Na sio lazima upande yote hata ukikutana na waliopanda mengine mka share experience unaweza jua lipi bovu lipi zuri..niliwahi mention KLM kwa watu walio wahi panda wacha waliponde hasa kwenye msosi....yaani nimejikuta sitaki hata kulijaribu sababu ya feedback za waliolipanda
Natamani kujua Tz ni ya ngapi bila kujali umbali wake na ile ya kwanza
Source ya hizi ranking ni ipi? And how reliable is it? Maana siku hizi kila mahali online kuna ranking na zina tofautiana kwahiyo inabidi uangalie ipi ni reliable maana zingine zipo kibiashara
Binafsi Emirates hawajawahi kuniangusha.Nimewahi tumia KLM na Oman air ila kwa huduma na comfortability hawaifikii emirates. Next is Qatar,sijawahi tumia hawa waarabu wa Doha ili niwalinganishe na Emirates
Mkuu usije jaribu KLM,wadachi hamna kitu.Sio tu chakula hata entertainment zao hovyo pia,labda kwa denge zao za route nyingine,ila kwa route ya Dar to Schiphol haina maraha kama ice ya emirates.
Upo sahihi mkuu kuwa kila mtu na taste yake.Binafsi sina time na chakula kikubwa kwangu ni entertainment maana hewani bila kuburudika safari inaboa na sisi wazee wa economy viti vyetu haviwezi kuwa kitanda kwahyo kulala ni shida.Inategemea unacho prefer...wengine ukarimu wengine msosi...
Niliacha kupanda KLM...ila my next flight lazima nitumie KLM maana nilikutana na pilot charming sana JNIA juzi kati...mpaka nika feel vibaya kwa nini sikuwa mmoja wa abiria wake...alikuwa ana chat na kila mtu na kumuuliza kama ni mmoja wa abiria wake; ndege yao ilikuwa late siku hiyo...I said no...akauliza why...nikamwambia price yenu iko juu kuliko hili shirika nalotumia leo...akanambia next time panda KLM bana...
Kama kuna shirika la hovyooo ni Egypt Air....ukarimu sifuri...cheap ni very expensive...
Afu kuhusu msosi juzi nimepitia article moja yahoo wanasema chakula hata kiwe kitamu vipi ukiwa meter 10,0000 juu kinakuwa na taste mbaya.... na nimekubaliana na hilo
Emirates nimepanda ila i remember nothing...wakati mwingine mimi najali kufika zaidi...
Mara nyingi ndege ambazo huja JNIA na JRO ni kuukuu sana.
Ila tuseme unapandia kutoka Schiphol kwenda NY, LA, ATL, Miami, kwingine dunia ya kwanza, ndege zao huwa bomba sana.
Hata BA wakati bado wanakuja Tanzania ilikuwa hivyo hivyo. Ndege zao unazopanda tokea US kwenda London Heathrow ni nzuri sana kuliko zilizokuwa zinatoka London Heathrow kuja JNIA.
Hata Qatar ndege zinakojua Tanzania ni tofauti sana na zile zinazotoka Qatar kwenda US, Europe, Asia, na Australia.
Nilishawahi kupand Qatar airways jinsi wale mabinti wahudumu walivyokuwa wakarimu hadi nikafikiri wananitaka kimapenzi. bado kidogo mswahili mimi nitie aibu.
Natamani kujua Tz ni ya ngapi bila kujali umbali wake na ile ya kwanza
Ipo top 10 toka chini
Emirates wale waudumu wao, walikua wananikosha ukiwaaangalia sana wanakuacha na bonge moja la smile. basi mzee mzima nawatolea macho tu nione smile zao yaani unaweza sema mtoto kukuelewa kumbe ndo mbwembwe za kazi