Thamani yako kabla ya kupata nafasi

Aug 5, 2019
62
87
Kama huwezi kuisaidia jamii yako kwasasa wakati huna nyadhifa yoyote ile kisiasa unangojea uwe mwanasiasa (Mbunge) ndio uwasaidie wewe ni muongo wa kiwango cha lami na hupaswi kupata hata kura 1, na ndio watu wa aina hii wakishapata huo Ubunge ukiwauliza vipi wanasingizia mfumo
 
Umeongea jambo la msingi sana mleta mada, lakini kwa kuwa jamii yetu inasumbuliwa na tatizo la unafiki, mara nyingi hatuambiani ukweli, na anayeamua kuongea ukweli hapati uungwaji mkono, hivyo wengi hukata taamaa na kuacha iwe inavyokuwa.
 
Siasa inawaendesha wajinga na wasomi.
Mbali na wao kusingizia mfumo, Bado Kuna uzembe kuntu katika sheria ya kuwania uongozi.
Mfano:
A/uwe raia halali wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
B/Uwe unajua kusoma na kuandika kwa ufasaha
C/Uwe na miaka kuanzia 30+

Sasa kwa vigezo kama hivi mtu wa darasa la Saba atapata nyadhifa kwa kuwa Ana tu hela atalaghai ,mwisho anaingia kwenye maamuzi ya kitaifa ,mbali zaidi ni kufanya maamuzi na kuwaongoza wenye degree,master ,na PhD zao.
Unategemea kiongozi kama huyo atabadilisha kipi ili hali kapata kwa njia za hongo hongo kwenye chama .
Cha msingi kungekuwa na vigezo vikali kwanza kwa yeyeto anayetaka kuwania nafasi ya uongozi serikalini ili kupunguza viongozi wanaongoza kwa mihemko.
 
Back
Top Bottom