Westernised African cities... why should the west be interested in?!
They'll talk about Japan, they're modern and have got Japanese architecture. Same thing applies to China. The day we invent our own things and modernise them, surely they'll talk.
Hiii ndiyo mentality kubwa tuliyonayo Waafrika. Ni mentality nzuri kama inatumiwa ipasavyo, kwani inahimiza ushindani, ubunifu na maendeleo. Lakini kwa vile siye tumezungukwa na dhiki za kupindukia, tunafikiri Wazungu wakija kwetu na kuona tuna madaraja, majumba na mavitu kemkem ambayo michoro yake imetoka kwao, na pahala pengi funding imetoka kwao (indirect kutoka kwetu), tunafikiri kuwa wakiona mambo kama hayo watababaika na kuyafanya yawe headlines huko makwao. Tunajidanganya. Hatujiulizi kwanini kila leo hii wanaonesha mbuga za wanyama wetu? Kwanini wako so interested...kwanini... wanapenda kuona nini hawa watu?!!
Wazungu wanababaika wakiona watu kama India wakiiga technology za kurusha satellite, hata kama wameiga. Wanababaika wakiona watu wana handle maliasiri zao na kuzitumia ipasavyo kama nchi za Uarabuni zilivyo. Wanababaikia watu kama northern Korea wakirusha makombora ya masafa ya mbali hata kama ni technolojia za kuigwa. Wanababaikia nchi zinavyo mudu utalii kama nchi za Singapore, Indonesia na nyinginezo kwenye tiger economies.
Wangebabaika sana kama michoro ya nyumba zetu za matope ingelikuwa inapatikana online, tungekuwa na kumbukumbu ya michoro ya nyumba zetu kwa karne kadhaa zilizopita, tungelikuwa tumezi-modernise nyumba zetu za asili na ku-retain architectural distinction. Dhahiri wangelituongelea na kuonesha kila pahali Africa kama tungelihakikisha kuwa mahitaji muhimu yanapatikana kwa kila raia wa nchi zetu.
Jamii ijuayo uwiano thabiti kati ya dharau, ubinafsi, chuki na ustaarab dhidi ya jamii nyingine na baina ya watu wake ni jamii yenye maendeleo. Isiyojua ni dumazi.