TGIF: Yote tisa ngoma ni za Wasukuma, Wangoni na Wamakonde! hamtaki!!

Mwanakijiji umenikumbusha mbali sana!! I miss home now, ilikuwa baada ya mavuno watu kila siku "Chagulaga" na baskeli pembeni baada ya ngoma, maisha yalikuwa bila stress! Lakini sasa no more, hapa nilipo najidundika na stress za kizungu. Kutoka Shinyanga - Ukenyenge.
 
Wasukuma nadhani wanaongoza kwa ngoma,na ni kitu kilichoko damuni kabisa,kwa tafiti isiyo rasimi,hata majeshini wengi wako kikosi cha bendi,hata polisi wako wengi tu kwenye bend wanapiga ngoma.
Ngoma maarufu kabisa ni zile za bhagalu na bhagika,zilizoasisiwa na wazee wetu kina ibhamba ngulu,kina gindu nkima,kina Jilya mag'ondi,kina Jilunga na wengine wengi.
 
nkingwa umenichekesha sana..Baba alikukataza...aliona mbali...
 
Back
Top Bottom