The 57th anniversary of Zanzibar Revolution

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,338
Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea mwaka 1964 ili kumuondoa madarakani Sultani wa Zanzibar na serikali yake, iliyoundwa hasa na Waarabu, na hatimaye kuweka uongozi mikononi mwa Waafrika, ambao ndio wengi visiwani humo (230,000 hivi), kwenye bahari ya Hindi, karibu na pwani ya Tanganyika.

Usultani wa Zanzibar ulikuwa umepewa na Uingereza uhuru wake mwaka 1963. Kabla ya hapo, Waarabu walikuwa wamefaulu kudumisha katika mfululizo wa chaguzi utawala waliokuwa nao tangu zamani za Zanzibar kuwa chini ya Usultani wa Omani.

Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP), kilichowakilisha hasa Waafrika, kilipoona kwamba bungeni kina viti vichache ingawa kilipata 54% za kura katika uchaguzi wa Julai 1963, kilipatana na chama cha mrengo wa kushoto Umma Party.

Tarehe 12 Januari 1964 asubuhi na mapema, mwanachama wa ASP John Okello (1937-1971 ?) kutoka Uganda aliongoza wanamapinduzi 600–800 wa kisiwa kikuu cha Unguja kushinda polisi wa nchi na kuteka silaha zao. Halafu walielekea Zanzibar Town walipompindua Sultani Jamshid bin Abdullah na serikali yake. Waliokufa katika mapigano wamekadiriwa kuwa 80 hivi tu.

Kumbe yalifuata kwa siku kadhaa (labda hadi tarehe 20 Januari) maangamizi ya kimbari dhidi ya wakazi wenye asili ya Kiarabu (waliokuwa 50,000 hivi) na ya Asia Kusini (waliokuwa 20,000 hivi); hakuna hakika kuhusu idadi ya waliouawa: makadirio yanataja kuanzia mia kadhaa hadi 20,000.

Kiongozi wa ASP Abeid Karume, asiyekuwa na msimamo mkali akawa rais wa kwanza wa nchi, na wanachama wa Umma party walipewa nafasi serikalini. Kufikia Machi Okello alikuwa ameshawekwa pembeni na kufikia Aprili kikosi chake kimeshanyang'anywa silaha[1].

Mwelekeo wa Kikomunisti wa baadhi katika serikali mpya uliogopesha nchi za Magharibi. Kwa kuwa Zanzibar ilikuwa chini ya athari ya Uingereza, serikali yake iliandaa mipango kadhaa. Hata hivyo, hofu ya kuundwa serikali ya Kikomunisti haikutimia kamwe, na kwa kuwa wananchi wa Uingereza na Marekani waliweza kuhama bila shida, mipango hiyo haikutekelezwa.

Wakati huo nchi za Kikomunisti za China, Ujerumani Mashariki na Umoja wa Kisovyeti zilianzisha mahusiano ya kirafiki na serikali mpya ya Zanzibar kwa kuitambua rasmi na kwa kutuma washauri.

Karume alifanikisha majadiliano ya kuunganisha Zanzibar na Tanganyika ili kuunda hatimaye muungano wa Tanzania; vyombo vya habari vilitafsiri muungano huo kuwa juhudi za kuzuia Ukomunisti kugeuza Zanzibar.

Mapinduzi yalikomesha miaka 200 ya utawala wa Waarabu Zanzibar, na yanaadhimishwa kila mwaka kama sikukuu ya taifa zima la Tanzania.
 
Allah awajaalie qauli thabit waislamu/waarabu wote waliokufa katika vita iliyoongozwa na kafiri okello laanatullah alaihi firauni mmoja huyo.

Hata siku moja haitatokea nishabikie ama kumuenzi huyo okello na wenzie alioshirikiananao kwa namna moja ama nyingine dhidi ya uvamizi huo na kuuwa waislamu/waarabu.

Dahh very sad 😔😔😔 kuna watu walikua makatili waliwanyanyasa sana na kuwauwa,,, wakina mama, wazee, watoto na wamama wajawazito, wengi waliuawa na hayo majahili😡😡😡. Watayakuta malipo yao kwa Mwenyezi Mungu, na pia walikuwemo baadhi ya waislamu walioshiriki vita hivyo na kuuwa waislamu wenzao, Karume n.k. ivi kweli unamshikia ndugu yako bunduki na kumuuwa kweli, inakupa roho!

Waliofanya ukatiri huo walidhani wataishi milele eee. Leo hatunao, imebakia kumbukumbu tu.
 
Kwa nini Okelo aliwekwa pembeni baada ya mapinduzi?
Koffi...

Okello alivikwa blanketi na likamuenea akidhani yeye ni Field Marshall wa kweli na yale mapinduzi yeye ndiye kayafanya.

Okello hakujua kuwa kulikuwa na watu walioandaa mapinduzi kutoka Tanganyika na ndani ya Zanzibar na wala hakuwa na tarifa yoyote kuwa lilikuwapo jeshi la Wamakonde wakata mkonge kutoka Kipumbwi Tanga waliovushwa mapema kwa kazi ile.

Laiti mapinduzi yale yangefeli Okello ndiye angesimama mahakamani kwa mauaji yale na shingo yake ndiyo ingekuwa ya kwanza kuvaa kitanzi.

Kwa ujinga wake na kupewa radio afanye matangazo kwa sababu maalum ya lafidhi yake yeye akaamini kafanikisha mapinduzi.

Ingetosha kwake yeye kuchukua fedha akajirudia kwao Uganda kwa salama lakini blanketi lilikuwa limempendeza na hakutaka kulivua ndiyo akatumwa Hashil Seif akamshughulikie.
 
Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea mwaka 1964 ili kumuondoa madarakani Sultani wa Zanzibar na serikali yake, iliyoundwa hasa na Waarabu, na hatimaye kuweka uongozi mikononi mwa Waafrika, ambao ndio wengi visiwani humo (230,000 hivi), kwenye bahari ya Hindi, karibu na pwani ya Tanganyika.

Usultani wa Zanzibar ulikuwa umepewa na Uingereza uhuru wake mwaka 1963. Kabla ya hapo, Waarabu walikuwa wamefaulu kudumisha katika mfululizo wa chaguzi utawala waliokuwa nao tangu zamani za Zanzibar kuwa chini ya Usultani wa Omani.

Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP), kilichowakilisha hasa Waafrika, kilipoona kwamba bungeni kina viti vichache ingawa kilipata 54% za kura katika uchaguzi wa Julai 1963, kilipatana na chama cha mrengo wa kushoto Umma Party.

Tarehe 12 Januari 1964 asubuhi na mapema, mwanachama wa ASP John Okello (1937-1971 ?) kutoka Uganda aliongoza wanamapinduzi 600–800 wa kisiwa kikuu cha Unguja kushinda polisi wa nchi na kuteka silaha zao. Halafu walielekea Zanzibar Town walipompindua Sultani Jamshid bin Abdullah na serikali yake. Waliokufa katika mapigano wamekadiriwa kuwa 80 hivi tu.

Kumbe yalifuata kwa siku kadhaa (labda hadi tarehe 20 Januari) maangamizi ya kimbari dhidi ya wakazi wenye asili ya Kiarabu (waliokuwa 50,000 hivi) na ya Asia Kusini (waliokuwa 20,000 hivi); hakuna hakika kuhusu idadi ya waliouawa: makadirio yanataja kuanzia mia kadhaa hadi 20,000.

Kiongozi wa ASP Abeid Karume, asiyekuwa na msimamo mkali akawa rais wa kwanza wa nchi, na wanachama wa Umma party walipewa nafasi serikalini. Kufikia Machi Okello alikuwa ameshawekwa pembeni na kufikia Aprili kikosi chake kimeshanyang'anywa silaha[1].

Mwelekeo wa Kikomunisti wa baadhi katika serikali mpya uliogopesha nchi za Magharibi. Kwa kuwa Zanzibar ilikuwa chini ya athari ya Uingereza, serikali yake iliandaa mipango kadhaa. Hata hivyo, hofu ya kuundwa serikali ya Kikomunisti haikutimia kamwe, na kwa kuwa wananchi wa Uingereza na Marekani waliweza kuhama bila shida, mipango hiyo haikutekelezwa.

Wakati huo nchi za Kikomunisti za China, Ujerumani Mashariki na Umoja wa Kisovyeti zilianzisha mahusiano ya kirafiki na serikali mpya ya Zanzibar kwa kuitambua rasmi na kwa kutuma washauri.

Karume alifanikisha majadiliano ya kuunganisha Zanzibar na Tanganyika ili kuunda hatimaye muungano wa Tanzania; vyombo vya habari vilitafsiri muungano huo kuwa juhudi za kuzuia Ukomunisti kugeuza Zanzibar.

Mapinduzi yalikomesha miaka 200 ya utawala wa Waarabu Zanzibar, na yanaadhimishwa kila mwaka kama sikukuu ya taifa zima la Tanzania.
Emmanuel...
Soma kitabu cha Dr. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' ujue historia ya mapinduzi.

Kipo mtandaoni search Google.

Mimi nilikuwa Mtafiti Msaidizi kuanzia mwaka wa 2003 - 2010 kilipochapwa kitabu Marekani.
 
Shukurani mkuu nitafanya hivyo.
 
Back
Top Bottom