TFF na NBC hazijawatendea haki wapenzi wa mpira wa miguu Tanzania

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Habarini Za Wakati kama Huu…

Vilabu vyetu vinavyoshiriki Ligi kuu Tanzania Bara huwa vinahangaika sana kwenye kuhakikisha Ligi Yetu Inakuwa Bora na Yenye kusisimua, Haya huonekana Wakati wa Usajiri na wakati wa Maandalizi ya Msimu Mpya. Wamekuwa Wakihangaika Sana kutafuta wadhamini na Wadau mbalimbali kuhakikisha Timu inakuwa imara na yenye ushindani Lengo likiwa ni Kuifanya ligi yetu kuwa bora.

Kupitia Haya Vilabu vimefanikiwa sasa ligi Yetu inashika Nafasi ya 8 afrika kwa Ubora.

Je TFF wanafanya nini Kuhakikisha kuwa Ligi yetu inazidi kuwa Bora, kubwa na yenye kuvutia? Ni kuendelea kutafuta wadhamini.

Lakini Najiuliza ni KWANINI TFF imekubali Udhamini Wa Tsh 2.5 Billioni Tuuuu… Kwa Level ya Ligi yetu ilipofikia, Kumpokea mdhamini wa 2.5 Billioni Ni Kuidharirisha Ligi yetu na Kuto itakaia Mema.

Niwe Muwazi Nilipo anza kusikia Tetesi kuwa NBC anaenda Kuwa Mdhamini nilijua Tuu hapa hamna Pesa Ni Porojo. Haiwezekani Mdhamini wa Ligi kwa Miaka 3 akaweza 2.5 Billioni kwa Vilabu Karibia 16 huku ni kurudisha Nyuma Ligi yetu na Kutokuitakia Mema Ligi Yetu.

Kiukweli TFF mnahusika Kwa Asilimia 100 kuihujumu Ligi Yetu. 2.5 Billioni Kumbe hata Vunja Bei, Clouds, Wasafi na Wengine wangeweza kuweka Hilo dau na Zaidi.

Swali Ni je TFF mlikosa Mdhamini wa zaidi ya 2.5 Billioni? Au vigezo vyenu ni vipi katika hili? Mnafikiria hali halisi ya Tanzania na vilabu vyake na Ligi ilipofikia? Mbona Azam Aliweka Pesa ndefu kila mtu akanyanyua mikono juu?

Ifike pahala sasa TFF uchaguzi wake uwe unafanywa na vilabu na wadau wa soka ili tupate viongozi wenye akili wanaoweza Kuifikisha ligi yetu pahala fulani.

Kama Ligi Ina Mdhamini wa 2.5 Billioni unategema Kuna Club itakuja kutoka na kusajiri Mchezaji wa Zaidi ya 2.5 Billioni au hata Wa 1 Billioni?

TFF na NBC mmetupiga na kitu Kizito Kichwani wapenzi wa mpira wa miguu Tanzania.

Karia OUT
 
Watanzania mna malalamiko sana.

Wakati Azam anaweka Bil 220+ mliilalamikia TFF kwanini wamekubali kupokea kiasi kidogo kwa miaka 10 na wengi mkaenda mbali mkisema Bil 220+ za Azam ni ndogo sana.

Hali halisi ya makampuni ya udhamini yako hivyo kama ambavyo Vodacom walivyokuwa na NBC walivyokuja. Sioni kampuni yoyote ya kitanzania ambayo inaweza kutoa walau Bil 20 kwenye soka mbali na Azam.
 
Umekurupuka.

Mbona inaeleweka kuwa ni 2.5B kwa mwaka huu wa kwanza.
Mkataba upo open kwa mazungumzo kati ya pande zote kwa miaka miwili iliyobaki ( kiasi chaweza kuongezeka)

Hii ni siasa Mkuu, Vigezo vya kumpata mdhamini Ni Vipi? Kwanini Kuwe na Mazungumzo Baadae?
 
Azam wametoa pesa nyingi kwa sababu yeye anaingiza pesa moja kwa moja kama mmiliki wa haki za matangazo ya television.Na ndio chanzo kikuu cha mapato kwa ligi yoyote duniani.

Halafu hela waliotoa NBC sio kwa miaka yote mitatu ni kwa msimu huu to get facts right.
 
Back
Top Bottom