TFF mnalifahamu hili?

ikhufa

Member
Apr 2, 2017
33
21
Kumekuwa na juhudi au hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha wanaongeza mapato yake na moja ya njia hizo ni kuhakikisha kuwa wanadhibiti mianya midogo midogo ya upotevu wa mapato.

Mnamo mwaka jana serikali kupitia waziri wa habari aliyekuwepo Mh. Nape Nauye walianzisha mfumo wa kielectronic wa kuingia uwanjani kuweza kuangalia michezo mbalimbali. ie njia ya kadi maalum.

Siku ya jana kulikuwa na mchezo wa VPL kiporo kati ya club ya Yanga wakiwakaribisha Toto Africa kutoka jijini Mwanza. Basi na mimi nilikuwa mmoja wa watanzania au wapenzi wa burudani waliokwenda kushuhudia mchezo huo.

Nilitoka nyumbani muda wa saa tisa kamili kutokana na haraka nliokuwa nayo ya kufika mapema uwanjani kwa bahati mbaya nilisahau kadi yangu ya selcome ambayo ningeitumia kuingia uwanjani. Lakini kwa bahati nzuri niliambiwa kuna huduma ya express yaani unakatiwa risiti bila kuwa na card japo ilinilazimu kuongeza sh 1000 zaidi ili nipate risit hii maana kiingilio kilikuwa 5000 mzunguko.

Basi baada ya kununua nikaelekea mlangoni ambapo hakukuwa na watu wengi sana lakini kama ilivyo kawaida hakukosi askari eneo la kuscan hizo card. Na kama kawaida yao wanakuwa very agressive hivyo hata kama huna kosa unakuwa huna amani maana jambo lolote atakalokwambia lazima atakukaripia.

Mimi nilifika eneo hilo askari aliyekuwa pale baada ya kuona nina risit bila kadi akanielekeza nitoke hapo nilipokuwa niende mlango mwingine ambao kulikuwa na askari wenzake wengi zaidi. Na nilipofika nikadakwa mkono wenye risit na mmoja wa maaskari hao na risiti kuchukuliwa nikaambiwa pita haraka so risit niliyokuwa nayo haikuwa scanned na nlifanya observation ya haraka haraka nikagundua mlango huo ndo unatumiwa na watu wenye risiti wengi.

Nilibaki na maswali kichwani ambayo sikupata majibu kamili moja lilikuwa je hizi risit za malipo wanazipeleka wapi? Au wanaenda kuwauzia watu wengine
NB; Hii sio mara ya kwanza kwenda kuangalia mpira nikasahau kadi lakini tofauti na jana safari iliyopita ilikuwa scanned na nikaingia.

WITO: Ninaiomba TFF ifuatilie suala hili maana serikali, vilabu na wao TFF watakuwa wanapoteza mapato.
 
Acha wajipigie bwana wakubwa wanapiga kwenye ndege ,escro nk hii nchi yetu sote acha nao wale
 
Shida ni vilabu vyenyewe, kwa nini havina viwanja vyake. Sidhani kama shida hii inaweza kutokea Azam Complex?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom