Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,842
- 10,765
Wakuu kumekucha tena. Nimejitia kuandika zaidi kuhusu mabinti kwa lengo moja tu, kujaribu kukifumbua macho kizazi kinachopotea kwa kasi. Najua majibizano na maneno makali yatokayo hasa kwa wanawake kwenye mada za namna hii lakini imefika wakati ukweli lazima usemwe.
Hapa naongelea mabinti wanawali ambao hawajamjua mume bado. Thamani halisi kabisa ya binti iko kwenye bikra yake. Mungu alipomuumba mwanamke alimwekea kiwambo (seal) ambacho ni ni muhimu kwa ajili ya kuweka agano na mume wake wa ndoa. Kama ijulikanavyo katika ulimwengu wa roho, maagano huwekwa kwa damu, ndio maana hicho kiwambo kinapotolewa damu humwagika kama ishara ya kuweka muhuri agano. Kiwambo hicho (hymen) ndio thamani kuu ya binti yeyote hapa duniani. Why?
Bikra ni ishara kuu kwamba binti hajamjua mume bado, kwamba anatambua thamani yake, kwamba uaminifu wake hautiliwi shaka kamwe, kwamba anaweza kujizuia na kujilinda hata mbele ya social pressure, kwamba ni mwenye tabia njema n.k. Binti bikira (mwana mwali) ukimtazama tu tabia na mwenendo wake huwa ni tofauti kabisa na mabinti wengine. Ni mwenye soni, ni mwenye kuepuka maongezi mabaya, ni mtiifu hata kwa wazazi n.k.
Ukimtazama binti aliyeyajua madyudyu utamtambua tu ,hili liko wazi kabisa. Hii haikutokea kwa bahati mbaya, ni mpangilio wa Mungu hali iwe hivyo. Hata kwa wale wasioamini Mungu bado mnaweza kushuhudia hiki nikisemacho. Hata wazazi huhitimisha mafunzo yao kwa binti pale anapoanza tu kushiriki ngono, kwani huhesabiwa kati ya watu wazima.
Sasa basi, tutazame madhara ya binti kujiingiza kwenye mapenzi kabla ya ndoa.
1. Atahesabiwa kati ya makahaba
Ni ukweli usiofichika kwamba mwanamke aliyeanza mapenzi mapema tangu awali aliitwa kahaba. Dunia ya leo imebadili kiasi maana halisi ya neno hilo kumaanisha ni mwanamke ajiuzaye. Lakini ni ukweli kuwa hata huyu ajitoaye huanza kutafuta matunzo kutoka kwa mwanamume anayejamiiana naye, huku ndiko kutafuta mapato (ujira) kwenyewe!! Kupoteza bikra huondoa kiwambo cha agano la mume, hivyo thamani ya mwanamke haipo tena. Hapa uaminifu hupimwa kwa maneno na si matendo tena ambapo ndoa hugeuka tendo la imani. Haipaswi kuwa hivyo, mwnamke ameumbiwa uaminifu tangu kuzaliwa kwake, mume anapaswa kumpima kwenye utii tu.
2. Ulimwengu wa mwili na roho hufunguka
Kama nilivyotoa utangulizi, binti akijiingiza tu kwenye ngono hujiona amekuwa. Tayari hakuna tena siri iliyofichika kwake kwani siri ya mwisho kwa mwanadamu ni tendo la ngono. Ataingia kwenye ulimwengu wa roho akiwa hayuko tayari, kwani tendo la ngono ni tendo la kiroho. Kwa sababu binti huyu hajawa tayari kuukabili ulimwengu, atasombwa na kila aina ya mafundisho kwani amejiingiza kwenye daraja la ujuaji. Kwake yeye si mwanamke mwenzake, si mwanamume wala wazazi wenye jipya la kumpa kwani mafunzo ya binti hukoma pale tu anapomjua mume.
3. Hujiondolea kabisa uwezekano wa kupata ndoa
Kuna tofauti kubwa kati ya kupata mume na kupata ndoa. Watu wengi wameingia kwenye ushirika wa kimahusiano wakidhani kuwa ni ndoa, mwishowe wameishia kujutia kwa kiwango kikubwa. Ushirika wa kimahusiano kwa maana kuwa tayari mwanamke alishafunga agano la ndoa na mwanamume mwingine kabla aliyemtoa bikra, agano la damu lidumulo mpaka kufa kwao, ndipo wakaja kupata mshirika wa kuishi naye kama mume na mke, wakifunga agano la mdomoni tu jambo ambalo ni maigizo ya mchana kweupe. Agano la ndoa ni la damu, binti awaache wazazi wake akiwa INTACT, akaanze maisha na mumewe. Hii ndio ndoa halisi, mengine ni ushirika tu wa mke na mume. Ndio maana ndoa za leo zimejaa malalamiko, manung'uniko, kukosa furaha, kukosa amani n.k.
4. Hugeuka mwanaharakati kwenye mahusiano
Baadhi ya sifa za mke wa ndoa ni heshima na adabu, aibu kwa mume, kutambua nafasi ya mume kwenye ndoa, uaminifu (huthibitishwa na bikra si maneno tu) n.k. Mwanamke aliyejiingiza kwenye ngono kabla, amefunguka ufahamu na kujidhani anaijua dunia kama wanaume tu, hivyo tofauti waliyonayo ni sex organs tu. Wengi wao hugeuka wanaharakati kwenye ndoa zao (ndoa kwa maana mpya) wakidai usawa kwenye mambo mbalimbali ambayo kimsingi ni mgawanyo wa majukumu. Hawaoni tofauti kati ya mtu mke na mtu mume, wasiokuwa na adabu wala heshima. Inashangaza kuwasikia wakidai, mwanamume angebebeshwa mimba kwa japo dakika moja tu asingeweza wakati kumbe huo ni uumbaji, na kama mwanamume huyu angebeba kweli mimba basi angekoma kuitwa mwanamume kwani ni tendo la mwanamke hilo. Ni aina ya wanawake walioharibika akili zao kwa kujazwa mafundisho ya uongo yaliyo kinyume na asili ya mwanadamu.
Hawa ni aina ya wanawake ambao wanadhani wanayajua mapenzi vema, huja na list ya "mimi nataka mume wangu awe na a, b, c..... kwa sababu wameshazibuka. Binti mwenye kulinfa usichana wake hatohangaika asilani kutafuta kijana mwenye kukidhi orodha ndeefu ya sifa kwani bado hajui mapenzi ni nini. Atatulia huku akisubiri ampate mume sahihi kwa kipimo cha wazaxi.
Kimsingi kuoa mwanamke wa namna hii ni bahati nasibu, kwani lolote laweza kuwa ndani ya ndoa. Aweza kuwa mtaratibu na msikivu kabla ya ndoa hasa wakati wa uchumba kusudi amnase mwanamume, kisha ndipo hufungua makucha. Pia kwa sababu ameshaonja ya dunia kabla, hujiingiza kwenye makundi ya wanawake waliozoelea ngono, ambao akili zao zimetawaliwa na namna ya dunia hii, kiasi kwamba apatapo mwanamume wa kumwoa hubadili mwonekano wa nje ili tu afanikishe lengo, kisha matatizo huhamia ndani.
Ni ukweli ndoa nyingi zama zetu zinakwenda kwa kauli mbiu ya kuvumiliana na kuchukuliana mizigo. Kama unabisha fuatilia aina ya mafundisho yatolewayo kwenye semina mbalimbali za ndoa, iwe kwenye dini au tu kwingineko. Vijana wanafunzwa kuwavumilia wake kwenye madhaifu ambayo kimsingi sio madhaifu, ni tabia, pia mabjnti wanafundishwa jinsi ya kuwazuga waume zao ili wawanase kwenye mtego wa penzi. Semina na machapisho ya "JINSI YA KUMTULIZA MUME na mengine ya JINSI YA KUMRIDHISHA MWANAMKE ndio yametamalaki katika zama hizi. Mwanamke akifundishwa jinsi ya kumridhisha mwanamke aliyezoelea maisha ya ukahaba wakati mwanamke naye akifundishwa jinsi ya kumtuliza mwanamume asiyeridhika na kilichomo ndani ya mkewe. Yaani ni ulimwengu wa maigizo tu, hakuna uhalisia.
Najua neno hili ni gumu mno, hivyo nimejiandaa kutupiwa mawe!!