GE2025 THBUB yatoa Mafunzo kwa Polisi Arusha Kuhusu Haki za Binadamu na Utawala Bora kuelekea Uchaguzi 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeendesha mafunzo kwa Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha kuhusiana na uzingatiwaji wa haki za binadamu na misingi ya Utawala Bora katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Akizungumza na Askari hao leo Septemba 17, 2025, Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Bw. Mohamed Hamadi amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa tume kufikisha elimu kwa makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo Jeshi la Polisi kwa ajili ya kukumbushana haki na wajibu wao katika kulinda haki za binadamu

Aidha, tume hiyo pamoja na mambo mengine ilipata fursa ya kusikiliza maoni mbalimbali kutoka kwa washiriki wa mafunzo hayo kwa ajili ya kuboresha utendaji wa kazi

Naye Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Faraja Sangwa amesema mafunzo hayo yamekuwa na tija katika kuboresha utendaji wao wa kazi na kuahidi kuwa wataendelea kuhakikisha wanazingatia haki za binadamu katika utekelezaji wa majukumu yao

1758116154437.png

1758116372446.png
 
Hakuna watu wagumu kuelewa kama hao viumbe, ukitaka kuelewa kaandamani kwa amani ndo utajua kunahaki za binadamu au unafanana na Kunguni na siyo binadamu, watakuminya ukutani kama wanapasua Kunguni...
 
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeendesha mafunzo kwa Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha kuhusiana na uzingatiwaji wa haki za binadamu na misingi ya Utawala Bora katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Akizungumza na Askari hao leo Septemba 17, 2025, Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Bw. Mohamed Hamadi amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa tume kufikisha elimu kwa makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo Jeshi la Polisi kwa ajili ya kukumbushana haki na wajibu wao katika kulinda haki za binadamu

Aidha, tume hiyo pamoja na mambo mengine ilipata fursa ya kusikiliza maoni mbalimbali kutoka kwa washiriki wa mafunzo hayo kwa ajili ya kuboresha utendaji wa kazi

Naye Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Faraja Sangwa amesema mafunzo hayo yamekuwa na tija katika kuboresha utendaji wao wa kazi na kuahidi kuwa wataendelea kuhakikisha wanazingatia haki za binadamu katika utekelezaji wa majukumu yao

Hiyo nayo ni sinema kama sinema zingine. Tunatwanga maji kwenye kinu.
 
Back
Top Bottom