Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 10,526
- 13,015
Sijui kwanini wanapenda kudanganya wakati wenzao wakitoa takwimu wanakuwa wakali hata kuwaweka ndani.
Mhariri wa gazeti la Uhuru la leo ameandika ukiwa na 10elfu na ukiwa unaishi Tandika Maguruwe unaweza kupika/kuandaa pilau ya kuliwa na watu wanne 4. uongo.
Wametoa mchanganuo wa mahitaji ya kuandaa pilau na kubakiwa na chenji ya tsh 200.
Nimejiuliza maswali mengi sana lakini kubwa ni umuhimu wa habari ile mpaka kuwa kwenye front page? Mhariri yule anataka kusema watu wanaolalamika ugumu wa maisha ni waongo maana sikukuu inaweza kupita kwa elfu 10 tu? Hajui mahitaji ya sikukuu kwamba sio pilau tu kuna mengine kama nguo nk.
Je, mhariri yule anataka kutuaminisha kwamba watanzania wote wanaishi Tandika Maguruwe? Mbona kuna maeneo bei zinatofautiana sana na huko Maguruwe?
Anachotakiwa kujua mhariri wa gazeti la Uhuru na wanaomtuma ni kwamba maisha ya watu yameharibiwa na utawala huu kiasi cha sikukuu kukosa maana. aidha upatikanaji wa hiyo elfu 10 umekuwa mgumu kweli.
Chukulia mfano mkulima wa korosho wa kule Misasa/ Mkuranga hajalipwa pesa mpaka leo kwa kinachoitwa kukagua mashamba hiyo elfu 10 anaipataje?
msidanganye watu