Hongereni Simba kwa ushindi wa jana.
Lakini nawakumbusha tena kuna mambo fulani yanonekana kama madogo madogo hivi yasipokemewa na benchi la ufundi au uongozi mtaendelea hivyo hivyo kutamba mna timu nzuri sana lakini makombe mtakuwa mnayaona yakipita hapo Msimbazi na "parade" yakielekea Jangwani.
1. Kulazimisha kucheza Lunyasi kwenye viwanja vibovu vya mikoani badala ya kutafuta tu matokeo kwa njia yoyote ile. Timu ipo Tanga uwanja wake sio rafiki sana kama KMC lakini mabeki wanalazimisha kuanza "build up" nyuma tena kwa pasi fupi fupi na nyingine zinapigwa katikati na kipa wao na wala sio pembeni. Kwa mtindo huo muda sio mrefu kuna mlio utatoka na nguvu zote zinazotumika sasa hivi kumkimbiza mtani wake zitakuwa kazi bure kabisa. Kuna "pressing" fulani Coastal walikuwa wanaifanya lakini walikuwa wanaikosea kidogo sana lakini sasa ikitokea timu ikaifanyia "homework" vizuri basi kuna beki yatamkuta kama yaliyomkuta Mwamnyeto maana hawa Kurwa na Doto hawana uvumilivu mchezaji akikosea anageuka kuwa adui wa timu bila kujali mangapi mazuri mchezaji ameyafanya.
2. Kuridhika na ushindi kiduchu. Hili ni kama Simba wamelaaniwa nalo. Simba ikishapata goli mbili tatu basi akili za wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wanajua mechi imeisha hata kama wanacheza na kibonde wanaoweza kumpiga 10-0. Wachezaji wanaanza kucheza "rede" uwanjani badala ya kutoa adhabu ya kikatili kwa timu pinzani. Hili watu wamelipigia sana kelele tangu mwanzoni mwa msimu lakini Simba wakalipuuza. Hivi viongozi wanakumbuka vizuri nini kilitokea msimu wa 2016/17 ambapo tofauti ya magoli 10 tu ndio ilimfanya Yanga akabeba ubingwa pamoja na kulingana pointi na Simba kila mmoja akiwa na pointi 68. Na mwishoni mwa msimu huu ikitokea Simba mmelingana pointi na Yanga mtamlaumu nani wakati kuna vibonde mlikuwa manakutana nao mnawafunga goli mbili tatu halafu mnaanza "show" za kijinga uwanjani na msemaji wenu anatamba kwenye vyombo habari akijisifu na pira biriani.
3. Kipa wao Kasali kujisahau na kusogea mbele sana ya goli. Asipojerekebisha yatamkuta yaliyomkuta Diara kutoka kwa Selemani Bwenzi wa Kengold. Coastal wamemkosakosa kama mara mbili hivi lakini yeye kama vile hajashtuka lakini kwa mechi chache zijazo akiendelea hivi atakutana na watu wenye "target" nzuri na nguvu za kupiga mipira mirefu kutokea mbali halafu kifuatacho atalokota kunyavu.
4. Mbinu za kuua mechi mapema sana. Simba huwa wanazembea sana na huanza kurelax hata kabla hawajaiua mechi. Mfano mzuri mechi ya jana na Coastal walipaswa walipoingia tu kipindi cha pili walazimishe (na ilikuwa inawezekana) kupata goli la tatu halafu ndio wa "relax". Lakini kwao ilikuwa tofauti walianza ku "relax" baada tu ya kipindi cha pili kuanza matakeo yake sasa kwa kua tofauti ya goli moja huwa halina "cover" wachezaji pamoja na mashabiki wao walikuwa roho juu mwishoni mwa mchezo wakati Coastal wamecharuka. Na almanusura Kibabage aharibu sherehe achilia mbali krosi moja ambayo kuna mshambuliaji mmojan wa Coastal alipiga kichwa akapaisha. Na tabia yao hii mbovu ndio ilisababisha wakagawana pointi na Yanga. Yanga mwanzoni mwa mchezo walipoteana kabisa wakaruhusu magoli mawili badala Simba waiue mechi kabisa kwa kuongeza magoli waka "relax" kilichowakuta sasa mechi ikawapalia mwishoni wakawa wanaomba mechi iishe lakini hawakujifunza kitu wamerudia makosa yale yale jana dhidi ya Coastal.
5. Mpanzu vitu vingi uwanjani anajitahidi anafanya kwa usahihi kwa kiasi kikubwa sana lakini kuutumbukiza mpira golini ndio imekuwa shida yake kubwa sana kwa sasa hivi. Ushauri wa bure kwa Simba mtafutieni Mpanzu mtaalam wa saikolojia maana sio kwa kukosa magoli ya wazi kila mechi kiasi kile. Angekuwa ni mchezaji mpya watu wasingeshangaa lakini ni mchezaji mzoefu na hata kwenye ligi yetu ameshadhihirisha kuwa ni mfungaji mzuri sana na amekuwa akifunga magoli magumu kweli kweli. Lakini sasa hivi hata magoli rahisi kabisa hata yale ya kugusa tu hawezi kufunga. Anahitajika apate ushauri nasaha ili arudishe ule utulivu wake ndani ya "box" kama alivyokuwa mwanzoni wakati amekuja tu Tanzania. Pia benchi la ufundi limkumbushe kanuni moja ya msingi sana timu kwanza yeye kufunga atafunga tu. Kwa hiyo awe anaachia mipira mapema kwa wenzake ikitokea wamefunga sawa sifa inaenda kwa timu nzima pamoja na yeye aliyetoa pasi hivyo asing'ang'anie kupita na mipira kati kati ya wachejizaji wa timu pinzani wakati wenzake wapo kwenye nafasi nzuri za kufunga. Yeye aachie mipira afungue nafasi wenzake wakimuona yupo kwenye nafasi sahihi watamrudishia atafunga tu tena utakuta wakati mwingine kwa urahisi zaidi. Asipokuwa makini na hili siku si nyingi atakuwa kama Jean Baleke aliyekuwa hatari sana na kufunga magoli magumu kweli kweli halafu akapotea kama upepo kimasihara hivi.
Ni mtizamo tu