za maoni za wananchi au kitu gani?
 
kama hiyo ndiyo dhana ya uhalali wa taifa kwanini Tanzania siyo halali basi? Maana watu walikubali Nyerere kuwa Rais maana "hakuna chombo chochote cha kuhalalisha uhalali wa nchi"?
Umekosea kuingiza neno halali in the first place, sijajua kwa nini unauliza uhalali wa Tanganyika kufanya muungano kuwa halali! sioni connection kabisa.

Mimi nataka tu ujibu hoja kwa nini wazanzibar hawawezi kujitoa kama wakitaka na kuridhia. Nataka uniambie imeandikwa wapi kuwa nchi zikiungana haziwezi kutenganishwa, ukinijibu hili swali, sina tatizo na mjadala huu.

sijajua mantiki ya kulazimisha kuwa rafiki na mtu ambaye hakutaki! ndio hapo kichwa kinauma,
 
Muungano upo kihalali lakini una matatizo ya msingi period!, Matatizo ya msingi ili kutatuliwa kunahitaji re-vamp of the whole system yaani kuuvunja au kupiga kura upya ...wananchi wa pande zote za muungano period!

kwenye logic hii inaitwa internal contradition:

kama

a: Muungano upo kihalali - maneno ya Tumain na

b: una matatizo ya msingi period!

basi

c: ili kutatuliwa kunahitaji re-vamp of the whole system yaani kuuvunja au kupiga kura upya ...wananchi wa pande zote za muungano period!

Kimantiki pendekezo la "c" haliendani hata kidogo na a na b! kwa sababu tunapiga kura wananchi wote ili kufanya nini? kuleta uhalali - hapana kwani "a" inasema muungano ni halali, je tunapiga kura ili kuondoa matatizo? je kwa kuvunja nchi kwanza tutakuwa tumeondoa matatizo? ni serikali ya nchi gani itasimamia hiyo kura. Na tunapovunja Muungano, Bara ni rahisi kusema turudi kwenye serikali ya Tanganyika, it will be very easy.. lakini Zanzibar warudi kwa serikali ipi, ya baada ya mapinduzi (chini ya ASP na wadau wake) au warudi chini ya serikali ya Umoja chini ya Sultani (ambaye bado yuko hai na anadai kiti chake!?) au wamuombe Muingereza wawe chini yao katika mazingira ya kabla ya uhuru 1963 ili awasaidia kujenga taifa jipya la Zanzibar?
 
Umekosea kuingiza neno halali in the first place, sijajua kwa nini unauliza uhalali wa Tanganyika kufanya muungano kuwa halali! sioni connection kabisa.

siyo mimi nimeingiza maneno haya... nihoja zimetolewa mara nyingi na ndio kiini kabisa cha kutaka kuvunja muungano; kwamba ulivyo sasa si halali! au umeshasahau suala la Wazanzibar 12 walioenda kwenye ofisi ya UN kupinga uhalali wa muungano ati kwa sababu mwanasheria mkuu hakuwa na nakala ya makubaliano ya Muungano na kwa vile hakuwa nayo basi mkataba huo haupo? Tunapozungumzia kuvunja muungano tunaanza kuzungumzia kwanza uhalali wake, hii katika prima facie tunakutana nayo. Hatuwezi kuzungumzia kuvunja muungano bila kuzungumzia uhalali wa Muungano. Kwa hiyo connection ipo na ni rahisi kuiona haiitaji utaalamu wa Fizikia ya anga za mbali.

Mimi nataka tu ujibu hoja kwa nini wazanzibar hawawezi kujitoa kama wakitaka na kuridhia. Nataka uniambie imeandikwa wapi kuwa nchi zikiungana haziwezi kutenganishwa, ukinijibu hili swali, sina tatizo na mjadala huu.
Jibu siyo gumu; hatuwezi kuacha kikundi cha wananchi ati kwa vile "wameridhia" basi wavunje nchi! Tukikubali hata kinadharia tu kuwa sehemu yoyote ya Jamhuri yetu inaweza kutoka sehemu ya muungano, itazuia vipi sehemu nyingine nayo kujitenga alimradi wananchi wake wameridhia? NIkukumbushe ili uelewa kidogo tunapozungumzia Tanzania tunazungumzia nini!

Tujiulize kwanza "Tanzania ni nini"; Katiba yetu inaanza katika ibara ya kwanza na sehemu ya ibara ya 2 kwa kusema hivi (msisitizo wangu):

1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.

2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la
Tanzania Bara
na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni
pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania
inapakana nayo.

Hii ina maana gani? Ina maana ya kwamba Tanzania haiwezi kuvunja na kikundi cha watu kutoka sehemu fulani ya jamhuri hiyo kwani kutakuwa ni kuvunja nchi. Kama wananchi wana haki ya kushiriki katika utawala wa taifa lao na kubadili au kutatua kero wanazoziona kwa kutumia njia na vyombo vilivyopo.

sijajua mantiki ya kulazimisha kuwa rafiki na mtu ambaye hakutaki! ndio hapo kichwa kinauma,

hilo ndio tatizo; huu siyo urafiki na wala siyo mahusiano kama ndoa ambayo yanavunjika kupeana talaka; hii ni nchi! Ni kutokana na hilo Ibara ya 28 inasema hivi:
(3) Mtu yeyote hatakuwa na haki ya kutia sahihi kwenye
mkataba wa kukubali kushindwa vita na kulitoa taifa kwa mshindi,
wala kuridhia au kutambua kitendo cha uvamizi au mgawanyiko
wa Jamhuri ya Muungano au wa sehemu yoyote ya ardhi ya
eneo la taifa
na, bila ya kuathiri Katiba hii na sheria zilizowekwa,
hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri
ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote
anayeshambulia
nchi.
(4) Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosa
la juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano.

Ni kwamba, hatuwezi kuvunja nchi kwa sababu watawala wetu wameshindwa kushughulikia matatizo yetu; tukishapata "hiyo" nchi nyingine nini kitazuia nayo kuvunjwa tukiwa na wanasiasa wenye matatizo yale yale?
 
Kuna wale wazee kutoka Pemba ambao walikuwa wanadai kwamba Pemba haijawahi kuungana na Zanzibar (Unguja) kwa hiyo wanataka Jamhuri yao sijui hatima yao mikononi mwa Usalama wa Taifa ilifikia wapi!
 
Kuna wale wazee kutoka Pemba ambao walikuwa wanadai kwamba Pemba haijawahi kuungana na Zanzibar (Unguja) kwa hiyo wanataka Jamhuri yao sijui hatima yao mikononi mwa Usalama wa Taifa ilifikia wapi!

Ni kweli kwa sababu unajua kwa masaa machache Pemba imewahi kuwa Jamhuri yake.. wakishavunja Tanzania, na Wapemba watasema na sisi tunataka nchi yetu (kumbuka wapemba wengi sana wako nje ya nchi).. na kwa kutumia mantiki ile ile ya "matatizo" nao watataka wawe na nchi yao. Tatizo ni kuwa watu wabara wanafikiria Wazanzibari wakiamua kujitenga na kuruhusiwa basi mambo ya kutaka kujitenga yatakoma. Watu wameshasahau vilivo vya watu wa Mtwara na hata Kigoma ambao nao walitaka kujitenga. Ili kujitenga kuwa nchi si lazima uwe nchi kwanza!
 
Cha kushangaza katika karne hii ya Sayansi na Teknolojia ni hiki:
Ni kama vile Wazanzibari hawakuwepo wakati mambo yafuatayo yalikuwa yanafanyika:
1. Kusainiwa kwa hati za Muungano,
2. Kupitishwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977,
3. Kuunganishwa kwa vyama vya TANU na ASP mwaka 1977,
4. Kuongezwa kwa mambo ya Muungano toka 11 mpaka 22 (suala la mafuta na gesi asilia likiwemo),
5. Kuondolewa kwa nafasi ya Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,
6. Kuanzishwa kwa vyama vingi vya Siasa,
7. Kufanya mabadiliko ya mara kwa mara (amendments) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 hadi ilipofikia mabadiliko ya 14 mwaka 2005,
8.....
Kama walikuwemo wakati mabadiliko hayo yote yanatokea kwa nini wanalalamika mara kwa mara kama vile walikuwa likizo? Mwanzoni walikuwa na heshima ya woga au walipeleka watu kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano ambao hawana sifa? Hii ni kwa sababu suala lolote lihusulo Muungano haliwezi kupitishwa mpaka theluthi mbili ya Wabunge toka Zanzibar na theluthi mbili toka Tanzania Bara wawe wamekubali otherwise halipiti! If that is the case, umefika wakati wa Wazanzibari kuwauliza wawakilishi wao kama walikuwa serious kwa kile walichotumwa kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano! Malalamiko ya baadhi ya viongozi hayawatendei haki wawakilishi wao, sana sana yanawadhalilisha!
 
05.jpg
 
Back
Top Bottom