TFF Na Soka la Vijana!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TFF Na Soka la Vijana!!

Discussion in 'Sports' started by NasDaz, Jul 20, 2009.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Under 17 imeisha! Na kwa waliofuatilia angalau kwa mchezo kati ya Mjini Magharibi na Tabora basi atagundua kwamba nchi yetu ina hazina kubwa ya vipaji vya soka! Hata hivyo, pamoja na kuonekana kwa nia ya kuendeleza soka la vijana nchini, shaka yangu ni kwamba isije ikawa ni nia ya kukamilisha tu kalenda ya TFF! Mathalani, msimu uliopita tuliona ligi ya vijana wa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom! Binafsi ligi hiyo ya vijana niliiona ni kama iliyolenga tu kukamilisha kalenda ya TFF kwavile sikuona kama ilikuwa na ushindani wowote wa maana. Timu karibu zote ambazo zilishiriki kwenye ligi hiyo (ya vijana wa timu za ligi kuu) zilionesha wazi kwamba ama hazikuwa na maandalizi ya kutosha au hazikuwa na maandalizi kabisa!! Pamoja na yote hayo, bila shaka wapenda soka nchini wangependa kuiona ligi au mashindano haya nayo yanakuwa ya kiushindani ili iweze kuzalisha wachezaji waliokomaa. Changamoto iliyopo ni namna gani basi mashindano hayo yanaweza kuleta ushindani. Ni matumaini yangu kwamba, endapo mashindano haya kwa vijana wa timu za ligi kuu yakiendeshwa vizuri na kiushindani basi bila shaka tutazalisha wachezaji wazuri sana. Na namna bora ya kuifanya ligi hii kuwa ya ushindani ni kuzifanya timu za ligi kuu kutoyadharau mashindano haya. Kwa mfano, tunaweza kuunda sheria kwamba robo ya jumla ya pointi za kila timu kutoka ligi ya vijana zijumlishwe kwenye timu zao zilizopo ligi kuu. Tuseme timu kubwa ya Yanga imemaliza ligi kuu na kujikuasanyia pointi sitini na mbili huku ikifuatiwa na Simba iliyojizolea pointi Sitini; halafu kwenye ligi ya vijana Simba imejikusanyia pointi hamsini na sita na yanga pointi arobaini na nne. Hapo maana yake ni kwamba tutachukua pointi 14 (robo ya pointi 56) kutoka timu ya vijana ya Simba na kuziingiza kwenye ligi kuu na hivyo kuifanya timu hiyo kuwa na 74 ( 60 za ligi kuu + 14 za ligi ya vijana)!Aidha, tutachukua pointi kumi na moja (robo ya 44 ) kutoka timu ya vijana ya Yanga na kuziingiza kwenye ligi kuu na hivyo kuifanya timu hiyo kuwa na pointi sabini na tatu ( 62 za ligi kuu + 11 za ligi ya vijana)! Hivyo basi, ingawaje Yanga ilikuwa na pointi nyingi kwenye ligi kuu, matokeo ya jumla itaifanya Simba kuwa ndie kinara wa ligi. Kwa mtindo huo, mara zote msimamo wa ligi kuu utakuwa unatikisika. Yule ambae angebaki kwenye ligi kuu atajikuta anashuka na yule ambe angeshuka atajikuta anabaki kwenye ligi kuu! Katika hili, sina shaka yoyote kwamba timu zilizopo ligi kuu hazitaifanyia masihara ligi ya vijana kwavile watafahamu kwamba ligi hiyo ina uwezo wa kuwakosesha ubingwa au hata kuwashusha daraja! NAJENGA HOJA!
   
 2. A

  Ambokile New Member

  #2
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa hatutafuti vipaji bali tunatafuta wazee kama vp TFF ianzie miaka 5
   
 3. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  you are right, lakini wakiwa serious hata hapo walipoanzia si haba!!! Ili tuweze kukimbia tunahitaji kufanya yote hayo (from 5 years na program za sasa) kwa pamoja!
   
Loading...