Tff na michael wambura vipi?

ikizu

JF-Expert Member
Oct 26, 2011
431
56
KATIBU mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT), sasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Micheal Wambura amelitupia dongo shirikisho hilo na kusema linafanya maamuzi kwa kukurupuka.Kauli ya Wambura imekuja siku moja baada ya Kamati ya Rufaa ya TFF kumsafisha na kusema, Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho hilo ilikosea kumuengua kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Soka Mara (FAM).
Hata hivyo, wakati Kamati ya Uchaguzi ya TFF ikitamka Wambura alistahili kugombea nafasi hiyo, tayari uchaguzi wa FAM umeshafanyika na kupata viongozi wapya, ambao ni Mwenyekiti Fabian Samo na Makamu, Deogratius Rwechungura.
Akizungumza jana, alisema aliamua kupigania haki yake mpaka dakika ya mwisho kwa vile alistahili kusikilizwa kutokana na kuwa na sababu za msingi.
"Nia yangu ilikuwa ni kuhakikisha haki yangu inapatikana ndio maana nilisimama kwenye misingi ya haki. Mimi nazifahamu sheri na taratibu ndio maana sikukata tamaa," Wambura
"Hili ni fundisho kwa TFF, ni lazima wawe makini wanapotoa uamuzi badala ya kukurupuka. Kama ningekata tamaa mapema, haya yote yasingetokea," alisema zaidi.
"Niliambiwa sina sehemu nyingine ya kukata rufaa zaidi ya Mahakama ya michezo ya Kimataifa (CAS), lakini kwa kuzijua sheria niliamua kutetea haki yangu."
"Sasa naweza kusema kuwa nimetendewa haki, hili liwe fundisho kwa wapenzi wa michezo kutokata tamaa mpka dakika ya mwisho, kutoyumbishwa na watu wasiojua sheria.
Siwezi kusema, kwa sababunimeshinda rufaa yangu basi uchaguzi ufanyike tena. Naepusha migogoro, soka haina utamaduni huo."
Kuhusu kugombea kwenye uchaguzi ujao wa mwakani wa TFF, Wambura alisema:
"Sijastaafu masuala ya soka, nipo tayari kugombea kwenye uchaguzi wowote kwa kuwa kugombea sio dhambi.
"Wambura alienguliwa kwenye kinyanganyiro cha kuwania uongozi wa FAM baada ya kukatiwa rufaa na Titus Osoro kwa madai kuwa aliwahi kuipeleka Simba mahakamani kinyume na katiba ya TFF na FIFA

HAYA MNAYAONAJE WANA JF/
 
Back
Top Bottom