Thadei Ole Mushi: Hivi Tanzania tuna Think Tanks?

..Think Tank ni taasisi sio msomi au mtaalamu mmoja mmoja.

..Ni taasisi inayofanya utafiti wa masuala mbalimbali kwa mfano uchumi, siasa, ulinzi, etc na kutoa ushauri wa kisera kwa serikali, au vyama vya siasa.

..Neno Think Tank halieleweki na linatumika vibaya hapa Tanzania.
Si ndio hao nimewtaja members wa hizo taasisi?
 
..samahani nimekuelewa vibaya.

..prof.kabudi, dr.tulia, na wengine sio think tank / think tanks.

..think tank ni TAASISI yenye wataalamu, inayofanya utafiti na kushauri mambo ya kisera.
 
Ngumu sana hii nchi..

May be watakusikiliza
 
Na Thadei Ole Mushi.

Bei ya mafuta imepanda sana lita moja ya Petrol kwa sasa inafika hadi Shilingi 3,000. Nimeangalia Lita moja ya Mafuta hadi inashushwa pale badarini ni shilingi 1,162.

Yakishafika tunaweka kodi na Tozo Mbalimbali hadi yanafikia zaidi ya 3,000.

Kazi ya Ewura ni kutangaza Bei Mpya tu badala ya Ku regulate na kuishauri serikali. Hawana kazi nyingine wao ni kutangaza tu.... hawawezi hata kunusa kinachoweza kutokea baadaye na kutoa Solutions. Nafikiri kwa Sasa Serikali inaweza kufanya yafuatayo.

1. Kwenye kila kipengele cha Tozo wapunguze angalau kwa Asilimia kadhaa, Mfano badala ya VAT kuwa asilimia 18 wafanye asilimia 10 katika kipindi hiki.

2. Kuna haja ya kuindoa Tozo nyingine kwa sasa zisiwepo hadi hali ya Uchumi wa Dunia utakapotengemaaa.

3. Serikali ipunguze Matumizi yake ambayo si ya lazima kwa sasa mfano kutembelea anuani za Makazi kwa Chopa.

Tusikae kimya.....kazi kubwa ya Serikali ni kuhakikisha maisha ya wananchi wake yanakuwa marahisi... tuchukue hatua angalau kidogo tu kuonyesha tunajali. Maumivu makubwa ya ongezeko hili la bei ya mafuta anaumia mwananchi wa kawaida kabisa huku chini.

Hivi tuna Think tanks za kushauri Serikali?

Pale Marekani Washington DC kuna kituo kinachoitwa "Peterson institute for International Economics" (PIIE).

Kituo hiki kazi yake kubwa ni kutafiti na kushauri masuala mbalimbali ya kiuchumi na mahusiano ya kiuchumi. Kwa Marekani ndipo "Think Tanks" wao wanapofanyia kazi. Ili uajiriwe hapa lazima kichwani pawe vizuri si suala la kushukuru kuondoka jalalani tu ila kweli uwe na independent Mind.

Hawa wajamaa wamepewa Uhuru mkubwa sana wa kutafiti na hawafichi kitu report yote wanaitangaza kama ilivyo, kule kwao top Researchers wote wapo hapa wanasugua akili na sio kitambi. Hawa wajamaa wakiitisha press kila mtu anasogelea TV, na kila Media inawasogelea.

Sio marekani tu nchi kibao kama China, India, Venezuela nk zina Pool ya Think Tanks yaani mtu au kiongozi akitaka kufanya jambo lazima awaone. Achana na Hawa unaosikia kuwa ni mshauri wa Rais masuala ya kisiasa au mshauri wa waziri mkuu. Hawa sifa yao lazima kwanza wawe Huru ndio maana kituo hiki cha Marekani ni private institute...

Mfano pale India wao wamegawanya Think Tanks wao kutokana na maeneo mbalimbali, wana vituo 48 vya Think Tanks kama ACDR hawa wanashughulika na Siasa tu, CICR hawa ni Kilimo tu nk.

Pale uarabuni kituo cha Bookings Doha Center January 30 mwaka 2019 waliitisha panel ya Think Tanks wote katika Zone yao. Waliohudhuria ni pamoja na Nader Kabbani, MKUU wa kituo cha utafiti cha (BDC), Ezzeddine Abdelmoula, manager wa utafiti wa Al Jazeera, Mahjoob Zweiri, mkuu wa Gulf Studies Center ya Qatar University, Sari Hanafi, professor wa American University wengine walikuwa Mohammad Almasri mkuu wa Arab Center kituo cha utafiti na undaji wa Sera, Osman Ayfarah mtangazaji wa Al Jazeera ndiye aliyesimamia majadiliano. Hawa wajamaa wanaiongelea miaka 50 ijayo, mojawapo ya recommendations walizotoa ni Viongozi wao wote kuchukua mawazo kabla ya kufanya chochote kwenye taasisi hizi za Think Tanks.

Nadhani hata hapa kwetu tuna watu wanaoweza kuunda tume ya wachumi wakafanya kazi na mwananchi wa chini akasaidika.

Ole Mushi
0712702602.
Hii nchi ina shida sana na utawala, hatuna viongozi wa maana hata kidogo toka ngazi ya chini mpaka juu
 
Wakati mwingine tunafikiri Na kuandika kama watoto wasiofanya analysis.
Tuko tayari kodi iondolewe Na miradi ya REA ife?
Tuko tayari miradi ya Reli ife?
Hiyo inachukua hela direct kutoka kwenye mafuta.
Hiyo kodi nyingine bado inachangia sana bajeti ya serikali, Leo hii tukiondoa VAT hilo pengo litajaziwa na nini?
Kabla ya kupayuka kama mlevi, Fanya uchambuzi na utoe majibu ya vikwazo
Hajapayuka Ole Mushi na wachangiaji hapa wanaongea UKWELI haswaaa.
Magufuli alipenda kusema "kushindwa kuweka mipango au kupanga, ni kuchagua au kupanga kushindwa". Think Tank ndio dira ya mipango.

Tuna mfano hai wa Air Tanzania, report ya CAG inasema kuwa ndege zimenunuliwa bila ya kuwa na business plan...je tungefanya kuwaconsult think tank ingewaje? Twende SGR, Gas ya Mtwara, na miradi mingine.

Tatizo ni utamaduni wa 10% na rushwa ndio unalididimiza bara la Africa.

Sisi kama watanzania na waafrika tunapaswa kubadilika.

Mwenyenzi Mungu atusaidie
 
Ngumu sana hii nchi..

May be watakusikiliza
Nchi hii sio ngumu. Tunapaswa tuache kulalamika, tubadilike kwa kuchukua hatua.

Tunawarithisha watoto wetu kupiga madili, rushwa na kulalamika...kuna awamu fulani iliongelewa vibaya hata na watoto wadogo.

Natakiwa kubadilika, sote tunatakiwa kubadilika. Mabadiliko ni pamoja na kuwaambia ukweli wanaotupoteza bila oga wowote.
 
Wasomi wenyewe njaa hawa wanaojali kuwafurahisha wanasiasa utatoa wapi think tanks? Kama professor mzima anasema ameokotwa jalalani, anamwita mwanasiasa Mungu.. unategemea nini
 
By Magufuli ,wapinzani wanachelewesha maendeleo Sasa tunaomba CCM watuletee hayo maendeleo
Wanasiasa wengi ni unpredictable and completely unreliable. Focus kubwa ni maisha yao binafsi. Kazi kubwa ni kumsfia aliyekuwepo madarakani akiondoka wanahamia kwa aliyeingia yaani full kumtumikia kafiri upate ...
Hii ya think tanks ni revolution kbwa.
Ilivyo kwa sasa think tank master general ni kionngozi wa mhimili uliojisimika zaidi. Kama sio killing tank ni nini!
 
Na Thadei Ole Mushi.

Bei ya mafuta imepanda sana lita moja ya Petrol kwa sasa inafika hadi Shilingi 3,000. Nimeangalia Lita moja ya Mafuta hadi inashushwa pale badarini ni shilingi 1,162.

Yakishafika tunaweka kodi na Tozo Mbalimbali hadi yanafikia zaidi ya 3,000.

Kazi ya Ewura ni kutangaza Bei Mpya tu badala ya Ku regulate na kuishauri serikali. Hawana kazi nyingine wao ni kutangaza tu.... hawawezi hata kunusa kinachoweza kutokea baadaye na kutoa Solutions. Nafikiri kwa Sasa Serikali inaweza kufanya yafuatayo.

1. Kwenye kila kipengele cha Tozo wapunguze angalau kwa Asilimia kadhaa, Mfano badala ya VAT kuwa asilimia 18 wafanye asilimia 10 katika kipindi hiki.

2. Kuna haja ya kuindoa Tozo nyingine kwa sasa zisiwepo hadi hali ya Uchumi wa Dunia utakapotengemaaa.

3. Serikali ipunguze Matumizi yake ambayo si ya lazima kwa sasa mfano kutembelea anuani za Makazi kwa Chopa.

Tusikae kimya.....kazi kubwa ya Serikali ni kuhakikisha maisha ya wananchi wake yanakuwa marahisi... tuchukue hatua angalau kidogo tu kuonyesha tunajali. Maumivu makubwa ya ongezeko hili la bei ya mafuta anaumia mwananchi wa kawaida kabisa huku chini.

Hivi tuna Think tanks za kushauri Serikali?

Pale Marekani Washington DC kuna kituo kinachoitwa "Peterson institute for International Economics" (PIIE).

Kituo hiki kazi yake kubwa ni kutafiti na kushauri masuala mbalimbali ya kiuchumi na mahusiano ya kiuchumi. Kwa Marekani ndipo "Think Tanks" wao wanapofanyia kazi. Ili uajiriwe hapa lazima kichwani pawe vizuri si suala la kushukuru kuondoka jalalani tu ila kweli uwe na independent Mind.

Hawa wajamaa wamepewa Uhuru mkubwa sana wa kutafiti na hawafichi kitu report yote wanaitangaza kama ilivyo, kule kwao top Researchers wote wapo hapa wanasugua akili na sio kitambi. Hawa wajamaa wakiitisha press kila mtu anasogelea TV, na kila Media inawasogelea.

Sio marekani tu nchi kibao kama China, India, Venezuela nk zina Pool ya Think Tanks yaani mtu au kiongozi akitaka kufanya jambo lazima awaone. Achana na Hawa unaosikia kuwa ni mshauri wa Rais masuala ya kisiasa au mshauri wa waziri mkuu. Hawa sifa yao lazima kwanza wawe Huru ndio maana kituo hiki cha Marekani ni private institute...

Mfano pale India wao wamegawanya Think Tanks wao kutokana na maeneo mbalimbali, wana vituo 48 vya Think Tanks kama ACDR hawa wanashughulika na Siasa tu, CICR hawa ni Kilimo tu nk.

Pale uarabuni kituo cha Bookings Doha Center January 30 mwaka 2019 waliitisha panel ya Think Tanks wote katika Zone yao. Waliohudhuria ni pamoja na Nader Kabbani, MKUU wa kituo cha utafiti cha (BDC), Ezzeddine Abdelmoula, manager wa utafiti wa Al Jazeera, Mahjoob Zweiri, mkuu wa Gulf Studies Center ya Qatar University, Sari Hanafi, professor wa American University wengine walikuwa Mohammad Almasri mkuu wa Arab Center kituo cha utafiti na undaji wa Sera, Osman Ayfarah mtangazaji wa Al Jazeera ndiye aliyesimamia majadiliano. Hawa wajamaa wanaiongelea miaka 50 ijayo, mojawapo ya recommendations walizotoa ni Viongozi wao wote kuchukua mawazo kabla ya kufanya chochote kwenye taasisi hizi za Think Tanks.

Nadhani hata hapa kwetu tuna watu wanaoweza kuunda tume ya wachumi wakafanya kazi na mwananchi wa chini akasaidika.

Ole Mushi
0712702602.
Pengine “think cups” watakuwepo.
 
Mtendaji wa kijiji ana elimu ya form four tena failure, wabunge wengine elimu ya darasa la saba. Unategemea mchango gani kwa hawa watu. Nchi inaongozwa na vilaza.
 
Think tank wapo wengisana na wanafanya kazi zao kwa weledi ndio maana Tanzania tunakwenda vizuri.

Naomba kuwatambua kwa chache tu

Dr. Mpango
Dr Mwigulu
Dr. Doto
Prof Kabudi
Dr. Kitila
Dr. Adeladus

Dr. Tulia
Dr Job
Prof Luoga

n.k
😀😀☺️😎 Kama hawa ndio sink tanks wako ukapimwe akili.
 
Wanasiasa wengi ni unpredictable and completely unreliable. Focus kubwa ni maisha yao binafsi. Kazi kubwa ni kumsfia aliyekuwepo madarakani akiondoka wanahamia kwa aliyeingia yaani full kumtumikia kafiri upate ...
Hii ya think tanks ni revolution kbwa.
Ilivyo kwa sasa think tank master general ni kionngozi wa mhimili uliojisimika zaidi. Kama sio killing tank ni nini!
Wakati wanapora uchaguzi uliwasaidia? acha wafanye wanavyotaka.
 
Wasomi wenyewe njaa hawa wanaojali kuwafurahisha wanasiasa utatoa wapi think tanks? Kama professor mzima anasema ameokotwa jalalani, anamwita mwanasiasa Mungu.. unategemea nini
Sijui sisi laia wa LY tutasema tuko wapi, kama Prof yuko jalalani
 
Bei ya mafuta imepanda sana lita moja ya Petrol kwa sasa inafika hadi Shilingi 3,000. Nimeangalia Lita moja ya Mafuta hadi inashushwa pale badarini ni shilingi 1,162.
Aisee

Anyway, tuendelee kubamizwa.

Watanzania tuna ujinga sana.

Tunaletaga ujuaji kwenye mambo ya msingi.

____________

Ole Mushi ni cross ya mmasai na mchaga? 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom