TFF mpaka Sasa hawajatoa Tamko dhidi ya Bakhressa!

TFF mpaka Sasa hawajatoa Tamko dhidi ya Bakhressa!

Bos amepaniki, Kauli aliyotoa mmilikiwa Timu ya Azam ndugu bakhresa kwamba wanajitoa kwenye ligi na kuhamia Zanzibar ni kashfa kubwa sana.

Kashfa hii inaweza kukimbiza wawekezaji na watu kuacha kuangalia soka la Tanzania.

Kasfa hii lazma ijibiwe vikali, sijui alitaka Feisali apewe pongezi kwa utovu wa nidhamu aliofanya?

Inasemekana aliuziwa mechi ya nusu fainali CRDB na yeye akauza mechi ya NBC, akaaminishwa kwamba atakuwa bingwa wa CRDB, Sasa Leo mambo yamekuwa tofauti fala Kawa Azam kauza halafu yeye kabaki na makopo, ndiyo maanah ata FEI amepaniki kwa sababu aliona mechi ya nusu fainali CRDB akacheza halafu mechi kubwa ya NBC aka-kaa mbao ndefu kitambala bench, Manula bench, kwa hiyo Fei alijua maboss wake wamezunguka mbuyu na yeye akaona isiwe tabu akatengeneza tukio na kupata red card na Ile kilikuwa lengo lake, kwa hiyo wasimfokee REFA Wala bodi ya ligi.​
Wewe ni mjinga kabisa,boss wa azam wala hajasema anajitoa,alisema kama tff na bodi ya ligi hawaitaki timu yake basi hashindwi kuitoa na kuipeleka zanzibar na wala hajalitaja tukio la fei,uongo umekuzidi.Alichosema kipo mtandaoni kamsikiliza acha kujamba hovyo hapo,balahau we
 
Umeweka maneno yako kuleta ladha mdomoni mwako, mimi ni mdu wa mpira ukiach kazi yangu mahakamani, Usiwe mwongo kama yuyle aliyempa ushindi aliyepata kura yake mwenyewe.
 
Kabla yake hakukuwa na Ligi?
Hakuna pengo lisilo zibika.
Hata yeye akifa wanaweza kuja waridhi wakaachana na mpira na Uwanja ukawa Yard ya makonten ambapo infact inalipa kuliko mpira kiingilio ni 2000.
Mzee tuwe serious kidogo! Kabla ya udhamini wa Azam Ligi ilikuwa hivi?

Au tuseme umeanza kufuatilia Ligi kipindi hiki cha Azam?
 
Wewe ni mjinga kabisa,boss wa azam wala hajasema anajitoa,alisema kama tff na bodi ya ligi hawaitaki timu yake basi hashindwi kuitoa na kuipeleka zanzibar na wala hajalitaja tukio la fei,uongo umekuzidi.Alichosema kipo mtandaoni kamsikiliza acha kujamba hovyo hapo,balahau we
Mbongo na uzushi ni kama chanda na Pete. Ndio Hawa wanakuambia Morocco wamesema wao sio Waafrika. Ukimwambia leta ushahidi anakuletea kitu kingine kabisa.

Kama huamini endelea kumbana huyo jamaa akuletee ushahidi ni wapi huyo mmiliki ametaja tukio la Feisal.
 
Bos amepaniki, Kauli aliyotoa mmilikiwa Timu ya Azam ndugu bakhresa kwamba wanajitoa kwenye ligi na kuhamia Zanzibar ni kashfa kubwa sana.

Kashfa hii inaweza kukimbiza wawekezaji na watu kuacha kuangalia soka la Tanzania.

Kasfa hii lazma ijibiwe vikali, sijui alitaka Feisali apewe pongezi kwa utovu wa nidhamu aliofanya?

Inasemekana aliuziwa mechi ya nusu fainali CRDB na yeye akauza mechi ya NBC, akaaminishwa kwamba atakuwa bingwa wa CRDB, Sasa Leo mambo yamekuwa tofauti fala Kawa Azam kauza halafu yeye kabaki na makopo, ndiyo maanah ata FEI amepaniki kwa sababu aliona mechi ya nusu fainali CRDB akacheza halafu mechi kubwa ya NBC aka-kaa mbao ndefu kitambala bench, Manula bench, kwa hiyo Fei alijua maboss wake wamezunguka mbuyu na yeye akaona isiwe tabu akatengeneza tukio na kupata red card na Ile kilikuwa lengo lake, kwa hiyo wasimfokee REFA Wala bodi ya ligi.​

soma ulichokiandika
 
Hongera kwa andiko zuri sana kuhusu tuhuma ambazo zimetolewa na mlezi wa Azam Fc kuhusu mwenendo usiofaa wa ligi yetu.Umeeleza kushangazwa kwa nini mpaka sasa TFF au bosi ya ligi hawajamuita kwa mahojiano ndugu Jamal Bakhresa.
Jamal Bakhresa hawezi kufunguliwa mashtaka na kamati za TFF kwa sababu yeye sio kiongozi wa timu ya Azam Fc.
MzeeJamal Bakhresa ambaye ni mdogo wake na Mzee Saidi Bakhresa yeye ni mlezi wa timu ya Azm Fc.
Mmiliki wa timu ni Yusuf Said Bakhresa mtoto wa Mzee Said Bakhresa.
Viongozi wa timu ya Azam Fc nafasi zao ni kuanzia Nassor Idrissa ambaye ni Rais wa timu.
Abdulkarim Amin ‘Popat Makamu wa Kwanza wa Rais.
Pia wana Makamu wa Rais anayeshughulika na akademi ambapo nafasi hii iko chini ya Omary Kuwe.
Pia wana CEO wa timu ambaye ndiye mtendaji mkuu wa klabu.
Wana mkurugenzi wa Fedha na mwisho wana bodi ya klabu.
Sasa basi hawa ndio viongozi wa klabu ambao TFF na bosi ya ligi wanao uwezo wa kuwashitaki kama wamefanya kosa ambalo lina stahili kufunguliwa mashtaka.

Naomba ufahamu tuna kamati mbili za mpira wa mguu ambazo zina sifa za kuwa chombo cha kimahakama, hivyo kuanzisha kesi na kutoa hukumu ya kesi za mpira wa miguu.Miongoni mwa vyombo muhimu katika mfumo huo ni Kamati ya Maadili na Kamati ya Nidhamu. Ingawa kamati hizi mbili zinaweza kuonekana kuwa zinafanya kazi zinazofanana kwa sababu zote hushughulikia makosa na mwenendo usiofaa, majukumu yake hutofautiana kwa kiasi kikubwa.
Kamati ya Nidhamu Kamati hii hushughulikia matukio yanayotokea ndani au yanayohusiana na mashindano, kama vile:
Mchezaji kufanya mchezo wa rafu na kupewa kadi nyekundu.
Mchezaji, kocha au kiongozi kumtukana mwamuzi.
Timu kuchelewesha mchezo kwa makusudi.
Mashabiki kufanya vurugu uwanjani.
Klabu kushindwa kutekeleza taratibu za mashindano.
Kamati ya Maadili hushughulikia masuala yanayohusu uadilifu, tabia njema, uwajibikaji na uaminifu katika uongozi na uendeshaji wa mpira wa miguu.
Masuala yanayoweza kushughulikiwa na Kamati ya Maadili ni pamoja na:
Rushwa katika mpira wa miguu.
Upangaji wa matokeo ya mechi (match-fixing).
Migongano ya maslahi kwa viongozi.
Matumizi mabaya ya madaraka.
Vitendo vinavyoharibu taswira ya mpira wa miguu.
 
Simba nao walitaka wajitoe kwenye ligi, kwan hao TFF walisemaje?
 
Mzee tuwe serious kidogo! Kabla ya udhamini wa Azam Ligi ilikuwa hivi?

Au tuseme umeanza kufuatilia Ligi kipindi hiki cha Azam?
Nitake radhi kijana, mimini mama mwenye wajukuu, mpira nimeanza kufuatilia 1986 nikiwa mwanafunzi shule ya Msingi.
Nilikuwa shabiki wa Nyota Nyekundu, badae nikahamia Reli ya Morogoro baadae Ushirika ya moshi na sasa nipo Timu yetu ya Mahakama japo haijapanda ligi ila tunacheza na sisi vetersan.

1990 nilikuwa mshabiki mkuu wa Hassan Haffif na Zamoyoni Mogela, wanandinga wa Simba FC.
Ramadhani mackenzi akiwa golini pale yanga alitusumbua sana na ndio walitushusha daraja na timu yetu ya Ushirika ikafa.

Mimi ninajua mpira kabla mama yako hajachumbiwa!
 
Back
Top Bottom