Alex Fredrick
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 680
- 1,338
HIVI TANZANIA TUNA THINK TANKS?
Na Thadei Ole Mushi.
Bei ya mafuta imepanda sana lita moja ya Petrol kwa sasa inafika hadi Shilingi 3,000. Nimeangalia Lita moja ya Mafuta hadi inashushwa pale badarini ni shilingi 1,162.
Yakishafika tunaweka kodi na Tozo Mbalimbali hadi yanafikia zaidi ya 3,000.
Kazi ya Ewura ni kutangaza Bei Mpya tu badala ya Ku regulate na kuishauri serikali. Hawana kazi nyingine wao ni kutangaza tu.... hawawezi hata kunusa kinachoweza kutokea baadaye na kutoa Solutions. Nafikiri kwa Sasa Serikali inaweza kufanya yafuatayo.
1. Kwenye kila kipengele cha Tozo wapunguze angalau kwa Ailimia kadhaa, Mfano badala ya VAT kuwa asilimia 18 wafanye asilimia 10 katika kipindi hiki.
2. Kuna haja ya kuindoa Tozo nyingine kwa sasa zisiwepo hadi hali ya Uchumi wa Dunia utakapotengemaaa.
3. Serikali ipunguze Matumizi yake ambayo si ya lazima kwa sasa mfano kutembelea anuani za Makazi kwa Chopa.
Tusikae kimya.....kazi kubwa ya Serikali ni kuhakikisha maisha ya wananchi wake yanakuwa marahisi... tuchukue hatua angalau kidogo tu kuonyesha tunajali. Maumivu makubwa ya ongezeko hili la bei ya mafuta anaumia mwananchi wa kawaida kabisa huku chini.
Hivi tuna Think tanks za kushauri Serikali?
Pale Marekani Washington DC kuna kituo kinachoitwa "Peterson institute for International Economics" (PIIE).
Kituo hiki kazi yake kubwa ni kutafiti na kushauri masuala mbalimbali ya kiuchumi na mahusiano ya kiuchumi. Kwa Marekani ndipo "Think Tanks" wao wanapofanyia kazi. Ili uajiriwe hapa lazima kichwani pawe vizuri si suala la kushukuru kuondoka jalalani tu ila kweli uwe na independent Mind.
Hawa wajamaa wamepewa Uhuru mkubwa sana wa kutafiti na hawafichi kitu report yote wanaitangaza kama ilivyo, kule kwao top Researchers wote wapo hapa wanasugua akili na sio kitambi. Hawa wajamaa wakiitisha press kila mtu anasogelea TV, na kila Media inawasogelea.
Sio marekani tu nchi kibao kama China, India, Venezuela nk zina Pool ya Think Tanks yaani mtu au kiongozi akitaka kufanya jambo lazima awaone. Achana na Hawa unaosikia kuwa ni mshauri wa Rais masuala ya kisiasa au mshauri wa waziri mkuu. Hawa sifa yao lazima kwanza wawe Huru ndio maana kituo hiki cha Marekani ni private institute...
Mfano pale India wao wamegawanya Think Tanks wao kutokana na maeneo mbalimbali, wana vituo 48 vya Think Tanks kama ACDR hawa wanashughulika na Siasa tu, CICR hawa ni Kilimo tu nk.
Pale uarabuni kituo cha Bookings Doha Center January 30 mwaka 2019 waliitisha panel ya Think Tanks wote katika Zone yao. Waliohudhuria ni pamoja na Nader Kabbani, MKUU wa kituo cha utafiti cha (BDC), Ezzeddine Abdelmoula, manager wa utafiti wa Al Jazeera, Mahjoob Zweiri, mkuu wa Gulf Studies Center ya Qatar University, Sari Hanafi, professor wa American University wengine walikuwa Mohammad Almasri mkuu wa Arab Center kituo cha utafiti na undaji wa Sera, Osman Ayfarah, mtangazaji wa Al Jazeera na aliyesimamia majadiliano. Hawa wajamaa wanaiongelea miaka 50 ijayo, mojawapo ya recommendations walizotoa ni Viongozi wao wote kuchukua mawazo kabla ya kufanya chochote kwenye taasisi hizi za Think Tanks.
Nadhani hata hapa kwetu tuna watu wanaoweza kuunda tume ya wachumi wakafanya kazi na mwananchi wa chini akasaidika.
Ole Mushi
0712702602.