TFF yaunda Kamati inayoongozwa na Paul Makonda ya kusaidia Taifa Stars ishinde kufuzu AFCON! Je, kazi yake ni nini hasa?

Tumbo Tumbo

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
1,278
1,553
Kuelekea kwenye mchezo wa kufuzu kushiriki michuano ya AFCON 2019, Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) limetangaza majina 14 yatakayokuwa kwenye kamati iliyopewa jina la Saidia Taifa Stars ishinde.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Katibu ni Mhandisi. Hers Said.

Wajumbe wengine ni pamoja na Mohamed Dewj 'Mo' Farouk Barhoza, Salim Abdallah, Patrick Kahemele na Abdallah Bin Kleb na Mohamed Nassor.

Wengine ni pamoja na Tedd Mapunda, Philimon Ntaihaja, Farid Nahid, Faraji Asas, Jery Muro na Haji Manara.

Stars watakuwa na kibarua mwezi Marchi kucheza na timu ya Taifa ya Uganda ili kufuzu hatua hiyo ya AFCON na dua zao zikiwa kwa Lesotho kupoteza mbele ya Cape Verde

Kwenye kundi L ambalo Stars ipo Uganda wamefuzu baada ya kufikisha pointi 13 huku Stars na Lestho zikiwa na pointi tano na Cape Verde wana pointi nne

IMG-20190220-WA0069.jpeg


My take:
Vyombo vyetu vya habari na waandishi wabobezi wa michezo ni kwangu pakavu, wao wangetuamsha kwa kufanya awareness raising campaign.

Tukatae ubabaishaji wa aina hii michezoni maana wanaonufaika ni wachache

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kamati tu wataunda hadi vikoba lakini bado hatutoboi.

Badala ya kuwekeza katika kuboresha michezo kuanzia ngazi za chini hadi ligi kuu wao wanakuja na ngonjera za kamati tena ktk mechi moja tu huku za awali mshaharibu. Inabidi waache kuchukulia mambo simplesimple na kutuletea Siasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa akili Hizi Za Tff mpira hautakaa Usonge mbele, acha tufungwe tu maana waganda wamejiandaa kwenda, eti kamati ya ushindi, hivi walishatafakari na kujiuliza kwamba ili Taifa Stars Ishinde inahitaji Kamati?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa jamaa wajinga sana... Tatizo ni kuwa na viongozi wasiojua mpira ni mwendo wa kukurupuka tu.
Sasa sijui hiyo kamati ndio itaenda kucheza au wanachukulia mpira ni kama harusi hivi ndio maana wanaunda kamati
Kwa akili Hizi Za Tff mpira hautakaa Usonge mbele, acha tufungwe tu maana waganda wamejiandaa kwenda, eti kamati ya ushindi, hivi walishatafakari na kujiuliza kwamba ili Taifa Stars Ishinde inahitaji Kamati?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa hicho ni kikundi cha wafanyabiashara na hapo makonda ndio muda wa kunyanga'anya kwa kusingizia stars. Huyo farukh ni tsn, bin kleb afroil, hersi ndio msimamiz wa GSM,faraj ni Asas na Ndugu yake farid nahid, kuna mo hapo na Nassor pia namuona sijui kama watatoa hela sababu zamn walikuwa wanachngia huku kodi wanabania siku hizi mnawabana kila Kona letu jicho
 
Au ndio tuseme Kwamba Haji manara Hamasa uwanjani watu wajitokeze. Dewji Hamasa kwa wachezaji kwa kuwaahidi kuwasajili simba wote endapo tu watashinda. Paul Makonda kuboresha ulinzi Dar stadium include. Jerry Muro faraja kwa Manara ili wafanye kazi vizuri kwa amani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamati za tff kusimamia timu hazijawahi kuleta mafanikio...hapo imejaa siasa na usimba tu inawa wapo Yanga wachache....hovyo kabisa....
 
Tati

Kwa maoni yangu hii kamati imekaa "kisiasa" zaidi watu kama Zitto kabwe wako wapi? au "Msomali" anaogopa kelele za Lumumba, Bashite hakustahili kuwepo kwa kuwa si mtu wa mpira bali ni mtu wa kurukia rukia kila jambo lenye mvuto kwa watu..Anyway hili ndio tatizo la kutengeneza kamati kabla ya kujua nini lengo na kazi ya kamati hiyo....
 
Back
Top Bottom